Kutoka Mtwara katika Picha

PICT0246 i.jpg

PICT0247 i.jpg

PICT0248 i.jpg

PICT0249 i.jpg
Angalia wakina mama hawa walivyo busy wakitafuta vitoweo. Jambo lililonishangaza ni kwamba sikuona wakina baba wengi katika zoezi hili la uvuvi wa aina hii bali wakina mama walikuwa wengi sana. Kweli wamama ujituma kazi nyingi sana na kipato chao huwa juu sana. Kwa nini wakina baba hawaonekani sana zaidi ya kuwakuta kwenye mnazi!? hiyo wanaweza kujibu wenyewe!

PICT0252 i.jpg
Hii ni barabara nilipita nikienda Msimbati.
 
PICT0256 i.jpg
Hii ni barabara ya kwenda Msimbati. Eneo hili ndilo lililo na utajiri wa gesi. Hapa pamefanywa kama hifadhi ya taifa. Lakini barabara sijui kwa nini hawakuijenga vizuri maana kule baharini pana utajiri mzuri ajabu. Paweza kuwa sehemu nzuri sana kitalii. Hata hivyo kama kawaida serikali zetu hazijaona umuhimu huo pamoja na kwamba kuingia eneo hilo unalazimishwa kulipa shilingi 2,000.= kama wewe ni mtz.

PICT0254 i.jpg
Huu ni ufukwe nilikutana nao wakati nakwenda Msimbati. Angalia mikoko ilivyopamba ufukwe wenyewe. Sehemu nyingine za fukwe niliona wakivuna chumvi. Katika kuvuna chumvi wao utengeneza mataruma kama yale ya kulimia mpunga:D
PICT0257 i.jpg
Hiki ni kituo cha Polisi pale Msimbati. Eneo hili ni mali hivyo ulindwa sana. Hongera jeshi la polisi.

PICT0258 i.jpg

PICT0259 i.jpg
Pamoja na utajiri wote uliowazunguka wakazi hawa wa Msimbati wanaishi maisha ya kifukara tu kama unavyoona. Sijui kama wanajua ni utajiri kiasi gani unachotwa jirani tu na maeneo yao. Angalia tu nyumba wanazoishi!
 
PICT0260 i.jpg

PICT0261 i.jpg
Hapa ndio sehemu ya Msimbati. Maeneo jirani na Mnazi bay.

PICT0263 i.jpg
Hii ni barabara iliyo ndani ya hifadhi. Pamepandwa minazi na mikorosho ndani ya hifadhi. Eneo zima ni mchanga mtupu na kama si juhudi za wawekezaji kuweka wavu maalum juu ya mchanga magari yasingepita. Lakini hapa ni barabara ya mchanga iliyowekwa wavu kama kilometa ishirini na huna haja ya kutumia 4wheel. Safi sana wawekezaji.

PICT0267 i.jpg

PICT0268 i.jpg
Hizi ni beach pale mnazi bay jirani kabisa na kituo cha kuzalishia gesi toka baharini. Ni moja ya fukwe nilizopenda na kutamani sana. Huwezi kulinganisha na fukwe za Dar zilizojaa uchafu na harufu kali kabisa. Kama zingeweza kuamishiwa Dar hizi jinsi zilivyo nzuri na safi..........!?!@&

PICT0269 i.jpg
 
Huu uzi ni wa mwaka 2009 miaka kama 11 hivi iliyopita. Wakati huo Mtwara ilikua inachipukia kuja juu. Leo siyo haba japo kumedidimia tena baada ya mambo ya gesi kupoa kabisa.
Kama mdau au wadau ikiwemo mleta mada akienda tena anaweza kuwa na picha nyingi na nzuri kuliko hizo. Kwa sasa anaweza kupata BNN ROYAL Hote,Cashewnut Hotel,LUWA EVERGREEN HOTEL,TIFFANY DIAMOND HOTEL,KIWANDA CHA DANGOTE, Vinu vya kuchakata Gesi kwa ajili ya Mtwara kule Kilambo,KIWANDA CHA CHEMICAL ZA WATAFUTA GESI,BUSTANI/MANDHARI NZURI PALE MZUNGUKO MNARANI,TAA ZA KUONGOZA MAGARI PALE BIMA(ingawa siyo issue sana,ila kwa kuwa ipo miji haina hata moja,nasi nayo siyo haba) nk nk nk.
Tutashukuru kama mtu atajitolea kuziweka humu.
Hii itasaidia kuwaelimisha watu ambao hawajafika Mtwara wapate elimu ya nini hasa kipo Mtwara

Ni matumaini tutapata mwendelezo wa picha kati ya zile za mwaka 2009 na leo hii 2021.
Enzi hizo Mashujaa Park, Tilla Park hazikua nzuri kama leo, hakukua na Naf Beach, Tiffany, BNN Royal, Shangan Apartments, Chuno road, Dangote, Luwa Evergreen, Shooters nk

Sent using Jamii Forums mobile app
 
i795_PICT0091i.jpg

Hii ndio barabara inatokea Lindi kuja Mtwara!

