ACT Wazalendo
JF-Expert Member
- May 5, 2014
- 610
- 1,540
Utangulizi
Tarehe 2 Agosti 2023 Serikali kupitia Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imetangaza bei mpya za mafuta ya petroli, diseli na mafuta ya taa. Taarifa hiyo imeonyesha kupaa sana kwa bei za mafuta kiasi cha kuzua taharuki na manungúniko miongoni mwa wananchi.
Taarifa inaonyesha bei za rejareja za petroli zimeongezeka kwa shilingi 463 (sawa na asilimia 16.9) kutoka shilingi 2,736 mwezi Julai hadi kufikia shilingi 3,199 mwezi huu (Agosti). Bei ya Diseli imeongezeka kwa shilingi 391(sawa na asilimia 15.3) kutoka 2,544 mwezi Julai hadi kufikia 2,935 mwezi huu kwa Dar es Salaam.
Bei hizi mpya zimeibua wasiwasi mkubwa hasa hasa katika kupandisha gharama za maisha na kuongeza kasi ya mfumuko wa bei ya bidhaa muhimu. Serikali kupitia Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) katika taarifa yake imeeleza kuwa mabadiliko ya bei yanatokana changamoto za upatikanaji wa dola za Marekani; mabadiliko ya sera za kikodi; ongezeko la gharama za mafuta katika soko la dunia (FOB) na gharama za uagizaji (premium).
Uchambuzi wa hoja na hali halisi ya gharama ya mafuta. Chama cha ACT Wazalendo tumepitia hoja zote zinazoelezwa kupelekea kupaisha kwa bei hizo ili kuona kwa kiasi gani zimechangia kwenye bei ya mafuta kwa kila lita moja ya Petroli na Diseli hadi kufika bandari ya Dar es Salaam. Uchambuzi wetu umegusia gharama halisi ya mafuta ya petroli, dizeli na mafuta ya taa katika soko la dunia (FOB); gharama za usafirishaji (premium); kodi na tozo za Serikali na gharama & faida za wafanyabiashara.
Kutakana na utafiti na uchambuzi tulioufanya tumebaini masuala yafuatayo;
Serikali kupitia EWURA imedanganya kuhusu ongezeko la gharama za Mafuta katika Soko la dunia. Mafuta yanayotumika mwezi huu (Agosti) ni yale yaliyoagizwa kwa bei ya soko la dunia ya mwezi Juni. Katika uchambuzi wetu tumeona kuwa gharama za mafuta katika Soko la Dunia kwa kipindi cha Mwezi Mei, Juni na Julai kwa kila lita moja ya petroli mwezi Aprili ilikuwa dola ya Marekani 0.53 (Tsh 1,311.7) kwa mwezi Mei ilikuwa dola ya Marekani 0.47 (Tsh 1,163.2) na Juni dola ya Marekani 0.47 (1,163.2) kwa mantiki hii bei ya mafuta katika soko la Dunia imeshuka na sio kupanda kama taarifa ya Serikali kupitia EWURA ilivyoonesha
Gharama za uagizaji wa Mafuta, katika Uchambuzi wetu tumebaini kuwa Gharama za uagizaji Mafuta kwa kipindi cha miezi mitatu hazikupanda bali zimeshuka. Taarifa za zabuni zinaonyesha gharama zilizotumika kuagiza mafuta kwa mwezi Juni zilikuwa dola ya Marekani 0.11 (Tsh 274.45) kwa lita Moja ikilinganishwa na bei ya mwezi Mei na April ambazo zilikuwa Shilingi 474 (dola ya marekani (0.19) na shilingi 499 mtawalia. Hivyo, basi mchango wa wa gharama za uagizaji (premium) sio hoja kubwa.
