Kwahiyo Zimamoto likiunganishwa na Polisi ndo vitendea kazi vitapatikana? Hoja hapa ni kuongeza vifaa/vitendea kazi,Siku za nyuma kidogo nilipiga simu jeshi la zimamoto na katika maongezi yetu na askari aliyekuwa mapokezi nikamuuliza ni kwanini huwa wanachelewa kufika eneo la tukio panapotokea ajali ya moto na hata wakifika huwa hakuna msaada wanaotoa.
Alichonieleza ni kuwa sio kama wanapenda kufanya hivyo bali hawana vitendea kazi vya kutosha na hivyo vilivyopo huwa mara nyingi huwa vipo kwenye garage na malipo huwa ni changamoto sana kiasi kwamba huwa wanashindwa kurespond majanga yanapotokea.
USHAURI
Najua fika jeshi la zimamoto limeanzishwa kwa Sheria za Bunge, napendekeza serikali ilivunje mara moja jeshi ili na kurudishwa kuwa kitengo cha jeshi la polisi maana naona fika askari wa jeshi ili la zimamoto huwa wapo idle sana kiasi kwamba wanaishi kwa mazoea maana hakuna kazi wanazofanya.
Tumeshuudia mkoani Kilimanjaro zaidi ya marambili soko la mbuyuni kuungua ila mara zote hizo jeshi la zimamoto mkoa wa Kilamanjaro huwa limeshindwa kutekeleza majukumu yake na mbadala wake kitengo cha zima moto kiwanda cha sukari TPC ndio huwa msaada.
Kurudishwa na kuwa kitengo ndani ya Jeshi la polisi kunaweza kuboresha ufanisi na kama hakuna majanga ya moto askari hawa wanaweza fanya majukumu mengine kama kuimarisha usala wa raia na mali zao.
Nawasilisha.