i796_PICT0093i.jpg

Magomeni Mnadani. Ni lini vijana hawa watajengewa soko zuri kwa ajili ya biashara yao? Ebu fikiri akitokea mwehu mmoja wa kuwasha moto vibanda hivi je hasara kiasi gani itawapata vijana hawa?

i797_PICT0104i.jpg

Nilifurahi kuona hair cutting Salon za chini ya mwembe. Vijana mnaona? msisingizie mgao wa umeme kazi mtindo mmoja hata kama hakuna umeme. Angalia jamaa anazo mpaka uniform zake na wateja wake!

i798_PICT0121i.jpg

Vijana wamejiajiri kuuza hata maji mitaani.

i799_PICT0123i.jpg

Mibuyu inapendezesha mandhali.

i800_PICT0154i.jpg

Hii ni sehemu ya mbele ya Boma Hotel. Hotel hii iko Mikindani. Mikindani ni eneo lililosheheni majengo ya zamani sana(Maghofu). Hapa palikuwa ni makazi ya waarabu na palikuwa na soko la utumwa kabla halijasambalatishwa na Dr Livingstone. Na majengo ya hii hotel inasemekana yalijengwa miaka ya 1890's na zamani ilikuwa ghofu baada ya serikali kushindwa kuiweka katika hali ya kutumika. Niliambiwa kuwa iliwahi kuwa hata chini ya umiliki wa jeshi la Polisi lakini nao walishindwa kulikarabati jengo na serikali ikampa mwekezaji toka Uingereza ambaye kalitengeneza vizuri sana. Ni hotel kubwa kwa Mtwara.

i802_PICT0160i.jpg

Hiki kifaa ni sehemu ya mizinga iliyokuwa ikitumika katika vita ya wajerumani na waingereza na kimeifadhiwa pale nje ya hotel ya Boma kama ukumbusho kwa kuwa sehemu hiyo ilitumika katika vita hiyo.
Admin mbona picha hazifunguki?
Au zilipata virus?
Tunaomba muzirejeshe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
lazima tukubali kuwa toka enzi za mwalimu mikoa ya kusini iliachwa nyuma kimaendeleo makusudi hususan mtwara kwa kisingizio eti cha vita ya msumbiji ikawa haiendelezwi zaidi ya kuwa na makambi na vituo vingi vya wapigania uhuru,ukibahatika kufika nachingwea nenda farm 17 ukajionee jumba la Samora Machel lingeweza hamishwa nadhani lingeletwa Dar liwe makumbusho,nilisoma mtwara miaka ile ya sabini kila shule ya msingi ilikuwa na Handaki nakumbuka hayati mwalimu Nyerere alitembelea mtwara akaingia ktk handaki letu shule ya msingi chikongola.Amini usiamini vijana wa rika lile toka Kusini hasa Mtwara tuliiva kisiasa na kimapinduzi ndiyo hawa akina john komba ,nchimbi na wengine wengi walioibuliwa na marehemu mzee mnauye acha masihara tulikuwa mahodari wa kuzama ktk mahandaki ndege ikipita shule nzima inabaki tupu,tumecheza paredi na kuimba nyimbo za kimapinduzi siku hizi hawawezi,ila tuliachwa watupu
Hii kitu ipo kweli pale Chikongola hadi leo? Mkuu ndo nasikia leo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa hiyo, kuhusu muda kwa mabasi yanayoenda Mtwara mjini na baashi Masasi unayapata mpaka saa 8 pale Temeke Sudan
 
Maeneo mengi ya mipakani na hasa ambako kulikuwa na vita vya ukombozi wa nchi jirani na Tanzania minara ya jinsi hii imejengwa kama kumbukumbu ya wapiganaji wetu. Kama inavyoonyesha mnara huu uliopo uwanja wa mashujaa Mtwara.

Baba huyu amepozi na Samaki wake akitoka kuvua. Angalia na wakina mama wale mbele yake nao wanatoka kutafuta samaki hasa kwa ajili ya biashara. Samaki Mtwara ni wengi na biashara hii inafanyika kwa wingi na hasa wakina mama wanaouza samaki wa kukaanga. Mkoa una utajiri mkubwa wa samaki.

Mibuyu ni miti inayoupendezesha mji huu wa Mtwara kwani imetapakaa kila mahali.

Uvuvi ni sehemu ya maisha ya watu wa Mtwara. Lakini hapana viwanda vya Samaki kama vile vilivyojazana Kanda ya ziwa. Kwa nini?

Kama kawaida usafiri wa Bajaj ndio usafiri wa kutumainiwa na wakazi wa mji wa Mtwara. Hakuna daladala kama za Daresalaam.
Hii dude ilianzishwa miaka 13 iliyopita. Muanzisha uzi hatujui hali yake ila abarikiwe sana. Bahati mbaya picha nyi gi ziliziwekwa miaka hiyo hazifunguki tena. Kwa sasa twaongeza Kutoka Mtwara katika Video:

 
Back
Top Bottom