Kukoroma usingizini: Fahamu chanzo na tiba yake

Wataalam naombeni mnijuze juu ya hili, hili tatizo husababishwa na nini? Nini utatuzi wake? Msaada tafadhali hili tatizo linasumbua sana hapa kwangu!
 
Ni tatizo kwenye mfumo wa upumuaji ambalo mara nyingi linasababishwa na kuwa na uzito mkubwa..
Tiba mojawapo ni kupunguza uzito wa mwili, mengine wataalamu wa afya watakuja kukusaidia zaidi mkuu.
 
Ni tatizo kwenye mfumo wa upumuaji ambalo mara nyingi linasababishwa na kuwa na uzito mkubwa..
Tiba mojawapo ni kupunguza uzito wa mwili, mengine wataalamu wa afya watakuja kukusaidia zaidi mkuu.

Nashukuru ila uzito mbona ni wa kawaida sana?
 
Unajua angalau kidogo kuhusu BMI?

Body Mass Index? Kwa urefu nilionao na umri wangu kilo 58 nilizonazo ni wastani hata daktari aliwahi kuniambia kwa mwili wangu nilionao sio uzito mbaya kwasababu natakiwa kuwa uzito kati ya kilo 55 - 60.
 
Unajua angalau kidogo kuhusu BMI?

Body Mass Index? Kwa urefu nilionao na umri wangu kilo 58 nilizonazo ni wastani hata daktari aliwahi kuniambia kwa mwili wangu nilionao sio uzito mbaya kwasababu natakiwa kuwa na uzito kati ya kilo 55 - 60.
 
koroma.jpg


Si jambo geni kusikia mtu wako wa karibu au mwenza wako anapokuwa amelala kuwa na kawaida akikoroma au kuwa na mikwamo mikwamo ya milio isiyo ya kawaida akiwa katika usingizi mzito.Iwapo utamtikisa au kumgusa hali hiyo hupotea kwa sekunde kadhaa na kama atapata tena usingizi mlio huo hujirudia tena.

Wengi wamekuwa wakijiuliza ni kipi husababisha hali ya kukoroma na wengine wamelichukulia kuwa ni suala la kimaumbile kama vile unene lakini sababu hasa wamekuwa hawaijui lakini kwa upande wa afya linaweza kuwa ni kiashiria cha tatizo la kiafya mwilini.Tayari kuna tafiti za sayansi ya tiba zinaonyesha mahusiano makubwa ya magonjwa ya moyo na watu wanaokoroma au pingamizi la usingizi.Watu wenye pingamizi la usingizi hasa watu wazima wameonyesha kuwa na dalili za magonjwa ya moyo.

Pingamizi la usingizi ni nini?
Pingamizi la upumuaji usingizini ni hali ya kushindwa kupumua kwa kutumia pua au mdomo kwa muda wa sekunde kumi. Tatizo hili hutokea zaidi ya mara 30 katika hatua za vipindi viwili ambavyo kitaalamu hujulikana kama mjongeo wa kasi wa macho na mjongea wa kawaida wa macho.Mjongeo wa kasi wa macho wakati wa usingizi ni kipindi kimojawapo cha usingizi wa kawaida ambacho huambatana na macho kucheza cheza yaani mtu anakuwa yupo usingizini huku macho yake yakicheza cheza.Kwa kawaida wakati mtu amelala hupitia hatua hii mojawapo ya usingizi na hutokea mara nne hadi tano katika usingizi.


Hali hii huweza kutokea kwa muda mfupi na mwishowe kipindi hiki hukawia kwa muda mrefu hasa inapokaribia asubuhi.

Inakisiwa kuwa mjongeo wa kasi wa macho huchukua asilimia 20-25 ya usingizi wa mtu mzima yaani dakika 90-120 kwa ujumla.Katika hali ya mjongeo wa kawaida wa macho ni hatua ambayo mtu anakuwa amelala lakini hawezi kuchezesha macho, kuota ndoto ni nadra sana kwa wenye kupata hatua hii. Akili huwa katika hali njema kabisa viungo vya mwili wake kutolegea ndio maana mtu anaweza kutembea huku akiwa usingizini. (sleep walk)Tatizo la pingamizi la upumuaji usingizini huathiri zaidi wanaume kuliko wanawake.

Watu gani wako kwenye hatari ya tatizo hili?
• Unene uliopitiliza
• Shinikizo la damu (Hypertension)
• Moyo kushindwa kufanya kazi vizuri (Congestive Cardiac Failure)
• Matatizo katika mishipa ya damu ya moyo (Coronary Heart Disease)
• Unyongovu/sonona. (Depression)
• Magonjwa sugu katika mfumo wa upumuaji (Chronic Obstructive Pulmonary Disease)
• Unywaji pombe kupita kiasi
• Uvutaji sigara kupita kiasi na matumizi ya madawa ya kulevya (ilicit narcotics)
• Historia ya mwana familia kuwa na tatizo hili.
• Watumiaji wa dawa zifuatazo: Barbiturates, Benzodiazepines, Ethanol,hypertensive and diabetic treatment----kwa kifupi dawa za usingizi, shinikizo la damu na kisukari.
•Maumbile- wanaume wana viambo vidogo vya kupitisha hewa kuliko wanawake.
•Aina ya ulalaji, mtu anapolala chali, huzifanya nyama za koo kutulia na hivyo kuziba mianya ya upumuaji.

