Kulikoni CHADEMA baadhi ya wagombea majmboni kutorudisha fomu?!

Nachojua mimi chadema imesimamisha wabunge na madiwani nchi nzima na majimbo yote na huu ulikuwa ni mpango wao na ndiyo sababu hasa ya operation sangara.

kinachotokea sasa si cha kulahumu viongozi wa chadema,mf aliyekuwa mgombea ubunge jimbo la Isimila ni mwenyekiti wa mkoa wa chadema Iringa,ilikuwaje hizo ni hila na mbinu zinazofanywa na ccm kunamambo viongozi hawawezi kuzuia,mbunge huyo alichukua form ya chama na kuteuliwa na kamati kuu kuwa mgombea halali wa jimbo hilo.Lakini pia alichukua form za tume za kugombea ubunge ,viongozi wameshangazwa na bwana huyo mpaka mda wa kurudisha form kuisha hajaonekana,jitihada za kumtafuta ziliendelea bila mafanikio kwani hata simu zilizimwa.baada ya kupatikana alijieleza anavyojua yeye na uongozi wa chama umechukua atua mara moja wa kumsimamisha uongozi,lakini hata yeye amejiudhuru,kwa hiyo unaweza kuona trend ilivyo.Sometimes Viongozi wa juu si wakulaumiwa najua kikatiba uongozi wa chini unachaguliwa na wanachama wa chini jiongozi wa juu hawezi kujua tabia na nyendo za kila mtu na hasa wanachama wenyewe wasipotoa malalamiko.Kumbuka Chadema ni Chama makini kinachoongozwa kwa kufuata katiba ya chama.Na si kwamba Viongozi wamekaa kimya Hatua zitachululiwa kwa wagombea wote waliojitoa bila baada ya kufanya uchunguzi ya nini kimesababisha hayo kutokea otherwise ni vigumu kutoa uamuzi bila facts.

Hata wale wabunge wa ccm waliopita bila kupingwa baadhi si kweli ukiacha case kama ya hapo juu ambayo imetokea pia kwa Lukuvi na maeneo machache Rufaa zimekatwa na tunaomba tume itende haki.

Nashahuri tusiwakatishe sana tamaa wapenzi wenzetu kwani ni lazima tujue wapinzani hasa Chadema wanafanyakazi kwa tabu sana.


Songa mbele Slaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
 
Ndugu yangu unanishock sana. Yaani una maana Chadema ikishinda itabidi itafute watenbdaji wa serikali yake yote wapya nchi nzima? Watumishi wa umma (Civil servants etc) wanatakiwa wasiwe na vyama hivyo hubakia palepale, chama chochote kikishika dola. Wanaobadilishwa ni mawaziri tu na maRC na maDC. Sidhani iwapo Chadema itashindwa kuwapata hawa.

.....well said ZK.....! Hii ndio tafsiri ambayo hata watendaji wa serikali wasio wanasiasa wanayo....hufikiria eti wakichagua upinzani vibarua vyao vitaota nyasi.....kitu ambacho si kweli kabisa!
 
Mpeni Kaisari yaliyo ya Kaisari! Tumefika mahali inabidi tutoe credit kwa wana CCM moja mmoja na si kwa chama chenyewe as such. Tuliyoelezwa yamefanya na Mama Anna Makinda katika jimbo lake yanapaswa kuuungwa mkono na mama huyo kupongezwa yeye mwenyewe kwa juhudi zake binafsi za kuwaletea wananchi wake misaada kwa ajili ya maendeleo yao. Congratulations Mama Makinda and keep it up. Unastahili kabisa kuendelea kuchaguliwa hadi uwe kibogoyo!
 
Hehehe hommie bana naona unampigie kampeni huyu bibi kiaina.... nina ushahidi kashindwa kujenga daraja tu kwenda kwa mama yake mzazi ndo alete maendeleo ya kushindilia barabara kila baada ya miezi 3 wapi na wapi? Kadaraja tu kwenda kijiji cha mama ake anashindwa kukaboresha hapo changa la macho asome alama za nyakati mwaka huu hata unaibu atausikia kwenye bomba.

Homu boi.....simpigii kampeni Makinda, ila ninasema tu mambo yale yaliyofanyika kule mitaa ya kwetu yeye akiwa mbunge......! najua kule kijijini kwao hakubaliki kabisa kutokana na sababu wanazozijua wao! Yes, ile barabara ya Njombe -Ludewa trust me huwa inafanyiwa periodic maintance za hali ya juu......! unaenda na ka-GX kako unatambaa fresh mpaka bush...hayo ndiyo ninayozungumza! Sijazungumzia weaknesses za Makinda hapa so far na wala sijasema she is our best candidate....upo mpwa?
 
Ni watu wa CCM disguised nini? Au wamekata tu tamaa?:confused2:

Nasema hiviiii uchaguzi Tanzania hakuna ila kila baada ya miaka mitano kunakuwa na drama/maigizo kwahiyo mkitaka msitake CCM watawaacha vinywa wazi siku matokeo yatakapotangazwa! mtakuja kukamatana uchawi nawaambia wenyewe kwa wenyewe wanalizana! Tafakari.....Chukua hatua
 
Back
Top Bottom