Mama Naa
JF-Expert Member
- Aug 31, 2020
- 385
- 950
Amani iwe juu yenu.
Ni jambo la kusikitisha sana tena mnoo kuona kada ya Ualimu haithaminiwi kabisa katika nchi ya ulimwengu wa tatu.
Humu Kuna mijadala mingi kuhusu Walimu na Ualimu lakini sisi wenye ndugu na jamaa zetu huko tunapata uhalisia ulivyo. Ualimu ni kazi ya ovyo tena iliyojaa ufukara na umaskini japo ukiwa nayo itakupa ugali maharage.
Sasa hivi kazi ya kuuza mihogo imekuwa Bora zaidi kuliko kuwa mwalimu.
Nina jamaa yangu ni mwalimu, kwako yeye Kila kitu ni ovyo kuanzia kula yake, Vaa yake, bata lake, mitoko yake na matibabu yake. Hawezi kukusanya hata 2M Kwa mwaka mzima labla akakope benki. Ikitokea Kuna harusi au msiba inabidi aende Maswi au Maboto ndio apate angalau 1M ya kutatua tatizo.
Wanaousifia Ualimu aidha ni wanasiasa au viongozi au hawana ndugu Wala jamaa kwenye hiyo kada vinginevyo huwezi kuusifia Wala kuutaka Ualimu.
Upande wa pili Nina jamaa yangu ambaye alikosa ajira akaamua kujiongeza Kwa kukaanga mihogo na kachumbali pale Ilala jijini Dar es salaam eneo la mchikichini.
Jamaa anatoa matumizi yote maji, umeme, chakula, Kodi, matibabu na matumizi mengineyo yote bado Kwa mwezi analaza laki sita.
Kwa mwezi = 600,000
Kwa mwaka = 7,200,000
Kwa miaka 5= 36,000,000
Kwa hiyo nchi hii KUUZA MIHOGO na kuwa MWALIMU Bora uuze mihogo.
Nimemaliza....