Kuna ukweli kuhusu ujauzto na hili?

kashonzo

Member
Jan 1, 2013
26
3
Kuna watu wanasema eti wajawazito wawili wakikaa sehemu moja LAZIMA mmojawapo kati yao ajifungue kwa upasuaji na mwingine atapoteza mtoto(miscarrage). kuna mtu anasema ilimtokea mwaka jana na kabla ya hapo alielezwa na mama mkubwa wake akapuuza. kuna ukweli wowote wadau?
 
Ushirikina' mkubwa mlionao kwa ushahidi mimi nina dada zangu wawili wamekaa hapa nyumbani tangu mimba hadi wamejifungua wote tena salama na ajabu wamepitana siku moja tu,mmoja kajifungua mtoto wa kiume mwengine wa kike so achana na mawazo yako hasi
 
Inategemea wewe kwako nani ana nguvu,unamkimbilia na kumtegemea zaidi ama Mungu ama shetani,kama ni wa kuelewa utakuwa umeelewa mwanzo mwisho.
 
inategemea upo mkoa gani kama upo kule geita wanapofufuka watu kila siku lazima hayo yatokee
 
Kuna watu wanasema eti wajawazito wawili wakikaa sehemu moja LAZIMA mmojawapo kati yao ajifungue kwa upasuaji na mwingine atapoteza mtoto(miscarrage). kuna mtu anasema ilimtokea mwaka jana na kabla ya hapo alielezwa na mama mkubwa wake akapuuza. kuna ukweli wowote wadau?

Kwa hiyo wakienda hospitali kliniki wakati wa ujauzito wenye mimba hawaruhusiwi kupanga foleni pamoja? Wee kama una mimba au mkeo ana mimba acha woga, mtajifungua salama tu mkizingatia mambo muhimu ya kisayansi kuhusu utunzaji mimba.
 
kukaa pamoja kwa maana ya kuishi nyumba moja kipindi cha mimba zao na cyo wkt wa kwenda kujifungua tu
 
Ushirikina' mkubwa mlionao kwa ushahidi mimi nina dada zangu wawili wamekaa hapa nyumbani tangu mimba hadi wamejifungua wote tena salama na ajabu wamepitana siku moja tu,mmoja kajifungua mtoto wa kiume mwengine wa kike so achana na mawazo yako hasi

hongera kwa kuwa na dada 2 waliopewa ujauzito siku 1 na kujifungua pamoja kwa kupishana siku 1.hiyo ni bahati
 
Kuna watu wanasema eti wajawazito wawili wakikaa sehemu moja LAZIMA mmojawapo kati yao ajifungue kwa upasuaji na mwingine atapoteza mtoto(miscarrage). kuna mtu anasema ilimtokea mwaka jana na kabla ya hapo alielezwa na mama mkubwa wake akapuuza. kuna ukweli wowote wadau?

Hakuna ukweli wowote mkuu ni inani zisizo na tija. Miaka yote niliyosoma hapo Muhimbili sijawahi kukutana na hicho kitu mkuu ni story za vijiweni hazina tofauti na zile za mjanzito asile mayai atazaa mtoto asiye na nywele kumbe wanaume walitaka kuyala wao tu.
 
Kuna watu wanasema eti
wajawazito wawili wakikaa sehemu moja LAZIMA mmojawapo kati yao
ajifungue kwa upasuaji na mwingine atapoteza mtoto(miscarrage). kuna
mtu anasema ilimtokea mwaka jana na kabla ya hapo alielezwa na mama
mkubwa wake akapuuza. kuna ukweli wowote wadau?

uongo mtupu , vipi matenity home ingekuwa balaaaa
 
Kuna watu wanasema eti wajawazito wawili wakikaa sehemu moja LAZIMA mmojawapo kati yao ajifungue kwa upasuaji na mwingine atapoteza mtoto(miscarrage). kuna mtu anasema ilimtokea mwaka jana na kabla ya hapo alielezwa na mama mkubwa wake akapuuza. kuna ukweli wowote wadau?

si kweli, mi nilikua mjamzito pamoja na dada yangu na wakat wa kujifungua tulirudi wote kwa mama na tulijifungua salama. Ni mipango ya mungu tuu!
 
Back
Top Bottom