3D nadhani ni kati ya wale waramba viatu wa mafisadi au fisadi mwenyewe. Hata hivyo amepoteza muda mwingi kujibu 'propaganda' mfu kwa propaganda mfu na chafu. Hakuna la maana analotaka kusema. Anasema Slaa asituharibie nchi. Nchi iharibike mara ngapi iwapo inatawaliwa na wezi wa mchana wanaojulikana? Nchi iharibike mara ngapi inapobambikiwa rais atokanaye na ufisadi, uongo, usanii, uchakachuaji, udugu, kujuana, kuhongana na jinai nyingine nyingi?
Bahati mbaya sina muda, ningemjibu huyu gendaeka inavyopaswa. Muhimu ni kumpuuzia kwa vile tunajua ima ni fisadi mwenyewe ua ajenti wao. Hawa ni wachumia matumbo wayatumiayo kufikiri badala ya vichwa. Pole sana 3D.
Nimesikitishwa sana na kauli ya Mzee Mwanakijiji ya tarehe 5 November, 2010 saa 3:05 asubuhi: Angalizo kwa wana JF - Lugha ya matumizi ya nguvu haina nafasi ambayo katumia muda mwingi kujaribu kujenga hoja kuwa katika ulimwengu wa waliostaarabu lugha zinazochochea matumizi ya nguvu hazina nafasi.
Nakubaliana na hoja kuwa nchi yetu kama nchi nyingine yoyote inahitaji kuwa na amani. Lakini natofautiana naye pamoja na watu wenye msimamo kama wake wa Uchaguzi umeshapita, tuangalie mengine. Huu ni msimamo wa CCM (ambao ni wa hadaa). Nitaeleza.
CCM imekuwa mstari wa mbele kutumia vyombo vya habari hasa magazeti kumchafua Dr. Slaa na kumtusi. Magazeti kama Al-Huda yalifikia hatua ya kuchapisha picha za mafuvu ya binadamu yakidai Dr. Slaa kuchochea mauaji ya Mwembechai dhidi ya Waislamu. Magazeti kama Tazama, Taifa Letu etc yamekuwa yakimtukana Dr. Slaa na baadhi yao kugawiwa bure hasa yakiandika taarifa hasi juu ya Dr. Slaa. Gazeti la Serikali Habari Leo limemchafua sana Dr. Slaa. Gazeti la Serikali la Daily News lilitoa msimamo kuwa Dr. Slaa hatakuwa Rais wa tano wa Tanzania (Serikali kuu haikujitenga na kauli hii).
Mwishowe Magazeti ya Mwananchi na MwanaHalisi ndiyo yaliyotishwa kufungiwa badala ya Al-Huda na mengine. Baada ya Uchafuzi huu Magazeti haya sasa yanaombwa na Kikwete Kusaidia kutibu vidonda vya Uchaguzi. Ni kweli yatafanya hivyo kwa kuwa Kikwete anajua kabisa kuwa ukihitaji magazeti yabomoe wakati wa uchaguzi yatumie halafu uchaguzi ukiisha yatumie tena kujenga kwa kuwa Watanzania ni mazezeta na wanaamini sana magazeti.
Kikwete anajua kuwa ukitaka kushinda iba kura, tumia majeshi kutisha na kupiga watu, tume ikishakuweka madarakani kwa ghilba wapo akina Mwanakijiji, Pengo, Mokiwa na Getrude Lwakatare ambao wakiongea tu Kubalini matokeo, tunataka amani basi Watanzania watakubali. Na akina Mzee Mwanakijiji wanatumia technique ya lugha Katika ulimwengu wa wasomi ili ukitofautiana nao uonekane siyo msomi na mpenda machafuko.
CCM wana akili timamu na wanaona kila hatua inavyokwenda. Uchaguzi utakuja, ataibuka Mrema au Slaa au Lipumba, atapigwa zengwe, ataitwa mdini. Kama ni Lipumba akigombea basi magazeti ya Kikristo ya kihafidhina yatamtukana Lipumba na kumwita mdini na mtu asiye na ndoa (Ilitokea year 2000). Kisha kura zitaibwa. Watu wote (including viongozi wa dini na akina Mzee Mwanakijiji) wataona kuwa kura zimeibwa. CCM itashinda. Polisi watapiga watu wanaodaiwa kuwa wapenda fujo na wanaotumiwa na viongozi waroho wa madaraka (Akina Dr. Slaa). Kikwete ataapishwa akiwa amejeruhi nchi.
