Hili sakata ni uchakachuaji mtupu. Nashangaa hawa watu wanasilimishwa nao hawataki. Hili ndio tatizo la watu fulani kujiona kuwa wao wamekamilika na kuchukuwa nafasi ya UUngu. Nafikiri viongozi wa kanisa nao wanakufuru kwa kudhania kuwa wao ndio waamuzi kwa imani ya mtu."Kilichotokea ni kwamba nilikuta baadhi ya wajumbe CCM ambao pia ni waumini wa kanisa hilo wakisema mapadri wanamkashifu mgombea wetu kuwa ana tabia mbaya wakati wao wana mapungufu mengi," alisema Kabanga akiwanukuu waumini wenzake.
"Ndipo nilipoanza kuwatetea mapadiri wangu na kuwaambia watu hao waache kuzungumza hayo kwa kuwa sote ni wakirstu swa Kanisa Katoliki na hao ni mapadiri wetu ambao hutupatia huduma za kiroho. Niliwaambia kuwa hata wakisema hivyo leo, padri ni padri na ataendelea kuwahudumia," alisema Kabanga.
Alisema katika mkutano huo aliwaomba waumini wenzake kuacha kuwakashifu mapadiri, badala yake kuendelea kufuata misingi ya imani ya kanisa hilo huku wakisikiliza mafundisho yao na kuacha kufauata matendo wanaoyofikiri yapo kinyume na mwenendo na maadili ya mapadri hao.
Kuhusu suala la mgombea wa CCM kukufuru utatu mtakatifu, yaani Mungu, mwana na roho, Kabanga alikanusha kuwepo na kitendo hicho na kueleza kuwa kauli zake zilitafsiriwa vibaya.
"Alichosema mgombea wetu ni kuhamasisha wanachama na wapenzi wake kuchagua mafiga matatu, mafiga matatu ambayo ni rais, mbunge na diwani na si vinginevyo," alisema Kabanga.
"Hata hivyo sisi kama chama tulimwita mgombea wetu na kumsihi kuacha kutumia maneno ambayo yanagusa imani kwenye kampeni zake," alisema Kabanga.
Kuhusu kutengwa kwake, Kabanga alisema uamuzi huo unamuuma na kumkosesha amani katika maisha yake ya sasa.
"Hata ninapokuwa njiani nikitembea, najisikia vibaya kwa jinsi waumini wenzangu wanavyoniangalia na jinsi wanavyozungumzia kuwa nimetengwa na kanisa," alisema.
Naye Chiritina Ninde, ambaye pia ametengwa na kanisa hilo, aliimbia Mwananchi kuwa mgombea wa chama hicho katika kampeni zake aliwataka wapiga kura kuchagua mafiga matatu ambayo ni rais, mbunge na diwani akirejea maandiko ya kwenye kitabu kitakatifu cha Biblia kuwa kuna nafsi tatu ambazo ni Mungu Baba, Mungu Mwana na Roho Mtakatifu ambazo Kikristo hutafsiriwa kuwa ni kitu kimoja.
Ninde, ambaye haruhusiwi kushiriki ibada, kupokea sakaramenti na huduma nyingine za kiroho zinazotolewa na kanisa hilo kutokana na kutengwa, anasema adhabu hiyo inamuumiza sana.
"Inauma sana mtu kutengwa na jumuiya uliyokuwa ukishiriki nayo katika kila kitu leo siruhusiwa kushiriki ibada wala kuhudhuria mazishi ya ndugu wala jamaa yangu ambaye kanisa litahusika... kwakweli hadi sasa sielewi cha kufanya," alisema huku akionyesha barua aliyokabidhiwa na kanisa la hilo Parokia ya Kristu Mfalme Desemba 17.
"Mimi nimezaliwa na kudumu katika imani ya kanisa katoliki hadi sasa. Sijawahi kusikia tukio kama hilo tangu kuzaliwa kwangu na wala sikutegemea kama ingefikia siku nikatengwa na kanisa."
Baadhi ya waumini walilimbia gazeti hili kuwa chanzo cha mgogoro huo ni kitendo cha kanisa hilo kutoa elimu ya uraia wakati wa kampeni, likihamasisha waumini wake kuchagua viongozi bora.
Lakini elimu hiyo ilichukuliwa na wanachama wa CCM kuwa ililenga kumsaidia mgombea wa Chadema ambaye ni Mkristo.
"Kila mara mapadri walitumia muda mwingi kuhamasisha waumini kuchagua viongozi bora huku wakitoa sifa za mtu anayefaa kuwa kiongozi. Lakini sifa hizo zilionekana kumhusu mgombea wa Chadema jambo lililowafanya waumini hao kutafisiri kuwa mapadiri wanaipendelea Chadema," alisema muumini mmoja aliyejitambulisha kwa jina moja la Joseph.
Mimi sioni sababu ya waumini walitengwa kujisikia vibaya iwapo imani zao ziko kwa Mungu wao. Hawa viongozi hawaweshi wala kuzima naiwapo wanaogopa kukosa kuzikwa watapokufa basi hilo si tatizo kwani sijasikia maiti akashindwa kuzikwa. Ninavyosikia kuwa Ukiristo umejengwa na kusamehe makosa sasa hawa wenzetu wanaposhindwa kuwasamehe wenzao ndio tuseme wanangojea mpaka 2015?