Dorothy Semu: Nimekivusha Chama cha ACT Wazalendo kwenye mawimbi ya ukandamizaji wa Demokrasia

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,989
HOTUBA YA NDUGU DOROTHY-MANKA JONAS SEMU WAKATI KUCHUKUA FOMU YA KUWANIA NAFASI YA KUWA KIONGOZI WA CHAMA CHA ACT WAZALENDO

Ndugu watanzania
Ndugu viongozi, wanachama, wapenzi na wafuasi wa ACT Wazalendo kipekee wote mlionisindikiza kutoka kila kona kujumuika nami hapa katika tukio hili la kihistoria kwa taasisi yetu.

Huu ni uchaguzi wa tatu tangu kuasisiwa kwa ACT Wazalendo na kwa sasa ni lazima kuwa na KC mpya.
IMG-20240218-WA0006.jpg

Ndugu wanahabari nimefika hapa, baada ya tafakuri ya kina na uamuzi usio na shaka, utayari wa kuendelea kuwatumikia wana ACT Wazalendo nikiomba ridhaa wanitumetena kutumikia katika nafasi hii ya juu kuliko zote. Nimechukua fomu ya kugombea nafasi ya Kiongozi wa chama.

Dhamira yangu hii ya dhati inaongozwa na mambo matatu.Jambo la kwanza naamini katika uongozi wa pamoja, utumishi wa watu na kuonyesha njia ili kutimiza kwa ukamilifu malengo makubwa ya taasisi kuelekea ndoto ya ACT Wazalendo .
IMG-20240218-WA0007.jpg

IMG-20240218-WA0005.jpg

Mmenipima kwenye majukumu mbalimbali mlioniamini kwayo kwa miaka hii nane, baada ya kuwa mtumishi wa umma kwa miaka 17.

Nitaje machache, nilipokuwa Katibu Mkuu 2017-2020 nimekivusha chama kwenye mawimbi ukandamizaji wa kidemokrasia, mawimbi ya kufutiwa usajili na hata kwa pamoja kuvunja rekodi za usimamizi wa kifedhana kuwa chama kinachokua kwa kasi kuliko vyote Afrika.

Nikiwa Makamu Mwenyekiti Bara mwaka 2021 nilipewa jukumu jingine la kukaimu Uenyekiti wa chama baada ya kutangulia mbele za haki kwa aliyekuwa mwenyekiti wetu mpendwa Maalim Seif *Mungu amrehemu
na kukakikisha anapatikana Mwenyekiti mwingine kwa mfumo wa kidemokrasia kama matakwa ya katiba yetu ya chama.

Mmeniamini kiungozi, nami nimerudisha kwa kuwa mtumishi mwaminimifu, nisiyelega wala kukata tamaa.

Ninataka kutumia uzoefu wangu na karama yangu ya uongozi sasa kuongoza jahazi hili la ACT Wazalendo kwenye kushika hatamu za kuongoza taifa hili.

Jambo la pili, ninaamini katika wajibu mkubwa wa vyama shindani, uwepo wa chama hiki katika siasa za vyama vingi umeendelea kutoa tafsiri halisi ya nini wajibu wa vyama vya siasa katika siasa za ushindani katika kuleta sera za kimapinduzi za kubadilisha kabisa hali ya umaskini wa watu wetu.

Sera mbadala zenye tija, kuendeleza siasa za masuala ambazo chama chetu kimejitofautisha nazo na kuendelea kuwa kimbilio na sauti kuu ya kutafuta maisha ya neema kwa kila mtanzania.

Ninataka nafasi hii ya kiongozi wa chama kuendeleza dhima hii ambayo chama cha ACT Wazalendo imeibeba kwa miaka kumi sasa na matumaini inayotoa katika uongozi wa nchi yetu.

Ninataka kuongoza ndoto hii ya ACT Wazalendo kufikia mabadiliko chanya, ya kweli, ya kiuchumi, kijamii na kiutamaduni.

Nafasi nilizo watumikia za Katibu wa Sera na Utafiti na sasa Waziri Mkuu Kivuli zimeendelea kunipika na kunipa uzoefu mkubwa ndani na nje ya nchi.

Jambo la tatu, mahitaji ya sasa ya chama baada ya kupitia hatua za kuukua na kusalimika (growth and survival) ni uimarishaji wa chama hiki katika kila nyanja.

Ndugu zangu uongozi ni kujitoa, kufanya kazi kwa bidii na maarifa, kufanya kazi pamoja kutimiza malengo ya chama na maslahi ya watanzania.

Nafasi zote hizo nilizowatumikia tumeweza kwa kushirikiana na viongozi wenzangu Chama chetu kinahitaji kujisimika kwenye ngazi ya chama kinachosubiri kukabidhiwa kuongoza serikali. Huu ni wakati wa kukamilisha njia ya kuelekea kwenye ushindi.

Baada ya kufanya kazi kwa umakini mkubwa kwa miaka kumi hii sasa anatakiwa kiongozi wa chama atakayepokea joho (mantle), akiwa na ari, mbinu na uwezo wa kujenga juu mafanikio makubwa ya uongozi uliotangulia.

Nina kila uwezo wa kuendeleza jukumu hili kubwa.

Ninaomba ridhaa ya Wajumbe wa Mkutano Mkuu waTaifa utakaofanyika Machi 5-6 kuendelea kuwa na imani kwangu na kunichagua kuwa Kiongozi wa chama wa pili wa chama cha ACT Wazalendo.
Asanteni kwa kunisikiliza.

Dorothy Semu
18 Februari 2024
 
Ijapo kuwa ni muda mfupi ila nina kumbuka nyakati nzuri nilizokuwa nazo pamoja nanyi hapo makao makuu nadhani tulianzia maeneo ya sayansi kama sijakosea. Nawaombea mfike mbali ndugu zangu.
 
Back
Top Bottom