Kuna ubaya wowote kulala hotelini au lodge badala ya kulala msibani pasipo na malazi ya kutosha?

Kwani huyo aliekufa ana status gan kwenye jamii mpaka ndugu wajitofautishe na waombolezaji wengine?
Ndiyo hivyo mkuu. Hadi kwenye misiba mfumo wa kibepari umesimika mirija yake ya kibiashara hata kwenye mambo ambayo siyo ya lazima.
 
Kuna siku watu watakuja kwako Msibani na wakalala loji wakatoka kwako kwa sababu hizo halafu wakaja asubuhi. Nadhani utaleta hapa jibu utakuwa umeona Kama Ni sahihi wao kwenda kulala loji ama sio sahihi
 
1. Je, ni sahihi kwa mwenyeji wa msiba kama nyumba yake haitoshi waombolezaji wote kulala akiwatafutia lodge/hotel ya jirani na kwake na kuwalipia wageni wake anaowaheshimu sana waweze kulala hapo?
2. Na ikitokea huyo mwenyeji anatamani kuwalipia lodge lakini akawa hana fedha ya kuwalipia hao wageni wao wenyewe wanaweza kujilipia?
3. Kama waombolezaji wa karibu sana wa mfiwa wanaweza kulipiwa vyumba vya kulala lodge inakuwaje kwa muombolezaji baki na yeye mwenyewe akiamua ajiongoze ili alale mahali pazuri?
4. Nijuavyo hata waombolezaji msibani wakati wa kuandaliwa pa kulala pia kuna madaraja. Wenye umuhimu mkubwa uandaliwa pa kulala kwenye vyumba vya nyumba yenye msiba, wengine utafutiwa vyumba kwenye nyumba za majirani na hata wengine wenye umuhimu fulani utupiwa japo kamkeka ka kulalia n.k. Wengine wote wasio na umuhimu mkubwa uachwa wajilaze popote watakapoona panawafaa. Kwa mazingira hayo, mimi kama mtu baki kwa nini nisijitafutie pa kuegesha mbavu zangu kwa amani?
 
Kwako wewe ni sawa kwa sababu alielufa hakuhusu ila uyo best ako kama utoeza kumsapoti apo kukuche then we nenda uko lodge haina shida ata kidogo,

ila kwa kawaida msibani kama unamsopti bora mkeshe kama ni wanywaji wekeni stock kama ni walaji chomeni nyama , ila mi uzoefu wa kwenda misiba ya watu wageni huwa tunaandaliwa space kabisaa kama hujaandaliwa nenda kalale lodge
 
Kuna siku watu watakuja kwako Msibani na wakalala loji wakatoka kwako kwa sababu hizo halafu wakaja asubuhi. Nadhani utaleta hapa jibu utakuwa umeona Kama Ni sahihi wao kwenda kulala loji ama sio sahihi
Sasa wakija inabidi uwaandalie space zao za kujiegesha acha wenyeji bora wakose sehem kuna siku nilienda ktk msiba wa rafiki yangu kizuri si walevi so tukateka eneo letu akatuletea mashuka ila kiukweli hatukulala ni pombe adi majogoo
 
Back
Top Bottom