Kupanda bei za bidhaa ni kaa la moto kwa wenye vipato vya chini

Nyendo

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,214
4,160
Hali ya maisha mtaani ni tia maji tia maji kwa misemo ya watu wa kipato cha chini, yaani hali ni tete kweli kweli. Kila ukienda kununnua bidhaa unakuta bei mpya ikiwa imepanda maradufu. Yaweza kuwa hata mara mbili ya bei ya awali uliyonunua kipindi cha mwisho. Jambo hili linafanya maisha kuwa magumusana kwani kipato hakitoshelezi mahitaji ya mtu au mtu na familia yake.

Hali hii ilianza kujitokeza mapema kabla ya vita inayoendela yaUrusi na Ukarain japo kwa sasa ndio imekuwa kichaka cha kujifichia kuwa vitu vinapanda bei kwa kuwa kuna vita na nchi zinazopigana ndio zilikuwa zinazalisha gesi na ngano kwa wingi nk. Lakini kanla ya vita hii bei zilianza kuoanda na hapo awali mzigo wote alitupiwa adui wa Dunia ambaye ni janga la Dunia UVIKO 19. Na hata kabla ya hilo janga vitu vilionekana kuanza kupanda japo mwanzo tuliambiwa ni kupanda kwa mafuta katika soko la dunia. Je, viongozi hutafuta kichaka cha kufichia tatizo la msingi ambalo huenda sisi wanachi hatulijui?

Gesi, Mafuta ya kupikia, sukari, ngano nk vimepanda bei kiasi ambcho mwananchi wa kipato kidogo anashindwa kumudu gharama ya kuvinunua. Wengi kwa sasa badala ya kununua mafuta ya kupikia wamenza kutafuta suluhisho kwa kutumia mafuta ya wanyama, au nishati mbadala wa gesi kitu ambacho ni hatari kwa afya na hatari kwa misuti na nchi kwani misitu ikiadimika tutakosa mvua na kupata njaa.

Tuachane na Majanga ya vitana Uviko. Je, nini viongozi wetu wanafanya kuhakikisha sisi watu wa chini tunaweza kuishi kutokana na kupanda kwa bei za bidhaa kiholela? Je, kuna jitihada zozote za kuchukua kuwanachukua kudhibiti mfumuko wa bei au wanatafuta tu gogo la kuangushia kuwa hawawezi zuia maana kuna hiki kinaendelea Duniani?

Sikatai yawezekana ni kweli lakini je, wanaacha wananchi wahangaike washindwe hata pata chakula chao? Kama hali ya uchumi imekuwa mabaya kiasi hiko cha bidhaa kupanda hadi mara mbili mbona hakuna hali ya dharyra kutangazwa ili watu waweze ambaiwa hatua za kufanya ikiwa kama kupunguza matumizi yasiyo ya lazima.

Nafikiri tuache siasa na maisha ya watu, tusiwe watu wa kutafuta kichaka cha kujificha bali tuwe watu wa kutafuta tatizo ni nini ili liweze kutatuliwa na kuepusha bei za vitu kupanda hata bila sababu za maana.
 
Hali ya maisha mtaani ni tia maji tia maji kwa misemo ya watu wa kipato cha chini, yaani hali ni tete kweli kweli. Kila ukienda kununnua bidhaa unakuta bei mpya ikiwa imepanda maradufu. Yaweza kuwa hata mara mbili ya bei ya awali uliyonunua kipindi cha mwisho. Jambo hili linafanya maisha kuwa magumusana kwani kipato hakitoshelezi mahitaji ya mtu au mtu na familia yake.
Hali ni mbaya mbaya mbaya kupita maelezo
 
Niongeze sauti msikie na nyie huko nyuma mliokingwa na wambele ,mama anafungulia nchi badoooooooooooooooo mbu wameingia ndani na kuwauma watuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu mpo na bado mama amefungua kakipande tu ka nchi kalikokuwa kamefungwa na magufuliiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii,au mnasemaje aendelee kufunguliwa nchi au aifunge Kwanza,semeni nasubiria jibu nikamwambie
 
Mama anafungua nchi now pambaneni maana Magufuli licha ya kupambana kwake kuhakikisha watu wanaishi katika usawa wenzie walimuona chizi wakaamua kumdedisha.

Tutalia kilio kimoja wote sasa. Maana nchi imesharudi kwenye matabaka sasa hamna usawa tena.
 
Watanzania sisi ni wapuuzi sana ngosha mlitaka aende mungu akasikia kilio chenu sasa hivi tena mnataka mama nae aende hivi mnataka raisi gani subiria tuisome namba nyie ndo mlikesha bar siku ya msiba.
 
Back
Top Bottom