Kasumba ya kuna uchungu wa mzazi kwa mtoto aliyemzaa haina ukweli

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,340
51,900
KASUMBA YA KUNA UCHUNGU WA MZAZI KWA MTOTO ALIYEMZAA HAINA UKWELI.

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli.

Mada hii inaweza ikawa Tata. Pengine ikazua mfuragano wa kutoleana hoja. Ni vizuri kila mmoja atoe hoja zake Kwa utulivu kutetea upande wake.

Kuna dhana au tuseme Kasumba iliyoenea Duniani kote kuwa kuna uchungu wa Asili unaomuunganisha Mama na mtoto aliyemzaa au Baba na mtoto, tuseme mzazi na Mtoto. Lakini hasahasa imezoeleka kuwa mama ndiye anauchungu zaidi na watoto aliowazaa kuliko mtu yeyote.

KASUMBA au dhana hiyo sio yakweli. Hivyo mtu akisema ni Uongo hatakuwa anakosea Sana. Ni Sawa na Ile kasumba au dhana isemayo Damu ni nzito kuliko Maji. Ile ni dhana isiyo na Ukweli wowote.

Ni Imani tuu Watu waliojiwekea na mtazamo Watu walioamua kuwa nao lakini hakuna uhalisia wa Jambo Hilo.

Dhana au kasumba hiyo ni Uongo Kwa hoja zifuatazo;

1. Uchungu wa mzazi Kwa Watoto haulingani.

Katika chunguzi zangu nilizozifanya, nimebaini kuwa uchungu wa mzazi Kwa mtoto mmoja kwenda Kwa mtoto mwingine haufanani.

Wote anaweza kuwa amewazaa mwenyewe lakini kuna mmoja anauchungu naye zaidi kuliko wengine. Na sio ajabu kuna wengine Hana kabisa uchungu nao,

Hiyo pekeake inaonyesha kuwa kuzaa pekeake haitoshi Kwa Mzazi hasa Mama au Baba kuwa na uchungu Kwa mtoto.

Kuna mtoto ndani ya familia yenu akipatwa na janga au hata akifa Mama au bàba yako atakuwa na uchungu, huzuni, maumivu Makali kuliko hata angefariki mtoto mwingine.

Kama kuzaa ingekuwa ndio tiketi ya mzazi Kupata uchungu basi uchungu wa mzazi Kwa Watoto wake ungekuwa the Same(Sawasawa).

Mzazi anaweza akakupa maneno ya kukufariji kuwa wote anauchungu nanyi lakini kiuhalisia(ukweli) ni kuwa yupo ambaye anauchungu naye kuliko wengine.

Hii inamaanisha Ipo sababu ya ziada ambayo Ipo mbali na ishu ya kuzaa.

2. Kumbadilishia Mzazi mtoto Wakati wa kijifungua bila ya yeye kujua na akawa na uchungu na mtoto huyo Kwa kudhani alimzaa.

Mama anaweza kuwa na uchungu na mtoto ambaye hakumzaa Kwa kudhani alimzaa. Hivyo hapo ishu ni mtazamo na sio tukio la kuzaa.

Mama Wakati WA kujifungua unaweza ukambadilishia mtoto wake bila ya yeye kujua lakini ukashangaa akawa na uchungu naye kama alimzaa yeye.
Hii ni Kwa sababu Akili yake, mtazamo wake, Imani yake imejijenga au ameamua kuijenga hivyo. Lakini sio tukio la yeye kuzaa pale.

Kama ishu ilikuwa kumzaa mtoto ndio KUNAKUPA uchungu naye kiasili yaani automatically, au unakuwa connected na mtoto basi hata ungebadilishiwa automatically ungeona kuna Jambo haliko sawasawa.

Kwa upande wa kinababa, ndio Kabisa. Wapo Wababa wanauchungu na watoto wanaodhani ni Watoto wao wakuwazaa kabisa, kumbe walibambikizwa. Alafu siku wakija kugundua kuwa huyo mtoto/Watoto sio wako huo uchungu unapotea na sio ajabu akawatimua.

Kama hiyo haitoshi, Mzazi aliyekuzaa na ukabadilishwa anaweza akakutana na wewe na asikutambue na sio ajabu anaweza akakutendea mambo mabaya bila ya uchungu na wewe licha ya kuwa ukweli uliojificha ni kuwa alikuzaa.

