Kufanya kazi ya Ualimu ni hatari sana kwa maisha yako

Mama Edina

JF-Expert Member
Dec 18, 2022
747
1,814
Wanaosimamia maisha ya watu wameidharau Sana.

Wanatarajia watoto watendewe nini Kwa kutekeleza watendaji wake, hasa walimu. Fikiria Walimu Wakuu wanapata posho kwa kazi anazozifanya mwalimu wa kawaida. Ni kama utumwa.

Mratibu Elimu kata anapata posho ya kazi ipi wkat anayeteseka na Kaz ni mwalimu wa kawaida. Kuna watu huwaambiii kitu Ili waendelee kula.

Nimuombe Rais Mh Mama ufanye kitu
 
Wanaosimamia maisha ya watu wameidharau Sana.

Wanatarajia watoto watendewe nini Kwa kutekeleza watendaji wake, hasa walimu.


Fikiria Walimu Wakuu wanapata posho. Kwa kazi anazozifanya mwalimu wa kawaida. Ni kama utumwa.

Mratibu Elimu kata anapata posho ya kazi ipi wkat anayeteseka na Kaz ni mwalimu wa kawaida.

Kuna watu huwaambiii kitu Ili waendelee kula.

Nimuombe Rais Mh Mama ufanye kitu
Ukuu wa shule ni stress asimwambie mtu, Kuna wakati inakulazimu uweke pesa zako Kisha uendelee kuidai serikali vinginevyo mambo hayaendi.

Mkuu wa shule anastahili posho sio Kwa kimavi kile.
 
bf960b8b-1955-40fc-b285-8112cc88add2.jpg
 
Kiujumla hakuna kazi iliyo rahisi wala hakuna kazi yenye maslahi ya moja kwa moja.
Hata Urais ni kazi ambayo mwenye nayo hufikia hata kuijutia japo kisheria yupo juu ya wote na anawasaidizi wengi lakini bado haiwi nzuri moja kwa moja kwake sembuse ualimu ambao ni wito ambao sio kila mtu amejaliwa.

Ualimu ni huduma katika jamii ambayo huyo anaehudumu anakua amejaliwa Karama ya kufanya huduma hiyo.

Kwangu mimi mwalimu nashindwa kujua nimuweke nafasi ya ngapi kwa umuhimu wake pengine kuliko mtu yoyote baada ya mzazi.
Hapaswi kubezwa wala kulaumiwa au kutukanwa, ingawa ni binadamu anaweza akawa na mapungufu yake ila bado nafasi ya mwalimu ni ya kipekee kuliko hata upekee mwenyewe.

Mwalimu kulingana na Karama aliyojaliwa kuufanya wito na huduma ya ualimu ni mara chache sana anakatishwa tamaa na changamoto kama za kulipwa kidogo na kutokuthaminiwa na jamii yote, na hata kuto kukumbukwa.

Ndio maana waalimu wengi wamefikia uzee mzuri usio na changamoto za afya .
Mungu aendelee kuwa upande wao kwa kila hali na nyakati.
 
Back
Top Bottom