Kupita bila kupingwa - is this democracy too?

Source: Gazeti la MTANZANIA toleo la Jumanne 16 Novemba, 2010, Uk 1 na 2:

Mtikila naye bwana, is he serious? Kama atakuwa serious this time itakuwa safi saaaana!

Mch. Chris hapa kuna miongoni mwa points za nyongeza kwa Liberty Desk yako katika kesi hii:-

1) Wabunge hawa hawakuchaguliwa na wapigakura katika uchaguzi wa 31.10.2010 kwa mujibu wa sheria zinazohusika na uchaguzi huo; walichaguliwa na mchakato upi kwa mujibu wa sheria zipi?

2) Katika kujenga mazingira haramu ya kubaki wagombea pekee walicheza rafu mbaya sana ya kuwaondolea wagombea halali wenzao demokrasia, ambayo ni haki yao ya kikatiba kwa kila mgombea.

3) Mwenyekiti na Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi pia washitakiwe kwa kosa la uhaini kwa kuvunja katiba ya JMT kwa kuhalalisha kiharamia wagombea hawa na hatimaye kuwatambua kama wabunge halali huku wakijua hakika kwamba wanavunja sheria mama-katiba kuhalalisha wabunge batili bila kujali msitakabali wa sheria za nchi.
 
Mtakila ana uthubutu wa pekee.

Nadhani anamaanisha maana huyu jamaa yeye anapambana na vitu ambavyo awali huonekana kituko ila mbeleni taratibu watu wanaanza kumuelewa.

Kwangu mimi kuwapitisha bila kupigiwa kura ni uvunjifu mkubwa wa katiba na haki ya raia kujichagulia viongozi wao. Hata kama amekuwa peke yake na upinzania hawajasimamisha mgombea basi tungerudi zama zile za kale za kura za Ndio na Hapana.

Hawa kwangu mimi ni wabunge wa wana-CCM na sio watanzania kwenye majimbo husika. UPUUZI MTUPU
 
Huyo ndiyo mtikila, mahakama sehemu ya maisha yake, asipoenda huko anapata taabu na kiu kama ya wavuta sigara .
 
Kesi hii atashindwa kwa sababu katiba ndio inaruhusu ibara ya 78 (2) (a) (b) [toleo la 2005]. Au akishinda CJ atamwambia ni kweli lakini limekaa kisiasa zaidi hivyo suala hilo liende Bungeni ambako wengi wa wabunge wanafurahia kupita bila kupingwa.
 
kwani ni wabunge wa aina gani wanaotakiwa kuingia bungeni
Mimi najua
1.kuchaguliwa majimboni
2.kuteuliwa na raisi
3.viti maalum
 
hiyo ibala ya 78 (1) na (2) inazungumzia wabunge wanawake viti maalum sio kupita bila kupingwa, hivyo mwana jamvi hapo sikubaliani nae ingawa mi mi si mwanasheria hivyo REV naona yupo sahihi kwenda mahakamani.
 
Kesi hii atashindwa kwa sababu katiba ndio inaruhusu ibara ya 78 (2) (a) (b) [toleo la 2005]. Au akishinda CJ atamwambia ni kweli lakini limekaa kisiasa zaidi hivyo suala hilo liende Bungeni ambako wengi wa wabunge wanafurahia kupita bila kupingwa.

Let me refresh your memory katiba hairuhusu hata kidogo kwani kuna aina tano tu za wabunge chini ya katiba soma ibara 66 (1) (a) mpaka (e). Sheria ya uchaguzi inaleta chini ya kifungu 44 aina nyingine ya wabunge ambao katiba haijawagusia kabisa. Zaidi ya hiyo sheria imenyang'anya haki ya msingi ya raia kuchagua wabunge, Kwa hiyo pamoja na kukosa wapinzani ilitakiwa wapigiwe kura na wakubaliwe au wakataliwe na raia.
 
Kanuni za kudumu za bunge zanaelezea kuwa "mbunge" ni mtu aliyechaguliwa au kuteuliwa kwa mujibu wa ibara ya 66 ya katiba kuwa mjumbe wa Bunge la Jamhuri ya muungano.

Kulingana na kanuni hizo na pia na katiba ya nchi hakuna mbunge wa jimbo wa kupita bila kupigwa. Kinachotakiwa iwapo mgombea wa ubunge hakumpata mpinzani mtu huyo anapashwa apigiwe kura za hapana au ndiyo.

Kwakuwa jambo hilo halikufanyika kwa hao wabunge wanaosemekana walipita bila kupigwa hawana budi wahenguliwe.
 
Naunga mkono hoja. Kwa mujibu wa katiba ya TZ,sura ya pili,ibara ya 66,kifungu cha 1 a mpaka e,kimeainisha aina ya wabunge. Hao waliopita bila kupingwa hawapo. Ivyo ni BATILI
 
Sheria jamani za Tanzania ni kwa ajili ya kuwabeba Deep Green, wewe umeona wapi OCD anapigwa mtama na raia ndani ya kituo cha polisi (Maswa) then RPC anadai eti yeye mwenyewe OCD ndie ana haki ya kushitaki au kutoshitaki! ni kichefuchefu kwa kwenda mbele :redfaces:
 
Kama katika kusoma barua ya MMKjj pamoja na nukuu ya vifungu vya Sheria/Katiba naona bado hoja hii ya Wagombea waliopita bila kupingwa inaweza kwenda mahakamani kupingwa bila tatizo lolote.
Kwa uelewa wangu sheria yoyote inayotungwa lazima izingatie masharti ya Sheria Mama yaani Katiba ya JMT.
Katika hili labda wanasheria mtujuze imekaaje!
 
