Nyaka-One
JF-Expert Member
- Oct 27, 2013
- 4,318
- 5,999
Maisha yetu ya kitanzania wote tunayafahamu. Nimemsindikiza rafiki yangu kwenye msiba wa ndugu yake wa karibu na mazishi ni kesho kutwa.
Nikiangalia kwa haraka haraka kwa udogo wa nyumba msiba ulipo na idadi ya waombolezaji ambao wengi wao wanaonekana watalala nataka nimshauri huyu rafiki yangu tutafute mapema vyumba vya kulala kwenye hotel ya kawaida au lodge iliyo jirani ili kuepuka kukosa mahali pa kulala hapa msibani au kubanana kulala kwenye mikeka, ndani ya gari, kwenye masofa, magodoro tupu machache yaliyopo n.k.
Pia kuepuka kushambuliwa na mbu, kuibiwa begi au kuchomolewa vitu kwenye begi n.k. maana kwenye misiba hayo mambo utokea sana.
Ni nini maoni yako wewe mwanaJF kama kuna ubaya wowote wa kutafuta chumba nje ya nyumba msiba ulipo au ni lazima kulala msibani?