Kukatisha matangazo Mubashara ITV dhidi ya mkutano wa ACT Zakhiem

Msanii

Platinum Member
Jul 4, 2007
22,606
29,755
Tarehe 19 Februari 2023 chama cha ACT Wazalendo walifanya mkutano wao wa Kwanza ambapo viongozi wake wa kitaifa walishiriki na kuongea na wananchi.

Cheche zilianza kuonekana pale aliposimama Makamu Mwenyekiti wa Zanzibar ambape pia ni makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar alipoelezea umma kuhusu ACT kuanzisha mchakato wa maridhiano ambao ulikuja baadaye kuwashirikisha CHADEMA lakini hilo halijawahi kusemwa popote.

Alisimama Mwenyekiti wa Taifa wa ACT ambaye naye alielezea miaka 7 ya giza ambapo vyama vilisitishwa kufanya shughuli zake za kisiasa, vyombo vya habari kutishiwa na kushughulikiwa endapo vitatoa habari zinazoikosoa serikali. Lakini hata waandishi na wanachi walioonesha mwelekeo huo walishughulikiwa kikatili na serikali.

Hatimaye alisimama mzee wa Terrible Teens yaani Kiongozi mmkuu wa Chama bwana Zitto ambaye bila hiyana alipita mulemule kuuelezea umma maswahibu ya wananchi kutokujua matumizi na udhibiti wa kodi zao hadi kununua madege ambayo mengine yapo grounded kwa sababu ya kutu.

Alipoanza kuelezea details za namna fedha za ndege zilivyotengwa na kununuliwa ndipo ghafla ITV walikata matangazo yao ambayo hapo awali tuliambiwa yatakuwa live hadi mkutano utakapoisha.

Hii ina maana kubwa sana. Inamaanisha kuwa pamoja na juhudi za Mama Samia kutuelezea namna anavyouthamini uhuru wa vyombo vya habari na vyama vya siasa kufanya shughuli zao, lakini kiuhalisia kazi bado sana na uhuru huo unaotolewa una mipaka yenye miba mikali.

Kinachofuatia ni ITV kuanza kumulikwa vikali na taasisi ya vipenyo na huko mbeleni msishangae wakapigwa dafrao kali huku mkishindwa kuunganisha nukta za tukio la jana.

Ninapinga vikali kitendo cha ITV kuamriwa kuuondoa matangazo ya live mkutano wa ACT Wazalendo pale Mbagala Zakhem siku ya tarehe 19 Februari 2023.
 
Wacheni siasa za mipasho hizo.Hazina tija.Futa vyama vyote tutengeneze mfumo mwengine wa utawala si demokrasia na wala si ufalme.Kama tutashindwa kujiundia mfumo wetu basi afadhali tuchukue kidogo kutoka China.
 
Hivi hujui sheria za mikusanyiko mwisho ni sasa 12 jioni next time uwaeleze wasanii wa siasa waweke mambo ya msingi mapema sio kama ibada za kilokole.

USSR
Sheria hiyo inatekelezwa kwa wapinzani pekee?

Mara ngapi hata hivi karibuni CCM wanapitisha mikutano yao hadi kuzidi muda wa saa 12 alasiri?


Majibu mepesi sana mnatoa
 
Sheria hiyo inatekelezwa kwa wapinzani pekee?

Mara ngapi hata hivi karibuni CCM wanapitisha mikutano yao hadi kuzidi muda wa saa 12 alasiri...
Malalamiko ya aina hii yamesikika mara ngapi.CCM na chama chochote hawawezi kuacha vituko.Tunapoteza muda wa kufanya mambo ya maendeleo.

Mikutano yenu iwe ya ACT au CCM inapoteza pesa na muda wa watu kufanya kazi bure na hakuna cha maana munachozungumza,
 
Kuwa na adabu, kwani YANGA sio umma?? Unajua maana ya WANANCHI??
Milion 15 za Rais kwenda Yanga kwa anayehoji ni wazi hana ufahamu wa maana ya matumizi binafsi ya Rais.

Lakini ningeshangaa TAKUKURU wangesema watanunua magoli hayo
 
Wakati JPM anagawa mlikua mnalalamika hamkujua matumizi binafsi ya Rais?
Milion 15 za Rais kwenda Yanga kwa anayehoji ni wazi hana ufahamu wa maana ya matumizi binafsi ya Rais.

Lakini ningeshangaa TAKUKURU wangesema watanunua magoli hayo
 
Tarehe 19 Februari 2023 chama cha ACT Wazalendo walifanya mkutano wao wa Kwanza ambapo viongozi wake wa kitaifa walishiriki na kuongea na wananchi...
Muda wao wa maongezi waliolipa uliishia hapo walihitajika kuongeza salio!
 
Back
Top Bottom