Naombeni msaada wa dawa ya kuzuia kukoroma usiku

kwisha

JF-Expert Member
Sep 9, 2021
1,666
4,365
Mwenzenu nimekuwa na tatizo la kukoroma saana usiku mpaka imekuwa kero kwa mke wangu. Kuna kipindi alikuwa ana lalamika eti namkosesha usingizi kwasababu ya kukoroma kwangu.

Nilibisha nikaona anaanza vituko, nikampiga mkwara usiku huu nilivyokuwa nimelala amerecord video fulani yangu nikiwa usingizini na kuniamsha.

Nilivyoamka akaniambia kuwa amechoka, anakosa usingizi kwasababu ya kulala kwangu. Nikataka kupiga mkwara kama kawaida yangu akanionyesha video, kuangalia hivi ni mimi kweli.

Nakoroma kama vile mtu ambaye ana maji kwenye koo, nikashindwa la kusema.

Naomba msaada kwa yeyote ambaye anaweza jua tatizo hili linachangiwa na nini na dawa yake ni nini.

Naomba anisaidie mwenzenu ndoa yangu mbichi kabisa lakini kwa style hii naona hatuna marefu uko mbeleni. Mimi situmii pombe, au sina kitambi sasa sijui tatizo litakuwa wapi?!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kukoroma haijawahi kuwa tatizo la kuvunja ndoa, kakuchoka anakutafutia sababu.
 
Tafuta njia mbili ila inatakiwa kupata mtaalamu.

kama unatatizo la upumuaji lipo kwenye pua au mdomo utumie njia ipi.

IMG_0475.jpg

IMG_0474.jpg
 
Mkeo akiamka anatakiwa akugeuze kidogo tu na hutakoroma. Ukilalia mgongo akugeuze kiubavu, Kama umelala kiubavu akugeuze ubavu mwingine au akulaze kifudifudi n.k. vile vile usile mbususu usiku Ili mwili kuupunguzia uchovu ichakate asubuhi au masaa kadhaa kabla ya muda wa kulala. Huyo mkeo mwambie ndoa Zina mengi avumilie ipo siku yataisha.
 
Umemshauri vizuri Sana mkuu, nimeipenda hii
 
Mwenzenu nimekuwa na tatizo la kukoroma saana usiku mpaka imekuwa kero kwa mke wangu. Kuna kipindi alikuwa ana lalamika eti namkosesha usingizi kwasababu ya kukoroma kwangu.

Nilibisha nikaona anaanza vituko, nikampiga mkwara usiku huu nilivyokuwa nimelala amerecord video fulani yangu nikiwa usingizini na kuniamsha.

Nilivyoamka akaniambia kuwa amechoka, anakosa usingizi kwasababu ya kulala kwangu. Nikataka kupiga mkwara kama kawaida yangu akanionyesha video, kuangalia hivi ni mimi kweli.

Nakoroma kama vile mtu ambaye ana maji kwenye koo, nikashindwa la kusema.

Naomba msaada kwa yeyote ambaye anaweza jua tatizo hili linachangiwa na nini na dawa yake ni nini.

Naomba anisaidie mwenzenu ndoa yangu mbichi kabisa lakini kwa style hii naona hatuna marefu uko mbeleni. Mimi situmii pombe, au sina kitambi sasa sijui tatizo litakuwa wapi?!

Sent using Jamii Forums mobile app
angalia style yako ya kulala. hapo manake hewa haingii na kutoka vizuri
 
Tiba za kuacha kukoroma ni surgery au mazoezi kupunguza unene nyamanyama

Unapolala mwili huwa una relax na muscles zote zina relax aka kulegea
Muscles za eneo la koo zinapo legea hushuka chini na kuzuia hewa kupita na kusababisha huo mkoromo

Anza na mazoezi sana
Punguza kula vyakula vya nyama nyekundu, mafuta, wanga na sukari sukari za viwandani zinazo patikana kwa wingi kwenye bia soda na juice
Kunywa maji kwa wingi angalau lita kuanzia tatu kwa siku
Epuka kulala kifudifudi

Ukishindwa hilo nenda kwenye surgery wakapunguze hizo nyama zinazolegea kwenye koo
 
Kuna siku kutokana na uhaba wa vyumba kujaa hapo nilipofikia nililala na dingi mdogo nilijuta ahsubuhi inaingia naiona sikulaa siku ile kwanza alisema tusizime taa kwamba ukizima taa mbu ndio wanakufaidi vizuri alipoanza tu kulala yule bwana alianza kukoroma huku anajamba usiku mzima.shughuli ndio ilikuwa hiyo sikulala siku 2 zote siku aliyoondoka kurudi mkoani nilifurahi sana nikawa mwenyewe nililala usingizi mzito mpaka saa 2 ndio kuamshwa na wenyeji wangu chai iko tayari
 
Padilisha mtindo wa kulala usitazame juu lalia ubavu, pili usile Sana usiku, vyakula mafuta mengi usiku acha kabisa mfano nyama unasinzia Sana asikuambie mtu. Piga mazoezi nahisi una uzito mkubwa Sana.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom