Yo Yo
JF-Expert Member
- May 31, 2008
- 11,217
- 1,706
Atakuwa anatafuta jina langu la ukweli ili aje anitishe kuwa ananijua nina Rasta na mzuzu......Anyway mkuu pale BOT watoto wa vigogo bado wanapeta .....Ndulu alitupiga changa la machoLabda Mkuu William anaogopa kukujibu hili usijemletea Hansard nyingine hapa. LOL. Kuna list moja ya Wafanyakazi wa BOT niliiona kule Fesibuku, ilikuwa inatisha.
Dogo wa Kigoda sijui ali re-seat lini form foo?Watoto vigogo BoT wasafishwa
Na Ramadhan Semtawa
WAKATI watumishi wengine tisa wa Benki Kuu (BoT), wakifunguliwa kesi mahakamani kwa kughushi vyeti, watumishi wengine 18, maarufu kama watoto wa vigogo waliodaiwa kuajiriwa kinyemela wamebainika kuwa na sifa stahili.
Kukamilika kwa uchunguzi huo na matokeo, kunaondoa na kumaliza utata uliokuwepo tangu awali kuhusu ajira za watoto ambao baba zao wengine wapo serikalini na waliostaafu.
Gavana wa BoT, Profesa Benno Ndulu, alithibitishia gazeti hili jijini Dar es Salaam kuhusu watoto hao kubainika na sifa stahili.
Watoto ambao wameonekana kuwa na sifa, majina ya koo zao ni pamoja na Lowassa, Sumaye, Kawawa, Lumbanga, Hassan Mwinyi, Muganda, Mahita, Nchimbi na Mkapa.
Katika orodha hiyo, majina mengine ya ukoo yanayotajwa ni pamoja na Luhanjo, Kamba, Mongela na Kigoda.
Akizungumzia mchakato huo ambao alisema uliendeshwa kwa uwazi na umakini, Profesa Ndulu alisema katika uchunguzi huo watoto wanane kati ya 18 ambao walikuwa wanafanya kazi za kitaaluma wote walikuwa na sifa.
Kwa mujibu wa Profesa Ndulu, jambo la msingi lililotumika katika uchunguzi huo ni vigezo vya ajira kwa kuanzia mwaka 2000/01 hadi 2006/07.
Akifafanua hilo, Profesa Ndulu alisema kabla ya mwaka 2005, kulikuwa na vigezo tofauti na baada ya mwaka huo, walioajiriwa baadaye 2006/07, walipaswa kuwa na vigezo vipya tofauti na vile vya mwaka 2000 hadi 2005.
Profesa Ndulu alisema kabla ya mwaka 2005, kazi za kitaaluma kigezo kikuu kilikuwa ni shahada ya kwanza, lakini baada ya mwaka huo kigezo kikawa ni shahada ya uzamili (MA).
"Kwa hiyo, watoto hao wanane mnaoita wa vigogo wote walikuwa na basic entries (sifa za kujiunga), waliajiriwa kwa vigezo stahili, ambavyo kipindi hicho ilikuwa ni shahada ya kwanza, lakini pia waliendelea kusoma na kuweza kufikia shahada ya uzamili ambayo ni kigezo cha baada ya mwaka 2005," alifafanua Profesa Ndulu.
Alisema vijana hao ambao wanafanya kazi nzuri, waliingia na sifa stahili na bado wamekuwa wakijiendeleza kwa kusoma zaidi.
"Tena ni vijana wachapakazi tu, wamesoma vizuri, wanafanya kazi vizuri na tayari tumewapa barua za kuwataarifu kwamba wana sifa stahili," alisisitiza Profesa Ndulu.
Profesa Ndulu alisema watoto wengine kumi ambao hawakuwa wakifanya kazi za kitaaluma, nao waliingia wakiwa na sifa.
Kwa mujibu wa Profesa Ndulu, watoto hao walikuwa na kazi ambazo ni pamoja kuhesabu fedha.
Akizungumzia sifa zao za kujiunga, alisema kwa kazi ambazo si za kitaaluma, kigezo kikubwa kilikuwa ni kidato cha nne na kujua hesabu na Kiingereza.
"Hawa nao 10, wote walikuwa na sifa hizo, wanafanya kazi zao kwa mujibu wa taratibu na hakuna namna yoyote ya kughushi ambayo walifanya," alifafanua Profesa Ndulu, gavana ambaye amekuwa akiisafisha BoT.
Alisema uchunguzi huo uliangalia watumishi 50 wakiwemo hao 18 watoto wa vigogo na kuongeza kwamba, wengine pia walibainika na sifa huku wale ambao walikiuka walichukuliwa hatua.
Hata hivyo, alisema tayari BoT imetoa tangazo kwa kuwataka watumishi hao kujisomea kwa gharama zao wenyewe vinginevyo hawatapanda madaraja.
"Kwa hiyo, kama mtu hatajiendeleza, ajue hatapanda daraja, atabaki hapo hapo na kuathiri ajira yake," alisisiza Gavana Ndulu.
BoT ambayo ni taasisi nyeti katika kipindi cha kuanzia mwaka 2000 chini ya uongozi wa hayati gavana Daud Ballali, ilikumbwa na tuhuma mbalimbali.
Miongoni mwa tuhuma hizo, ni pamoja na hizo za watoto wa vigogo kuajiriwa katika mazingira yaliyohisiwa kuwa ni tata, kashfa ya ufisadi katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) na gharama kubwa za ujenzi wa majengo pacha ya benki hiyo.
.