Kutokana na kukithiri kwa habari za Walimu ‘kuwapa kipigo’ wanafunzi, Wanahabari hawajafanya kazi yao vizuri

Kiranja wa jamii

JF-Expert Member
Jan 2, 2023
228
552
Kwa siku za hivi karibuni vyombo vya habari vimeripoti taarifa za Walimu kutoa adhabu inayoonekana kupitiliza kwa wanafunzi jambo linalozua taharuki kwenye jamii na walimu kushushiwa kila aina ya lawama

Binafsi siungi mkono walimu kuadhibu wanafunzi kupitiliza. Hata hivyo kwa yaliyoripotiwa hivi karibuni binafsi naona kuna namna vyombo vya habari vinataka kuuaminisha umma kwamba walimu wa siku hizi hawana huruma na watoto wala hawatumii akili

Kwanini nasema hivi?

Ukiangalia namna story inavyoripotiwa utagundua kwamba anayeripoti yeye ameona tukio la mwanafunzi kuumizwa kisha akaruka kwenye hitimisho la kutupa lawama kwa Mwalimu bila kutaka kujua historia ya mtoto, Kama anaishi na wazazi, matukio yake ya nyuma, hadi kufikia hatua hiyo kulitokea nini? Haya yote hakuna anayekumbuka kuyaangalia

Sasa hivi karibu kila mwanafunzi anaenda sekondari. Hapa wamo wanaopenda na wasiopenda shule. Hawa wasiopenda shule utakuta kuna wacheza kamari humohumo, wavuta bangi, wanaobeti na matukio mengi ya ajabu ajabu

Baada ya siasa kuingilia elimu siku hizi imekuwa vigumu sana kufukuza wanafunzi shule na kamati za nidhamu na hata bodi ya shule. Sababu kubwa inayotumika hapa ni kwamba kwa umri wao wakifukuzwa kwenda mtaani wataenda kufanya nini huko?

Hii imepelekea shule nyingi kuwa na watoto wajeuri, wahuni na wasiowajibika Kama wanavyotarajiwa.

Kuna baadhi ya wanafunzi wako shuleni lakini hata wanafunzi wenzao hawatamani kuwaona

Kwa mfano, hii habari ya huyu mwanafunzi aliyedokoa maandazi swala lake linaweza kuonekana la ajabu kwa walimu kumshambulia.

Lakini kabla ya kuwahukumu walimu, tunatakiwa tujue background ya mtoto kwasababu mtoto ambaye hajawahi kuonywa mara kadhaa, hana tabia za ujeuri shuleni anapofanya kosa anazua mshangao na hivyo si rahisi kuadhibiwa kwa namna inayoogopesha

Jambo lingine, tutambue kabisa watoto majeuri huwa hawakubali adhabu kirahisi. Lazima atataka kupambana na walimu tu! Sasa anapotaka kupambana ndio shida inapoweza kutokea. Ogopa sana kumuadhibu mtoto mjeuri anayetaka kuonyesha ujeuri wa kupambana na wewe.

Ushauri wangu ili kuwaondoa walimu kwenye hili kadhia, ni vema wizara husika ziondoe kabisa adhabu mashuleni hasa hii inayohusisha viboko kwasababu siku hizi wanaiita ukatili

Naamini tutapata madhara kwa Sasa tukiondoa fimbo lakini huko mbele mazingira yatatutengeza na tutazoea tu. Hainasababu ya walimu kuanza kujengewa chuki kwenye jamii kwa watoto hawa ambao hata jamii imeshindwa kuwalea.

Leo utakuta watoto kibao wamejazana kumbi za starehe hadi asubuhi wakati getini pameandikwa chini ya miaka 18 hawaruhuwi

Leo utakuta watoto hadi na sare za shule wamepanga foleni kwenye mashine za kubeti muda wa masomo na jamii inaangalia

Leo utakuta watoto wanauziwa vilevi na watu wazima na wanatumia mbele yao bila woga

Jamii inaangalia, Serikali inaangalia, wazazi wanaangalia!

Ni lini mwanafunzi anayewaza mikeka yake atamsikiliza Mwalimu?

Ni lini mwanafunzi anayekesha disko atamsikiliza Mwalimu?

Ni lini mwanafunzi anayevuta bangi, anayejihusisha na ngono na watu wazima atamsikiliza Mwalimu?

Waandishi wa habari wanalojukumu la kupita mashuleni, kufanya uchunguzi kwa kuona wenyewe, kuongea na wanafunzi, walimu na wanajamii kubaini uhalisia wa wanayopitia walimu kwenye kujaribu kurekebisha tabia za wanafunzi

Tukumbuke wanaotoa matamko watoto wao wamelelewa vizuri na hawasomi shule hizi ambazo walimu wanakunjana na wanafunzi

Tukiishi kwa kutegemea matamko na comment za Instagram hatutoboi kwani miongoni mwa wanao comment ndo hao hao wanaohitaji msaada
View attachment 2520926
 
Back
Top Bottom