Dalili na Viashiria
• Kula zaidi kipindi cha mchana
• Kukoroma
• Ushuhuda wa mwenzi wako – wakati wa pingamizi la upumuaji au mitweto
• Kukosa usingizi kipindi cha usiku
• Uchovu
• Kuamka usiku kwenda kukojoa mara kwa mara

Vipimo Vya Uchunguzi
• Polysomnogram-kipimo cha picha kina choonyesha hali ya tishu za njiani ya hewa (puani).
• Actigraphy

Matibabu:
1. Muendelezo chanya wa shinikizo katika mfumo wa hewa
2. Matibabu ya matatizo yanayoweza kupelekea kupata tatizo hili mfano kupunguza uzito kwa wale wenye uzito uliopitiliza, kutibu shinikizo la damu, kupunguza unywaji wa pombe na uvutaji sigara.

Lakini zipo dawa ambazo zimezagaa mtaani zinazodaiwa kuponya ukoromaji hata hivyo hazijathibitishwa kumaliza tatizo hilo.
Jambo la muhimu ni kufuata hatua muhimu na kujua chanzo kinachokufanya ukorome hasa kwa kuwashirikisha unaolala nao.
Kwa mfano waweza kumwambia unayelala naye akuangalie wakati unaokoroma ni wakati gani na hivyo kujua chanzo. Hapo utajua kipi kinasababisha ukoromaji wako na namna ya kukomesha.Lakini kwa ujumla waweza kubadili aina ya kulala, kwa mfano kuacha kulala chali, penga kamasi kabla ya kulala, safisha chumba kabla ya kulala ili kuondoa hewa chafu inayoweza kusababisha vumbi na hatimaye mikoromo.

Chanzo: Mwananchi
 
Mkuu mimi nashkuru sina ilo tatizo la kukoroma ila kuna sehemu umenigusa kabisa. Hapo katika hali ya mjengeo wa kawaida wa macho. Nilikua najiuliza sana mbona mimi sina tabia yakuota ndoto? Nasikiliza tu ndoto za watu ila mimi kuota ni mara moja moja sana. Leo umefungua macho mkuu shukran
 
Kumbee....mm pia sioti ndoto kbsaa...na ninajiuliza sana ni kwann kumbe iko hivyo.sasa ili macho yawe yanacheza tufanyaje mkuu
 
Dr wale ambao wana uzito mkubwa kuliko inavyostahili (wanene) ambao mara nyingi wengi wao hukoroma wakiamua kufanya mazoezi kwa mfano kukimbia na hivyo kupunguza uzito wao ili ushabihiane na uzito unaotakiwa kuendana na umri, jinsia na urefu wao basi wengi wao kukoroma hupotea kabisa.
 
Mimi pia sina tatizo la kukoroma ila hapo kwenye mjongeo wa macho nina swali. kuna mdogo wangu na hata baadhi ya wanae na binamu yangu nimeona hii hawakoromi ila wakilala macho hayafumbi kabisa (yaani yanakuwa kama yamefumba robo tatu so karangi keupe ka jicho unakaona kama robo) kiasi kwamba kwa mtu usiyejua unaweza kufikiri hajalala kumbe yupo usingizini tena wa pono. Hii inatokana na nini?
 
Wakuu nipo msibani tumelala matanga. Kwa kuwa hapa Iringa pana baridi kidogo, hivyo watu wote tumelala ndani.
Katika chumba cha wanaume nilicholala tupo watu 13. Karibu nusu ya hawa watu wanakoroma kiasi nimeshindwa kulala naperuzi JF. Ajabu kelele hizi za kukoroma sizisikii upande wa akinamama.
Nijuzeni kukoroma ni ugonjwa au ni tatizo la kimaumbile? Inakuaje mpaka mtu anakoroma? Kwa nini wanaume ndiyo wanaokoroma sana?
Tuchangie mawazo hawa ndugu zetu waepuke vipi tatizo hili kwani linakera na kufadhaisha.
 
Wewe una umri gani ? kukoroma ni kama ndevu. mwanaume asiye na ndevu hakoromi sawasawa na kina mama. Siku ukibalehe na ukaota ndevu na ww utakoroma
 
Kama kweli chumba kimoja mmelala wanaume 13 kwa usalama wako bure utoke nje.

Umenifanya nicheke kwa nguvu...nitaonekana mwanga buree usiku wote huu...

Mleta mada...wanawake pia wanakoroma ila ndo sio kwa libesi kama wanaume....
 
Wakuu nipo msibani tumelala matanga. Kwa kuwa hapa Iringa pana baridi kidogo, hivyo watu wote tumelala ndani.
Katika chumba cha wanaume nilicholala tupo watu 13. Karibu nusu ya hawa watu wanakoroma kiasi nimeshindwa kulala naperuzi JF. Ajabu kelele hizi za kukoroma sizisikii upande wa akinamama.
Nijuzeni kukoroma ni ugonjwa au ni tatizo la kimaumbile? Inakuaje mpaka mtu anakora? Kwa nini wanaume ndiyo wanaokoroma sana?
Tuchangie mawazo hawa ndugu zetu waepuke vipi tatizo hili kwani linakera na kufaisha.
Hiyo kitu hata mimi ni balaa hasa nikinywa yale mambo yetu inakuwa shida zaidi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom