Masanilo
Platinum Member
- Oct 2, 2007
- 22,286
- 4,493
Panadol huondoa maumivu ya kichwa. CHADEMA ni maarufu kipimo cha mtu mzima meza tembe 2x3 kwa siku kwa siku 7 ni tiba kamili.
Wewe umeshindikana upo na huku?
Panadol huondoa maumivu ya kichwa. CHADEMA ni maarufu kipimo cha mtu mzima meza tembe 2x3 kwa siku kwa siku 7 ni tiba kamili.
Kilichotokea jimboni Chunya kwa mfano:Mwanachama mmoja wa CHADEMA alienda kuchukua form ya ubunge kwa tiketi ya CHADEMA,Uongozi wa mkoa wa CHADEMA ukamuwekea pingamizi kwamba sio chaguo lao na watasimamisha mgombea mwingie... TIA MAJI,TIA MAJI SIKU YA KURUDISHA FORM HII HAPA... CHADEMA haikupeleka mbadala wa yule waliyemuwekea pingamizi!
Mnyamahodzo,
Sema nikupe facts zingine au unaenda na wewe kukusanya data? Kama umeridhika, nitake radhi kwa kunisema vibaya kwenye post yako ya kwanza kny thread hii......!
Tafadhari naomba usiwe na Munkari kiasi hicho kuwa mtaratibu. Sijakusema vibaya. nimesema ukweli. Kama nawe umo ndani, utang'aka. Kitu kizuri ni kuwa facts za kuniambia barabara zinatengenezwa kila baada ya miezi mitatu, au kuanzisha MAKINDA CUP, au kuwapatia vyerehani 60 wale wakinamama wa vijiji kadhaa(kijiji kimojawapo walipewa 2) ziwaendeleze wakinamama hawa wakitanzania. Facts za namna mwalivyojiandikisha majina kwa ajili ya mbolea ya ruzuku halafu wasiopate walichoomba na mbolea kuuzwa mkoa mwingine?
Facts ya kuwataka wanachi wajenge dispensary halafu nurse Glade B (sawa na wa RED Cross) ndiyo mkuu wa kituo, tabibu, nurse, na mgawa dawa vyote yeye? nikubaliane nazo hizo.
Sijui uko Njombe kweli au uko Pwani? Unajua wewe ulipo. Kikubwa ielzee ukweli hali ya Njombe na kitu kile huyu mama alichofanya kwa watu wa Njombe; ametumia ukimya wao na uoga wao kuwakandamiza.
Jivunie; Anna makinda amewafanyia nini watu wa Njombe Kusini for 15 years? ainisha kinagaubaga.
Nadhani ni matatizo ya kiutendaji ndiyo yalowafanya wakashindwa kurejesha hizo forms. Kwa kawaida CHADEMA mwaka huu nategemea itatisha kuliko chaguzi zake zote zilizotangulia, na kuliko chama chochote cha siasa kwa upande wa upinzani. Kikubwa ni mambo ya kusubiri na kuona.
:welcome:
Tafadhali usiwe munkari. Nimekujibu kwa kukueleza ukweli.
facts gani ambazo unataka kunipa; zile kugawa vyerehani 60 kwa wakinamama wa vijiji tofauti wanaambiwa wavitumie kujiongezea kipato (that 60 being distribited, not placed at one centre), ama zile za kuorodhesha majina kwa ajili ya mbolea ya rudhuku halafu hampati mlichokihitaji na mbolea nyingine kwenda kuuzwa Songea? Ama facts za kuzigeuza ofisi za serikali ya mitaa na kujenga majengo ambayo yamefanywa zahanati ambazo Mkuu wa kituo ni Nurse Glade B, ambaye ndiye tabibu, nurse, mgawa dawa vyote yeye ili tu aonekane amewaletea wananchi huduma za hospitali karibu? No No Noooo ! Siwezi kuzikubali.
Sifahamu unamfahamu makinda toka lini namna alivyojiingiza katika siasa za Njombe.
acha usanii, ukizingatia wewe ni Rev. sasa CUF imeingiaje hapa?ooooh mai mai wamesimamisha wagombea wao! TGIF
....Sikiliza mkuu, wewe naona unazungumzia zaidi mambo ya hearsay.....! mimi nimekwambia nimeona mama yangu ana mifuko mitatu ya Mbolea ndani kwake, ana dawa ya ukungu na si yeye tu amepata hivi vitu....na ndivyo anavitaka sasa wewe unaniambiaje watu wemeandikisha then mbolea ikachengeshwa? hapo ndipo tunatofautiana na wewe....nakwambia mimi nimeona kwa macho yangu mbolea imegawiwa kijiji kizima....hadithi gani unaleta ndugu yangu?
Nachukua jembe nikalime mahindi mkipatana mwenzenu navuna!
Nyie mavuvuzela mbona nyie mko hapa na hamkuchukua fomu kokote? Tupishe bwana msitutaabishe bure. Twajua tufanyalo.watakuja na maelezo ya ccm ndio wachawi.....mimi binafsi ningependa kuona demokrasia inakuwa na wapinzani wanapata nafasi hasa katika kata na majimbo (haimaanishi sitaki wapate rais). lakini naona baado. Binafsi siwasanifu kwa janga hili ila naona ambavyo bado tuna safari katika mageuzi ya siasa za tz. naamini si kosa la kiutendaji hili...hapa kuna shida ya mgombea mwenyewe sijajua though ni ipi..kuna shida ya baadhi (si lazima hawa ambao hawakurudisha fomu) ya wachumia tumbo kukubali kununuliwa ili kuuza jimbo...bado tuna njaaa bado tunataka demokrasi kidogo ina challenge sana. Nimewahi kusikia mgombea fulani alikuwa anauza ushindi wake kila uchaguzi kwa kukubali kusaini matokeo ya kushindwa ilhali anajua ameshinda...big shame! watu bado hawajajua wanataka nini lol
mix with yours
Mkuu sawa wee tukana tu lakini kumbuka ni kura zao hawa unaowasema ndizo zitakazo kupa ushindi.Nyie mavuvuzela mbona nyie mko hapa na hamkuchukua fomu kokote? Tupishe bwana msitutaabishe bure. Twajua tufanyalo.
Wakuu leo nimesikia asubuhi katika radio Wapo kuwa kuna baadhi ya majimbo wagombea ubunge wa CHADEMA hawakurejesha fomu zao hadi ilipofika jana kwa muda waliotakiwa.
Majimbo hayo ni pamoja na lile la Isimani kwa mh. Lukuvi na la Anna Makinda. Pia mengine sikuweza kuyapata maana nilipatwa na mshangao.
CHADEMA jitokezeni hapa mtueleweshe yaliyowasibu wanachama wenu hawa tena viongozi huko waliko na hawakurejesha fomu??!!
Je hii inaashiria nini?
Naamini mmeanza vizuri na ni vema mmalize vizuri. Msitoe nafasi ya changamoto kwa wagombea wengine. Kinachotakiwa ni kuongeza idadi ya wabunge mjengoni!!
Maumivu ya kichwa huanza pooole pooole.
Mchungaji wew chunga kondoo kuna mbwa mwitu wanataka kuwameza. Usiwaache tafadhari.
Kulima tuachie sisi, we tuhimize tukupe zaka.
Usisahau kutupa yarohoni.
Wachungaji siku hizi wanakula Kondoo wanaowachunga.Tumeona Singida na Iringa
Ndugu mwenye mawazo nimekubaliana na mawazo yako hapo juu.....! Sasa hapo nilipohiglight ndicho kilichotokea Njombe kusini kwa Makinda sawa.....?
Hehehe hommie bana naona unampigie kampeni huyu bibi kiaina.... nina ushahidi kashindwa kujenga daraja tu kwenda kwa mama yake mzazi ndo alete maendeleo ya kushindilia barabara kila baada ya miezi 3 wapi na wapi? Kadaraja tu kwenda kijiji cha mama ake anashindwa kukaboresha hapo changa la macho asome alama za nyakati mwaka huu hata unaibu atausikia kwenye bomba.