Fahamu Kuhusu Uvula

Wild Flower

Member
Jul 20, 2023
80
96
Uvula ni sehemu ndogo inayoning'inia nyuma la Koo ambayo inajulikana kwa jina maarufu zaidi kama Kidaka tonge au Kilimi. Kiungo hiki hakipatikani kwa Wanyama wengine zaidi ya Binadamu (Mammals)

Ingawa huonekana kama kiungo kidogo ndani ya Mwili lakini Uvula ina majukumu muhimu kwenye Mwili wa binadamu ikiwemo kuzuia Chakula kisiingie kwenye Mfumo wa Hewa na kutokea Puani. Uvula ndio Kiungo ambacho huzuia tusipaliwe wakati wa kumeza Chakula

Uvula husaidia katika uzalishaji wa Sauti wakati wa Kuzungumza kwa kutamka maneno yanayosikika vizuri. Inashiriki katika kurekebisha shinikizo la hewa na kusaidia kuunda sauti tofauti

Pia, husaidia katika kuzalisha Mate ambayo ni muhimu kwa kudumisha Unyevu wa Koo na Pua, na kuchangia kusafisha njia ya Hewa.

Aidha, Watu wengi hawajui kuwa kukoroma Usingizini kunahusiana na Uvula. Kukoroma husababishwa na kuziba kwa njia ya hewa ya juu pale Mtu anapokuwa amelala, hivyo kusababisha Uvula kutoa sauti ya mtetemo (kukoroma)

Katika hali mbaya, endapo Uvula imekuwa ndefu sana huweza kusababisha kuziba kwa njia ya hewa na kuleta Changamoto za kupumua. Ni muhimu kushauriana na Daktari ikiwa kutatokea
 
Back
Top Bottom