Mwanakijij tunakupongeza sana kwa hili.........sisi wengine tulikuwa hatulijui kwani hatujaisoma katiba wala hatuna, kuna umuhimu wa kila mtanzania kuwa na katiba na kuisoma. Viongozi wa Serikali wanatambua hili la mbunge kupita bila kupingwa ni kinyume na katiba lakini wanalifumbia macho kwani wana maslahi nalo! Hii siyo sahihi.......inatakiwa hawa viongozi wahusika ni pamoja na tume wote wapelekwe mahakani kwani wamevunja katiba ya nchi, pili hawa wabunge waliopita bila kupingwa nawo wapelekwe mahakani. Ufanyike uratibu huwo mapema na tujulishwe...........natumai watanzania wako tayari kuchangia garama za kesi ili haki ipatikane, Mwanakijiji Mungu akubariki


Mwanakijiji anastahili sifa nyingi. Ni wachache sana, kama wapo, ambao walikuwa wameliona hili. Wengi tulikuwa tumejiunga na mkumbo wa kudhani kuwa CCM imewapiga mabao wapinzani bila kuangalia matakwa ya Katiba. Sasa kazi siyo kuishawishi Tume ya Uchaguzi kuchukua hatua bali vyama vya upinzani vichukue hatua za kisheria/kikatiba kuhakikisha kuwa utapeli huu wa CCM haufanikiwi. Hasante M.M.
 
Hlafu on to p of this mwananchi wa kawaida huruhusiwik kugombea mpaka uwe mwanmachama wa chama cha siasa!!!! Our constitution sucks!!!!!!!!!
 
Thanks Mzee Mwanakijiji, umetutoa usingizini tulipokuwa tumelala totoro, natumaini hata NEC wenyewe watakubaliana na wewe kuwa wamefanya kosa kubwa na kuvunja kiapo kwa kwenda kinyume cha sheria japo hawawezi kusema hadharani lakini nafsi zitakubali.

Mi nafikiri sasa ni wakati muafaka wa kufungua kesi mahakamani kupinga uhalali wa wabunge wetu hawa wanaojiita wamepita bila ya kupingwa, Yupo wapi mchungaji mtikila nadhani hili ni dili kwake na ni lazima atshinda hii kesi.
 
Last edited by a moderator:
Mwanakijiji anastahili sifa nyingi. Ni wachache sana, kama wapo, ambao walikuwa wameliona hili. Wengi tulikuwa tumejiunga na mkumbo wa kudhani kuwa CCM imewapiga mabao wapinzani bila kuangalia matakwa ya Katiba. Sasa kazi siyo kuishawishi Tume ya Uchaguzi kuchukua hatua bali vyama vya upinzani vichukue hatua za kisheria/kikatiba kuhakikisha kuwa utapeli huu wa CCM haufanikiwi. Hasante M.M.
Hii imenikumbusha ile clip ya Lawrence Mwasha alipokuwa anajidai amepita bila kupingwa, alidhani CCM ikeshachagua habari ndiyo inakuwa imeishia hapo, matokeo yake wote tumeona. Bigup sana mwanakijiji kwa hii, hope imeshawafikia walengwa.
 
Thanks Mwanakijiji, umetutoa usingizini tulipokuwa tumelala totoro, natumaini hata NEC wenyewe watakubaliana na wewe kuwa wamefanya kosa kubwa na kuvunja kiapo kwa kwenda kinyume cha sheria japo hawawezi kusema hadharani lakini nafsi zitakubali.

Mi nafikiri sasa ni wakati muafaka wa kufungua kesi mahakamani kupinga uhalali wa wabunge wetu hawa wanaojiita wamepita bila ya kupingwa, Yupo wapi mchungaji mtikila nadhani hili ni dili kwake na ni lazima atshinda hii kesi.

Mi nashauri mmoja wa wana JF haswa mwanakijiji atuongoze wengine ndani ya jamvi hili kujua gharama za kesi na afungue kesi. Natoa wito kwa watu ambao wako interested kuchangia. Wakati wa maneno matupu umeisha.

Iko wazi kuwa gharama za kumnyamazisha mpinzani ni ndogo sana (kama yule wa musoma aliyepewa euro 2000 (Less tha 4 million) akajitoa) kuliko hata gharama za kampeni. Hii itasababisha sasa yeyote atakayepita CCM kwenye kura za maoni ahonge ili apite bila kupingwa. Na hawa watu wana mbinu za hali ya juu. Wataanza kuwaandaa watu katika vyama vya upinzani ili wajiandae kugombea kwa kujifanya wako active kwenye chama.

Ikiwezekana sheria ibadilishwe ili atakayekuwa hana mpinzani jimboni atakiwe kupigiwa ndiyo/hapana na ashinde kwa 80% ya kura.
 
Back
Top Bottom