Hivyo hapo ishu ni Imani, mtazamo na upendo wa mtu mwenyewe.

3. Wazazi wengi wanauchungu na wao wenyewe na sio Watoto wao.
Wazazi waliowengi wanapofanya mambo mazuri Kwa Watoto wao sio Kwa sababu ya maslahi ya Watoto Bali Kwa sababu ya wao wenyewe hasa nyakati za uzeeni.

Taikon nadiriki kusema kuwa, kama kusingekuwa na uzee au magonjwa basi hiki kinachoendelea Kwa wazazi wengi kisingekuwepo.

Mzazi anaweza kukuambia anakusomesha au anahangaika kwaajili yako lakini ukichunguza Nia ya ndani kabisa utakuja kubaini kuwa haikuwa kwaajili yako Bali kwaajili yake.
Ni wazazi wachache Sana, yaani kwenye elfu moja akawepo mmoja ambaye anauchungu na wewe bila kutaka malipo.

4. Wazazi wengi hujifanya wanauchungu na watoto wao Wale waliofanikiwa au wenye ramani.
Binadamu bila kujali ni Mimi mwenyewe au mzazi wangu, au wewe au mzazi wako, anaongozwa Kwa kiasi kikubwa na ubinafsi.

Ni rahisi Kwa mzazi kuwa na uchungu na wewe ikiwa anaona umefanikiwa. Ni rahisi kukufanyia Unafiki ambao kama hutokuwa makini unaweza kuutafsiri kama uchungu (upendo). Ukiwa katika Hali ngumu ni ngumu kuuona upendo wa Wazazi wengi Kwa Watoto.

Ingawaje kuna Ile kujidanganya na kujipa moyo ili kutokuonekana Mbele za jamii kama unawakosea adabu wazazi wako. Lakini kama utakuwa wale Watu wa black and white basi utaungana na Mimi kuwa hakuna kitu kinaitwa uchungu wa mzazi Kwa mtoto kisa alikuzaa.

Ila kuna mtazamo, Imani, na Roho ya upendo ambayo inaweza kuja natural bila kutegemea kama alikuzaa au hakukuzaa.

5. Wapo Wazazi wanaotupa Watoto wao na wengine kuwaua Kabisa.
Hii ni moja ya Sababu inayothibitisha kuwa Hakuna uhusiano wowote wa uchungu (upendo) wa mzazi Kwa mtoto au Watoto wake.

Kama ingekuwa kitendo cha kuzaa tuu papohapo unakuwa na uchungu na mtoto wako kikamilifu basi isingeripotiwa mahali popote kuwa kuna Watoto wametupwa jalalani, au chooni, au kuuawa. Au wengine kuwatoa kafara Kwa Imani za kishirikina.

Matukio hayo yanathibitisha kuwa hakuna uhusiano wowote isipokuwa ni ishu ya kiimani, kimtazamo tuu.

6. Wazazi wengi wakizaa Watoto wenye ulemavu au wenye Sifa Fulani Mbaya huchukia na pengine kutamani kuwaua.

Kuzaa na kuwa na uchungu na mtoto ni vitu viwili vilivyombali mbali Kabisa.
Nimewahi kuona na kushuhudia mzazi anamficha mtoto wake kisa amemzaa na ulemavu WA ngozi. Nimewahi kushuhudia mzazi hampendi mtoto wake kisa amemzaa ni mweusi Mno Wakati yeye alitaka Mweupe.

Nimewahi kushuhudia mzazi hataki Watu wamjue mtoto wake kisa anakasoro Fulani kulingana na mtazamo wake. Hata uchungu Hana.
Hii inamaanisha kuwa Ile kasumba ya kusema Mama anauchungu na mtoto ni dhana tuu ya kuwafanya wazazi wawapende Watoto wao.

Ni sawasawa na ule msemo usemao "Mama ni mama hata kama ni rikwama" ni msemo tuu ili kuwaweka Sawa Watoto wasiwadharau Mama zao na wawapende. Ila kiuhalisia haubadilishi chochote.

Taikon Master ninajua yakuwa Uhuru ndio Jambo pekee ambalo litapembua mvivu na mbichi kujua ukweli ni upi na Uongo ni upi.

Ili Dunia ibakie salama hasa kimahusiano ni lazima Uhuru wa kiimani na kiakili udhibitiwe ili kuficha uhalisia na Ukweli wa mambo. Lakini kama usipodhibitiwa basi haya ninayoyasema yatakuwa bayana. Waziwazi kabisa.