Changamoto ya Uhaba wa Dola za Marekani, ni kweli nchi yetu inakabiliwa na uhaba wa dola za Marekani ambayo ndiyo Fedha inayotumika katika kufanya manunuzi na uagizaji wa bidhaa za nje (importation) ikiwapo mafuta, changamoto hii ni kubwa sana kwani uhaba wa Dola za Marekani Una athari kubwa sana kwa taifa utakwenda kuathiri kwa kiasi kikubwa Uchumi wa Taifa na uchumi wa mtu mmoja mmoja, Uhaba huu unatokana na Kukosekana kwa uwiano wa urari wa kibiashara (balance of trade) kati ya mauzo ya nje na uagizaji wa bidhaa na huduma kutoka nje (import and export), katika mwaka wa Fedha 2022/23 Mauzo ya nje yalikua Dola bilioni 12 na Mnaunuzi yalikua Dola Bilioni 16, nakisi ni Dola za kimarekani bilioni 4 ambayo haijawahi kutokea nakisi kubwa namna hii kwa miaka ishirini (20) kadiri nchi inavyouza nje ndivyo inaongeza hifadhi ya Fedha za kigeni (Foreign reserve) na kadiri unavyonunua Zaidi unapunguza hifadhi na kusababisha kupungua kwa uwezo wa Taifa kuagiza bidhaa.
Kuongezeka kwa kodi ya mafuta, katika bajeti ya mwaka huu Serikali imeongeza shilingi 100 katika kila lita moja ya petroli na Diseli. Athari za uamuzi wa Serikali kuongeza kodi kwenye kila lita moja ya mafuta ndio imeanza kuumiza wananchi.
Serikali kusitisha kutoa Ruzuku ya mafuta kwa petroli na Diseli. Licha ya changamoto hii Serikali imeondoa ruzuku ya mafuta ya Petroli na Dizeli iliyokua ikitolewa kuanzia Agosti 2022 ili kupunguza makali ya bei na kuleta nafuu kwa walaji, hivyo Serikali imeondoa ruzuku na kuongeza ushuru katika Petroli na Dizeli.
Kushuka kwa thamani ya Shilingi dhidi ya Dola, thamani ya shilingi ya Tanzania inaendelea kuporomoka kwa kasi Agosti 3 mwaka 2022 Dola ya moja ya kimarekani ilikua sawasawa na shilingi za kitanzania 2,315.00 lakini mpaka kufikia agosti 3 mwaka 2023 Dola moja ya kimarekani ni sawa na Shilingi za kitanzania 2,545.00 ongezeko la shilingi 172.24 sawa na asilimia 10 kwa kipindi cha mwaka.
Hii ni hatari sana kwani itatubidi kutumia fedha nyingi sana kunua bidhaa nje, hali itakayosababisha bidhaa hizo kupanda bei (mfumuko wa bei) kama Mafuta (nishati), Mbolea na bidhaa za chuma ambazo tunatumia gharama kubwa kuagiza bidhaa na huduma hizo.
Kuhusu Uhaba wa Mafuta katika baadhi ya maeneo nchini, Kumekua na malalamiko ya uhaba wa mafuta ya petroli Dizeli na Mafuta ya Taa katika maeneo mbalimbali nchini kama vile Kagera, Katavi, Manyara na baadhi ya maeneo Mkoani Lindi, EWURA ilitoka hadharani na kusema kwamba ni njama za baadhi ya wafanyabiashara kuficha bidhaa hiyo ili kusubiri bei ipande waingize sokoni, Tunaona ni muhimu sasa EWURA ijitafakari upya kuhusu utekelezaji wa mamlaka yake ili Wananchi wa maeneo husika wasiendelee kupata taabu ya uholela wa kupanda bei na kukosa huduma.
Hivyo basi, kupanda kwa gharama za bei ya mafuta nchini kumetokana na Serikali kuondoa Ruzuku kwenye mafuta ya Petroli na Dizeli, Serikali kuongeza ushuru wa Shilingi 100 kwenye kila lita ya Dizeli na Petroli na kuporomoka kwa thamani ya Shilingi dhidi ya Dola ya Marekani kutokana uhaba wa dola.
Tunataka hatua zichukuliwe;
Katika uchambuzi wa bajeti ya Serikali kuu kwa mwaka 2023/24 tuliitaka Serikali kuchukua hatua za haraka katika kupunguza matumizi ya fedha kuagiza bidhaa na huduma nje ya nchi. Hatua hizo ni mwafaka zichukuliwe sasa ili kunusuru nchi kuingia kwenye hali ngumu zaidi.
1. Hatua za kupunguza uagizaji wa bidhaa na huduma nje ya nchi
(i) Serikali ianze kutekeleza matumizi ya nishati mbadala (gesi asilia). Kwa kuanzia Magari yote ya Serikali yaanze kutumia Gesi asilia (CNG) ili kupunguza kutumia fedha nyingi za kigeni kuagiza bidhaa za mafuta. Pendekezo hili pia litapelekea kupunguza matumizi ya Serikali kwa takribani shilingi bilioni 500 kwa mwaka. Hivyo basi, Bohari zote za Serikali (GPSA) zifungwe mitambo ya kujazia gesi asilia (CNG) mara moja.
(ii) Serikali iweke msisitizo kwenye utekelezaji wa mradi wa Mchuchuma na Liganga ili kuzalisha bidhaa za chuma kwa matumizi ya ndani na nje. Hii itasaidia kuokoa fedha za kigeni zaidi ya Dola za kimarekani Bilioni1.1 ambazo tunatumia kuagiza chuma kutoka nje kwa mujibu wa taarifa za Serikali.
(iii) Serikali iharakishe Mradi wa kusindika Gesi asilia wa Lindi (LNG) na kuufungamanisha na Mradi wa kuanzisha kiwanda Kikubwa cha kuzalisha Mbolea. Hii itasaidia kuokoa Fedha za Kigeni tunazotumia kuagiza Mbolea kutoka nje, ambapo mwaka 2022 tulitumia Dola za Kimarekani Milioni 503.
2. Hatua za mahususi za kikodi
(i) Serikali kupitia Shirika la Maendeleo ya Petoli Tanzania (TPDC) ijenge Hifadhi ya kutosha kutunza mafuta angalau ya kutosha miezi sita ili kama kutatokea mabadiliko ya bei katika soko la Dunia yasiathiri uchumi wetu kwa haraka.
(ii) Serikali irejeshe utaratibu wa kutoa ruzuku ya mafuta kwa petroli na Dizeli hadi hatua zingine za kukabiliana na bei zikamilike na tunarudia wito wetu iweke Ruzuku ya shilingi 500.
(iii) Serikali iondoe tozo ya shingi 100 iliyoanzishwa katika mwaka wa fedha 2023/2024.
3. Hatua za kuongeza uzalishaji na mauzo nje
1. Kuongeza mauzo ya bidhaa za kilimo nje ikiwemo kuongeza thamani ya mazao. Kwa mfano Korosho iliyobanguliwa inaweza kutuletea mpaka Dola za Kimarekani milioni 500 kwa mwaka na Soya (kwa kuuza China) inaweza kuingiza mpaka Dola za Kimarekani Bilioni 1. Hivyo hivyo kwa mazao kama ya Ufuta, Mbaazi, Kahawa na Pamba yanaweza kutuletea Fedha nyingi zaidi za Kigeni kwa kuongeza tija na uzalishaji.
2. Kuweka vivutio katika sekta ya utalii kwa kuongeza matangazo na kuboresha miundombinu ya Utalii ili kuongeza idadi ya watalii maradufu ya idadi ya sasa. Tukifika watalii Milioni 5 kwa mwaka, nchi yetu itapata fedha za kigeni mara tatu ya tunazopata sasa na kuongeza ajira nyingi kwa Watanzania.
3. kuongeza ufanisi katika Bandari zetu ili kufaidika na Uchumi wa jiografia kwa kuongeza idadi ya mizigo inayopita na kutoka nchi jirani maradufu ya tunayohudumia sasa. Sasa hivi mapato ya Fedha za kigeni tunayoyapata kwa huduma za usafirishaji (transit trade) ni Takribani Dola za Kimarekani Bilioni 1.9 tu kwa mwaka 2022 ilihali uwezo wetu ni wa kufikia mpaka Dola za Kimarekani Bilioni 12 kwa mwaka.
Mwisho, changamoto ya uhaba wa fedha una mchango mkubwa sana kwenye kuongeza bei za bidhaa na huduma tunazozinunua kutoka nje.
Ndg. Is-haka Rashid Mchinjita
Twitter: @Isihakamchinji1
Msemaji wa Sekta ya Nishati.
ACT Wazalendo.
Ndg. Ester Akhoth Thomas
Twitter: @esterthomas_1
Msemaji wa sekta ya Fedha na Uchumi
ACT Wazalendo.
05 Agosti, 20223