Watu watabaki na alama za wino wa kura (indelible ink) huku wakizomewa na kutajwa kama wapenda fujo, wasokubali kushindwa, wanaotumiwa na wanasiasa na akina Mzee Mwanakijiji wataenda mbali zaidi na kuwaita wasioelimika na waliojiunga JF juzi tu. Kuna memba wa JF ameshauri wana JF wachanga wapewe muda wa mwezi mmoja wa Kutazama kwanza hoja zinavyotolewa na wakongwe kabla hawajapewa nafasi ya kuchangia.! Sawa bwana.
Ikumbukwe kauli za kuzuia Watanzania kudai haki yao na kutaka wawe makondoo (siyo kondoo) ni kuzuia mabadiliko. Haisaidii kutumia miaka milioni moja kujadili nguvu za hoja wakati inamchukua mgombea siku mbili kuchakachua kura na uongozi.
Pole Dr. Slaa. Pole sana. Najua hukutaka kugombea Urais. Ulichukua fomu ya Ubunge. Kamati Kuu ya CHADEMA ikakubana sana ugombee Urais. Ukakubali. Umejenga hoja sana katika kampeni (kama akina Mzee Mwanakijiji wanavyodai wanapenda). Kura zako zimeibwa. Sasa akina Mzee Mwanakijiji waliokushangilia wanakwambia Uchaguzi umeshapita, tugange yajayo. Kwa maana fupi tu Dr. Slaa usituharibie nchi yetu.
Watanzania wanapenda vitu vizuri lakini hawapendi gharama. Kwaheri Mkoloni Mzungu, karibu Mkoloni Mwafrika. Historia itatuhukumu. Nakubaliana na mawazo tofauti na yangu (kwa hoja lakini).
Mungu Ibariki Afrika,
Mungu Ibariki Tanzania,
Nawasilisha.
3D - Ni mbinu gani za matumizi ya nguvu (violent methods) ambazo unafikiri zinafaa kutumika sasa hivi Tanzania kupinga matokeo ya uchaguzi? Na kati ya hizo ni zipi wewe uko tayari kuzitumia ili kufikia malengo ya kisiasa.
Mbinu ambazo zinatumika hata na wenzetu duniani ni:-
1.migomo ya wafanyakazi na wanafunzi
2.maandamano ya watu wote
hizi ni njia mbili ambazo zikitumika huwa zinaleta matokeo mazuri daima, mfano hugo chaves alivyopinduliwa wananchi waliandamana bila kikomo wakahama majumbani mwao wakahamia barabarani mwisho chaves akarudi madarakani,pia kumbuka afrika ya kusini namna wanachi walivyopigana kufa kupona kuupinga ubaguzi wa rangi na wakafanikiwa, mimi hiki kijineno cha amani naanza kukichukia kwa sababu ndicho kinachohalalisha zuluma kwa mtanzania.NIONAVYO MIMI WAKATI SASA UMEFIKA WATU TUAMUE KAMA WALIVYOWAHI KUAMUA WATU WA THAILAND HAPO TUTAFANIKIWA.KUMBUKA UPOLE WETU UNALETA DHULUMA KWETU NA SUBIRA YETU YA KUFANYA MAAMUZI SAHIHI NDO KASI YA KUIBIWA KWA RASILIMALI ZETU.TUUNGANE PAMOJA TUFANYE MAAMUZI YA PAMOJA ILI TUSHINDE KWA PAMOJA.
MUNGU IBARIKI AFRIKA,
MUNGU IBARIKI TANZANIA,
AMEN!
mimi niko tiyari kwa maandamano
Mimi hata vita naona ni sawa maadamu ni kudai haki. Kuna mazingira yanahitaji vita ili ulete mabadiliko. Japo vita ni gharama kubwa
mkuu hakuna anayepinga wazo lako hujasema tunataka violence sisi tumeesema tunahitaji kufanya maandamano na migomo ya amani,LAKINI KUMBUKA kuwa selikali hutumia jeshi kusawazisha mambo hapa ndipo NINAPOTAKA WATANZANIATUAMUE KAMA WALIVYOWAHI KUAMUA WATU WA THAILAND HAPO TUTAFANIKIWA.KUMBUKA UPOLE WETU UNALETA DHULUMA KWETU NA SUBIRA YETU YA KUFANYA MAAMUZI SAHIHI NDO KASI YA KUIBIWA KWA RASILIMALI ZETU.TUUNGANE PAMOJA TUFANYE MAAMUZI YA PAMOJA ILI TUSHINDE KWA PAMOJA.Asante Mkuu MM,
Swali lako ni sawa na kumuuliza mtu, "Una maoni gani ya kipuuzi uliyonayo kuhusu......." So ni swalia ambalo tayari liko biased. Ni sawa na watu wanaotoa hoja humu JF halafu wanasema, "Nasubiri maoni tofauti ya wasiopenda maendeleo."