Wito; Upendo haujawahi kulazimishwa popote pale. Usijilizimishe kumpenda yeyote. Wala yeyote asijilazimishe kukupenda bila kujali ni nani. Walakini kila mtu atende wajibu na Majukumu yake ya kisheria. Kama mzazi ni jukumu lake kumhudumia Mtoto, hiyo ni sheria lakini haimaanishi kuwa ndio anaupendo na wewe. Hapo utakuwa unachanganya Madesa.

Na kama mtoto unajukumu la kumheshimu na kumtiti Mzazi wako lakini hiyo haitamaanisha unampenda. Hapo utakuwa unachanganya Madesa.

Kipimo cha Upendo kitakuja siku ambayo utalinganisha Kile kitu au Yule mtoto ambaye mzazi wako anampenda kuliko wewe na wewe hapo ndipo tutajua upendo upo au haupo.

Pale hazina ya Mtu ilipo ndipo Roho yake ilipo. Hapo ndipo anapopapenda, hapo ndipo anauchungu Napo.

Sio ajabu wapo wazazi wakiambiwa wachague Mali na watoto wao watachagua Mali. Halikadhalika wapo Watoto wakiambiwa wachague Mali na mzazi basi watachagua MALI.

Taikon leo sina la ziada. Karibuni kwenye mjadala.

Nawatakia Sabato njema.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
😂😂
Kwa sababu sio mnafiki.

Binadamu Kwa vile haijui kesho take ndio maana lazima atumie mbinu ya unafiki, asije baadaye kuumbuka😀
Unasemaje sio mnafiki wakati anatuambia ombeni mtapewa tafutenj mtapata...
Utaomba maisha yako yote na hicho unachoomba usipate, au anakupa kwa wakati anaotaka yeye. Kuna haja gani ya kuomba kama yeye anajua kabisa hata uombe vipi hakupi?

Mwisho wa siku unaambiwa huna imani.
 
Unasemaje sio mnafiki wakati anatuambia ombeni mtapewa tafutenj mtapata...
Utaomba maisha yako yote na hicho unachoomba usipate, au anakupa kwa wakati anaotaka yeye. Kuna haja gani ya kuomba kama yeye anajua kabisa hata uombe vipi hakupi?

Mwisho wa siku unaambiwa huna imani.

Hayo ni maandiko tuu Mkuu.

Unamuomba Mungu kwani yeye hajui nini unachotaka?
Ikiwa hakuna tofauti ya anayeomba na asiyeomba huoni kama hapo kuna Uongo?

Mungu haombwi.
Angalia mambo ambayo upo nayo asilimia 90% hukuyaomba.
Yale makubwa 100% hujayaomba.

Hukuomba kuzaliwa lakini ukazaliwa.
Hukuomba kuwa Mwanamke lakini imekuwa Mwanamke.
Hukuomba kuwa hivyo ulivyo lakini upo hivyo ulivyo.
 
Ni ukweli mtupu...
Wala hujadanganya tunayaishi haya katika nyumba na familia zetu...uchungu hutokea pale unapopush mtoto..akitoka ni ww na yeye sasa duniani je mtaivana?
Ila ki ubinadamu hapo kwny kifo kila kifo kinauma hapo hakuna mjadala hasa cha watu wako wa karibu na hasa watoto...
 
Ni ukweli mtupu...
Wala hujadanganya tunayaishi haya katika nyumba na familia zetu...uchungu hutokea pale unapopush mtoto..akitoka ni ww na yeye sasa duniani je mtaivana?
Ila ki ubinadamu hapo kwny kifo kila kifo kinauma hapo hakuna mjadala hasa cha watu wako wa karibu na hasa watoto...

Ni kweli kila kifo kinauma.
Lakini nakuhakikishia kuwa kuna kifo kikitokea hasa Kwa mtoto unayempenda Moto utakuwakia.
Bahati nzuri hata Watoto wenyewe au watu au marafiki zako wanajua fika.

Ukienda Kwa mganga WA kienyeji unafikiri ni Kwa nini sio kila mtoto unaweza mtoa kafara Ila wao ndio wanakuchagulia?
Wanajua fika kuwa yupo mtoto ambaye moyo wako ameushikilia, mmeivana, mna- bond, yaani unampenda kuliko wengine.
 
Back
Top Bottom