Kutoka Mtwara katika Picha

Kaa la Moto

JF-Expert Member
Apr 24, 2008
7,903
1,053
Maeneo mengi ya mipakani na hasa ambako kulikuwa na vita vya ukombozi wa nchi jirani na Tanzania minara ya jinsi hii imejengwa kama kumbukumbu ya wapiganaji wetu. Kama inavyoonyesha mnara huu uliopo uwanja wa mashujaa Mtwara.

Baba huyu amepozi na Samaki wake akitoka kuvua. Angalia na wakina mama wale mbele yake nao wanatoka kutafuta samaki hasa kwa ajili ya biashara. Samaki Mtwara ni wengi na biashara hii inafanyika kwa wingi na hasa wakina mama wanaouza samaki wa kukaanga. Mkoa una utajiri mkubwa wa samaki.

Mibuyu ni miti inayoupendezesha mji huu wa Mtwara kwani imetapakaa kila mahali.

Uvuvi ni sehemu ya maisha ya watu wa Mtwara. Lakini hapana viwanda vya Samaki kama vile vilivyojazana Kanda ya ziwa. Kwa nini?

Kama kawaida usafiri wa Bajaj ndio usafiri wa kutumainiwa na wakazi wa mji wa Mtwara. Hakuna daladala kama za Daresalaam.
 
Ma miss Mtwara wamepozi baada ya kumuona mpiga picha.=:)

Pweza ni mboga safi na wanapatikana kwa wingi pale Mtwara. Jamaa anawatayarisha kuwaweka katika soko.

Hizi ni boti za uvuvi za Kitanzania. Je huu ndio uvuvi wa kisasa tuonaosoma kwenye zile tunaita sera nzuri za vyama vyetu? Kweli tutaendelea kama tunawaacha wavuvi watumie zana kama hizi katika uvuvi? Kwa mbali laonekana soko na mgahawa wa wavuvi.

Mitaa ya Mtwara. Naweza kushukuru Manispaa ya Mtwara Mikindani kwa kutengeneza barabara zao nyingi kwa lami. Na hata zile za udongo ziko katika hali nzuri.

Hili si Bango ila ni mlango wa uwanja wa mpira wa Namfua stadium pale Mtwara. Soma ujumbe ucheke mwenyewe. Sijui kwa nini wameandika wakihusisha rangi za chama kile. Au nao ni mmoja wa viwanja vilivyodhurumiwa?

Barabara ni safi na za lami na wamejitahidi sana hata kuzitengenezea mitaro. Hongera viongozi wa manispaa ya Mtwara Mikindani.

Hii ni bara bara ya udongo lakini nzuri. Na hali ya usafi wa mji ni bora kuliko Kigoma. Nadhani wangewaleta watendaji wa Kigoma kuja kujifunza usafi hapa maana usafi hauitaji pesa ya kigeni.
 
Barabara Safi ya lami ikiwa na mitaro tena na mitaro ikiwa misafi.

Kanisa la Katoliki Mtwara

Bajaj zikisubiri abiria. Dreva mmoja alinidokeza kuwa anatakiwa kuwasilisha kwa tajiri yake shilling 13,000/= kila siku. Bajaj zote zimesajiliwa na Manispaa na kupewa namba za utambulisho.

Hapa ni Nachinondo kwenye klabu ya pombe ya kienyeji. Ajabu kubwa ni kwamba saa 1 asubuhi tayari kuna watu wanakunywa pombe. Saa ngapi wanafanya kazi sijui. Ni ajabu pia pamoja na walevi pamejaa pia watoto wadogo, hapa malezi yanakwenda kwendaje? wale wadau wa haki za watoto tuambieni kama ni sawa. Klabu hii inaendeshwa na manispaa.

Mji umepambwa na maua. Hongera sana Manispaa ya Mtwara Mikindani. Hapa ni eneo linaitwa Mnarani .

Mchicha ni moja ya kilimo cha kujipatia kipato cha ziada.

