Nawezaje kumaliza tatizo la kukoroma usiku?

Jun 25, 2023
23
21
Nimecopy comment ya mdau kama ilivyo kutoka hapahapa Jamii Forums.

Moral of story: naomba mwenye kufahamu suluhisho serious la kumaliza kabisa tatizo hili. Asanteni sana


"Likely una sleep apnea. Google sleep apnea na utapata maelezo mengi na ya kina na jinsi ya kupunguza kukoroma. Kuna mpaka mazoezi ya kufanya na app za kulipia zitakazokuongoza hatua kwa hatua jinsi ya kuimarisha hiyo misuli ya koo inayo-collapse usiku ukilala na hivyo kupelekea kukoroma.

Kisababishi kikubwa mara nyingi ni kuongezeka uzito au kuishi sedentary life. Na ushauri wa kwanza kwa daktari huwa ni kuambiwa upunguze uzito na/au uanze kufanya mazoezi. Utashauriwa pia uache kulalia mgongo na ulale kwa ubavu japo hili siyo suluhisho la kudumu.

Njia nyingine ni kutengenezewa mouth guard kama zile wanazovaaga akina Mandonga kwenye ngumi. Hii inatengenezwa kitaalamu baada ya kupima configuration ya taya lako na usiku unaivaa. Inasaidia kuhakikisha kuwa hewa inapita usiku bila kuzuiwa unapokuwa umelala.

Shida ya sleep apnea mbali na kukoroma kuna kipindi hewa inashindwa kupita kabisa na hivyo ubongo inabidi ukuamshe vinginevyo unaweza kukata moto watu wakaimba parapanda. Kwa hivyo usiku kucha ubongo haupumziki uko stand by kukushtua uamke ili upate Oxygen unayoihitaji sana. Ndiyo maana kesho yake mkoromaji mwenye sleep apnea anakuwa amechoka sana hata kama atakuwa amelala masaa 10. Kama uko bado kijana ni sawa lakini huko mbele ya safari sleep apnea inatajwa kuwa ndiyo chanzo kimojawapo kikuu cha strokes (+ heart attacks); na magonjwa mengine ya akili kama dementia na hata Arzheimer. Ubongo unahitaji supply nzuri ya Oxygen 24/7!

Na hiyo shtuka shtuka ya ubongo pia inaathiri sana afya ya moyo. Usiku moyo unatakiwa kupumzika na mapigo ya moyo hupungua sana mpaka kufikia hata 50s kama uko physically fit. Ukiwa mkoromaji sana maana yake moyo haupumziki maana unakuwa stand by usiku kucha kusukuma damu kwa wingi kwenda kwenye ubongo ili kuhakikisha ubongo una Oxygen ya kutosha. Mapigo ya moyo kwa mkoromaji yana-fluctuate sana usiku kucha moyo ukipambana kuhakikisha kuwa ubongo unapata damu (Oxygen) ya kutosha. Matokeo yake baada ya miaka 10 hivi au huko uzeeni unaweza kupatwa na shida za moyo kama moyo kupanuka na matatizo mengine.

Huku kwetu tunachukulia jambo hili kirahisi tu lakini tafiti mbalimbali zimeanza kulihusisha na ishu ya wanaume kufa mapema maana wakoromaji wengi ni wanaume hasa ukizingatia kuwa wenyewe ndiyo wanywaji wa pombe, wavuta sigara na wepesi wa kunenepeana - mambo ambayo yanatajwa kuwa yanaweza kusababisha ukoromaji na sleep apnea. Kwa hivyo tusichukulie ukoromaji kuwa ni jambo la kawaida. Wakati mwingine unaweza kusababisha matatizo makubwa japo ni kwa muda mrefu!

Kama walivyoshauri wadau hapo juu kwa sasa mwambie mkeo akusaidie kwa kuhakikisha kuwa unalala kwa ubavu. Anza kufanya mazoezi ili kupunguza mafuta mwilini (hata kama huna kitambi) na kuimarisha afya nzima. Fanya mazoezi ya kuimarisha hiyo misuli ya koo (Google au tafuta app nzuri itakayokuongoza). Kama hakuna mabadiliko basi nenda ukaonane na sleep specialist na yeye atakupima kama una sleep apnea ama la...na atapendekeza mambo ya kufanya.

Jitahidi ulimalize hilo tatizo..."
 
Back
Top Bottom