Msanii
Platinum Member
- Jul 4, 2007
- 22,690
- 29,909
Tarehe 19 Februari 2023 chama cha ACT Wazalendo walifanya mkutano wao wa Kwanza ambapo viongozi wake wa kitaifa walishiriki na kuongea na wananchi.
Cheche zilianza kuonekana pale aliposimama Makamu Mwenyekiti wa Zanzibar ambape pia ni makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar alipoelezea umma kuhusu ACT kuanzisha mchakato wa maridhiano ambao ulikuja baadaye kuwashirikisha CHADEMA lakini hilo halijawahi kusemwa popote.
Alisimama Mwenyekiti wa Taifa wa ACT ambaye naye alielezea miaka 7 ya giza ambapo vyama vilisitishwa kufanya shughuli zake za kisiasa, vyombo vya habari kutishiwa na kushughulikiwa endapo vitatoa habari zinazoikosoa serikali. Lakini hata waandishi na wanachi walioonesha mwelekeo huo walishughulikiwa kikatili na serikali.
Hatimaye alisimama mzee wa Terrible Teens yaani Kiongozi mmkuu wa Chama bwana Zitto ambaye bila hiyana alipita mulemule kuuelezea umma maswahibu ya wananchi kutokujua matumizi na udhibiti wa kodi zao hadi kununua madege ambayo mengine yapo grounded kwa sababu ya kutu.
Alipoanza kuelezea details za namna fedha za ndege zilivyotengwa na kununuliwa ndipo ghafla ITV walikata matangazo yao ambayo hapo awali tuliambiwa yatakuwa live hadi mkutano utakapoisha.
Hii ina maana kubwa sana. Inamaanisha kuwa pamoja na juhudi za Mama Samia kutuelezea namna anavyouthamini uhuru wa vyombo vya habari na vyama vya siasa kufanya shughuli zao, lakini kiuhalisia kazi bado sana na uhuru huo unaotolewa una mipaka yenye miba mikali.
Kinachofuatia ni ITV kuanza kumulikwa vikali na taasisi ya vipenyo na huko mbeleni msishangae wakapigwa dafrao kali huku mkishindwa kuunganisha nukta za tukio la jana.
Ninapinga vikali kitendo cha ITV kuamriwa kuuondoa matangazo ya live mkutano wa ACT Wazalendo pale Mbagala Zakhem siku ya tarehe 19 Februari 2023.