Hapa ni Magomeni mnadani Mtwara mjini. Hawa jamaa wanauza nguo za mitumba kwa bei ya mnada. Ujasiliamali huo. Sijui hawa wote ni kampuni moja?

Hili ni eneo la Magomeni Mnadani. Watu wako busy sana wakinunua nguo.
 
Kwa kweli nimezipenda picha. Ila mwenyepicha ameweka watermark kubwa mno ya copyright mpaka inaharibu hata mwonekano wa picha. Angepunguza kidogo tu ingelikuwa bado na maana na picha bado zingeonekana mwanana.
 
Kwa kweli nimezipenda picha. Ila mwenyepicha ameweka watermark kubwa mno ya copyright mpaka inaharibu hata mwonekano wa picha. Angepunguza kidogo tu ingelikuwa bado na maana na picha bado zingeonekana mwanana.
Loh! samahani Steve D. Nimezoe ku watermark kazi yangu lakini utangundua niliacha na picha nyingi zilizopo hapa na zingine zaja hazitakuwa/hazitakuwa na watermark. Sorry kwa hili kama limekukwaza.
MF
 
tafadhali leta na picha za akina dada wa makamo (19 - 30) kutoka Mtwara. Waombe ridhaa wasepe kwenye ukumbi wa jamii. :)
 
shukran nyingi hata mimi nitafurahi kama utaondoa hii water mark na pia umenikumbusha miaka yangu niloishi hapo Mtwara, karinbu na kanisa la Parish nafiokiri ndio lenyewe kwenye picha jee FIN club iko bado ? nitafurahi kuona picha za historical sites za Mikindani pia kwenye majengo ya historia .pia kama kuna uwezekano wa kuwasiliana nje ya ukumbi nitafurahi pia namaskarblue@gmail.com
 
shukran nyingi hata mimi nitafurahi kama utaondoa hii water mark na pia umenikumbusha miaka yangu niloishi hapo Mtwara, karinbu na kanisa la Parish nafiokiri ndio lenyewe kwenye picha jee FIN club iko bado ? nitafurahi kuona picha za historical sites za Mikindani pia kwenye majengo ya historia .pia kama kuna uwezekano wa kuwasiliana nje ya ukumbi nitafurahi pia namaskarblue@gmail.com
Picha za Historical buildings Mikindani zipo zaja. Uwe na Subira.
 
Mkuu FM heshima mbele,

Mimi je unaonaje kwa mtu anaependa kuweka vitega uchumi Mtwara panafaa.

Panaonekana ni pazuri sana na kuna lots of opportunities.
 
Mkuu FM heshima mbele,

Mimi je unaonaje kwa mtu anaependa kuweka vitega uchumi Mtwara panafaa.

Panaonekana ni pazuri sana na kuna lots of opportunities.

Yep, bila kusahau the nutritious-beefy samaki nchanga!!
 
Ahsante Mchukia Fisadi,

Picha zimenikuna hususa za kule mikindani na pia magomeni. je huna picha za kule Mdenga na Maji, Raha Leo, Shangani nk?....

Mtwara mpaka ufike ndiyo utafahamu uzuri wake! Pia nawasifia wenyeji wa mtwara... mkifahamiana tu ushakuwa Somo! (yaani rafiki), yaani ni waungwana na hawana makuu.

Je ulifanikuwa kula nyedi?

Je, Ulifanikiwa kufika kwa St Benedictine Mission?- Kwa Father Edifonse? (((pia kuna Father Buchard? bila shaka Muumba atamlani kama alikuwa hajamlani huyu!!))))
 
i795_PICT0091i.jpg

Hii ndio barabara inatokea Lindi kuja Mtwara!

i796_PICT0093i.jpg

Magomeni Mnadani. Ni lini vijana hawa watajengewa soko zuri kwa ajili ya biashara yao? Ebu fikiri akitokea mwehu mmoja wa kuwasha moto vibanda hivi je hasara kiasi gani itawapata vijana hawa?

i797_PICT0104i.jpg

Nilifurahi kuona hair cutting Salon za chini ya mwembe. Vijana mnaona? msisingizie mgao wa umeme kazi mtindo mmoja hata kama hakuna umeme. Angalia jamaa anazo mpaka uniform zake na wateja wake!

i798_PICT0121i.jpg

Vijana wamejiajiri kuuza hata maji mitaani.

i799_PICT0123i.jpg

Mibuyu inapendezesha mandhali.

i800_PICT0154i.jpg

Hii ni sehemu ya mbele ya Boma Hotel. Hotel hii iko Mikindani. Mikindani ni eneo lililosheheni majengo ya zamani sana(Maghofu). Hapa palikuwa ni makazi ya waarabu na palikuwa na soko la utumwa kabla halijasambalatishwa na Dr Livingstone. Na majengo ya hii hotel inasemekana yalijengwa miaka ya 1890's na zamani ilikuwa ghofu baada ya serikali kushindwa kuiweka katika hali ya kutumika. Niliambiwa kuwa iliwahi kuwa hata chini ya umiliki wa jeshi la Polisi lakini nao walishindwa kulikarabati jengo na serikali ikampa mwekezaji toka Uingereza ambaye kalitengeneza vizuri sana. Ni hotel kubwa kwa Mtwara.

i802_PICT0160i.jpg

Hiki kifaa ni sehemu ya mizinga iliyokuwa ikitumika katika vita ya wajerumani na waingereza na kimeifadhiwa pale nje ya hotel ya Boma kama ukumbusho kwa kuwa sehemu hiyo ilitumika katika vita hiyo.
 
Mkuu FM heshima mbele,

Mimi je unaonaje kwa mtu anaependa kuweka vitega uchumi Mtwara panafaa.

Panaonekana ni pazuri sana na kuna lots of opportunities.
Panafaa mkuu.
Wana umeme wa hakika kabisa sasa hivi tokana na gesi ya mnazi bay.
Lakini bahari na beaches zake pia zinavutia kuliko kawaida.
Uvuvi unaweza kuwa kitega uchumi kingine kizuri.
Wana karibu kila zao lakini wanavuna chumvi ambayo ni lulu kama vile waarabu wanavyojivunia mafuta. Kwani nani anaweza kula bila chumvi? na wanayo minazi na mikorosho kibao.
Bara bara ni nzuri, hasa baada ya kile kipande kidogo cha kilometa 60 ambacho kiko under construction kwisha, kwenda huko itakuwa ni raha kabisa.
Lakini kuna watu wengi sana jambo ambalo linaonyesha kuwa unaweza kufanya biashara.
Kumbuka ni mpakani pia.
Wana bandari.
Kwangu naona panafaa.
 
i803_PICT0164i.jpg

Hii ni nguzo iliyo ndani ya hotel ya Boma kule Mikindani ambayo inasemekana ni moja ya nguzo nzee sana lakini imara ambayo haijaharibika hadi leo. Imejengwa kwa mawe na udongo tu.
 
i804_PICT0165i.jpg

Huu mlango umetengenezwa mwaka 1895 na bado upo na unafanya kazi hapo hotelini. Haujaoza!
Wenzetu walitumia teknolojia gani?

i805_PICT0166i.jpg

Entrance ya Boma hotel

i806_PICT0172i.jpg

Swimming pool ya hotel ya Boma

i807_PICT0175i.jpg

Maana ya Boma zamani ilimaanisha sehemu palipokuwa na mahakama. Hii hapa ndiyo ilikuwa court room na hicho ncdicho kilikuwa kiti cha hakimu wa nyakati zile.

i808_PICT0176i.jpg

Barabara zinazopita ndani ya maeneo ya Boma hotel

i809_PICT0177i.jpg

Sehemu za mapumziko pembeni mwa swimming pool

i810_PICT0184i.jpg

Kitanda ndani ya hotel ya Boma.
 
Back
Top Bottom