Waziri wa ulinzi na jeshi la kujenga taifa azindua kituo cha afya Biharamulo

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Sep 6, 2020
789
499
WAZIRI WA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA AZINDUA KITUO CHA AFYA BIHARAMULO

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Dkt. Stergomena Lawrence Tax, tarehe 03 Mei, 2024 amezindua Kituo cha Afya. Waziri Tax alishuhudia pia makabidhiano kati ya Wizara na Kikosi cha Majengo ya kuishi Maafisa na Askari. Kwenye uzinduzi huo, Waziri Tax amesema kuwa Kituo hicho cha Afya ni muhimu na hatua ya kujivunia kwani kitatoa huduma za tiba kwa wanajeshi, familia za wanajeshi na wananchi wanaoishi maeneo jirani.

Akiongea na Maafisa na Askari pamoja na raia mara baada ya kukata utepe na kuashiria uzinduzi huo, Waziri Tax amemshukuru kwa dhati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuliwezesha Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania. Aidha, amewapongeza viongozi, maafisa na maaskari waliosimamia na kushiriki katika ujenzi huo kuhakikisha kuwa mradi huo unakamilika kwa vigezo na kuzingatia thamani ya fedha. Akasema "Dhamira ya Mheshimiwa Rais na Amiri Jeshi Mkuu Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan ni kuliwezesha Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi na kuhakikisha upatikanaji wa huduma zinazohitajika" alisema Waziri Tax.

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa amewashukuru pia Maafisa na Askari kwa kazi kubwa na nzuri wanayoifanya kwa kujituma, weledi na uhodari katika utekelezaji wa majukumu yao na akasisitiza umuhimu wa kusimamia na kutunza majengo yaliyozinduliwa, vifaa tiba na visima vilivyokabidhiwa ili vidumu na kuendelea kutoa huduma bora kwa muda mrefu.

Aidha, Waziri Stergomena Tax amemshukuru Mkuu wa Wilaya na Kamati ya Ulinzi na Usalama na taasisi zote za Serikali zilizoshiriki na kufanikisha ujenzi wa miradi hiyo, na kuwataka kuendeleza ushirikiano ili kuimarisha ulinzi na huduma kwa ustawi wa wapiganaji na raia kwa ujumla.

Kabla ya kukata utepe wa kuzindua rasmi jengo la la Kituo cha Afya cha K-9 Waziri Tax alipata fursa ya kutembelea jengo hilo na kupata maelezo na kupanda mti wa kumbukumbu katika eneo la zahanati.

20240504_113749_InSave_0.jpg
20240504_113749_InSave_1.jpg
 
Back
Top Bottom