Sasa nitajibu swali lako (sitajibu kuwa njia zangu ni violent):
Nashauri pawepo (na nitashiriki) na maandamano ya amani nchi nzima kupinga haya matokeo. Maandamano haya yaendelee hadi pale jumuiya ya Kimataiifa na serikali yenyewe itakapokuwa tayari kukaa chini kujadili hali iliyopo. Wasomi wa vyuo vikuu, sekondari wasiingie madarasani hadi pawepo na mazungumzo juu ya uchaguzi huu.
Nikumbushe tu kuwa violence hutokea pale serikali zinapowanyima wananchi haki ya kupinga kile wasichokiafiki. Kama violence itatokea katika mchakato huu itakuwa imesababishwa na serikali. Siungi mkono mawazo ya "Acha tu."
COST of development mkuu ni siyo sababu ya vita ila ni matatizo ya mipango yetu na matumizi mabaya ya rasilimali zetu hebu ona aibu kwa huo usemi wako RWANDA wametoka kwenye mapigano juzi tu mbona leo wako juu zaidi yetu? mkuu fikiri kwa kina utaona nguvu ya umma ndo italeta suluhisho la kweli.You are not serious. Vita vya Kagera tu ambavyo tulipigana kwa muda mfupi cost us a decade of development. Ushawahi kufika South Sudan, DRC, Liberia? Ukipata nafasi japo youtube uone mziki wa vita ukoje.
POa basi, unataka vita. Sasa nani apigane na nani? Chadema na CCM? with your 20% of 5 millions you think you have enough to kukusanya jeshi. Poa, let say unalo jeshi--mimi shemeji zangu ni Chadema damu, ingawa tunalewa Bar moja, sasa hapo vita itaanzaje? Acha mawazo haya babu.
Asante Mkuu, nashangaa kwanini akina MM hawaoni mambo rahisi kama haya!!
COST of development mkuu ni siyo sababu ya vita ila ni matatizo ya mipango yetu na matumizi mabaya ya rasilimali zetu hebu ona aibu kwa huo usemi wako RWANDA wametoka kwenye mapigano juzi tu mbona leo wako juu zaidi yetu? mkuu fikiri kwa kina utaona nguvu ya umma ndo italeta suluhisho la kweli.
. But Jamii Forum is a virtual world, not the real one.
wajerumani ndo waanzilishi wa vita vyote vya dunia lakini leo ndo wana lead economy of euro.pia hata uganda yenyewe walipigana na sisi lakin mbona wao wana uafadhali. kaa chini jiulize kwanini maskini ilhali tuna rasilimali kibao? utagundua hawa watawala na CCM ndo source wala sio vita vya idi amin. pia ninapotoa mfano wa rwanda ninajua kabisa kuwa ina idadi ndogo ya watu kuliko sisi ila kumbuka hapa ninitaka tuangalizie wenzetu imekuwaje wameweza kurecover haraka kutoka vitani wakati sisi miaka hamsini bado tunadidimia tu.Let us assume kwamba Rwanda wako juu kama unavyodai. That is one county out of how many? Pili, Kagame akifa leo, Rwanda is in chaos. Tatu, hakuna freedom of speech Rwanda. As the matter of fact sisi tungekuwa Rwanda, Dr. Slaa couldn't even get this far. Nne, Rwanda has 6-8 million people, compared to 40 of ours. Tano, Kagame kawekwa na western power as a gateway to get DRC minerals ndio maana he has been given impunity for all repression act against Hutu and we have been fed with this image of a liberator (but in reality, Kagame is a monster) tafuta wahutu wa Rwanda uwaulize leo. And there is no independent journalism in that country.
You still want to take Rwanda's direction?
Kaka, migomo ya wafanyakazi na maandamano ya wanafunzi will only work if you get the high turn out. The high turn out depends on the interest ya wanafunzi na wafanyakazi. Kwa Tanzania yetu hii ya leo, unategemea wafanyakazi wangapi ni wanachama wa Chadema? na ni wanafunzi wangapi wanaifagilia Chadema. Your assumption is Chadema is a mighty strong party, which is contrary to the truth. Ukiitisha maandamano, I guarantee you, utapata wahuni tu, who will expect some sort of mshiko at the end. Unless hayo maandamano yawe Jamii Forum, then you have a chance. But Jamii Forum is a virtual world, not the real one.
Kuna memba wa JF ameshauri wana JF wachanga wapewe muda wa mwezi mmoja wa Kutazama kwanza hoja zinavyotolewa na wakongwe kabla hawajapewa nafasi ya kuchangia.! Sawa bwana.
.
'No Court shall have jurisdiction to inquire into anything done by the Electoral Commission in the exercise of its functions according to the provisions of this Constitution.'