Dhana ya ualimu na mwalimu

Pesanyingi

JF-Expert Member
Apr 15, 2023
396
657
Hizi ni sababu zangu binafsi na kwa maono yangu kwanini walimu(ualimu) unadharaulika katika jamii ya hapa nchini.

Kwa wale ntakaowaudhi au kutowapendeza na uzi huu wavumilie kwa kila mtu ana mawazo yake na hatuwezi kufanana.

1. MFUMO WA UPATIKANAJI
Katika kuajiri walimu mimi naona unatumika mfumo ambao siyo mzuri kwani kuna watu wengi siyo wote hawana vigezo kama vile uelewa katika mambo mbali mbali ikiwemo kufundisha,ambao hupimwa kupitia mitiahani tu lakini face to face ukimhoji au kukutana nae utagundua hawafai kutuandalia vijana wetu.

2. KUROPOKA(KUELEZEA MATATIZO YAO KWA KILA MTU),hawa watu wamekuwa walalamishi sana tena kwa mtu yote yote hata kwa boda boda anaweza elezea changamoto za kazi yake bila kujali huyu ni nani na ana nafasi gani.

3.UGUMU WA MAISHA, kundi hili nadhani ndiyo kundi pekee ambalo halina posho ya kazi tofauti na kazi zingine zote navyojuwa,mimi wa uelewa wangu.Hivyo kuwapelekea kuwa na ugumu mkali wa maisha,mawazo mda wote na mwili kukosa nuru.Mbaya zaidi kwasababu ya uelewa wao hawajuwi wanahitaji nini au hitaji lao kuu kuwatoa hapo walipo.Serikali walipeni posho walimu nao ni wafanyakazi wenu hata katikati ya mwezi.Wao wanajuwa kudai ongezeko la mishahara tu kila mwaka.

4.UWOGA, kutokana na karibu 99.99% ya walimu kutoka katika familia za kimaskini basi nao wamekuwa waoga kwa kila mtu na kuishi kwa hofu muda wote kama digidigi.Ukitaka kuzulumu haki basi kundi rahisi ni walimu.

5. MIKOPO, Katika kundi nadhani namba moja linaloongoza kuburuzwa na mikopo hasa Ile kausha damu basi ni hawa ndug zetu,wamekuwa ni njia ya kuwatajirisha watu(taasi za kifedha) kupitia riba mbali mbali wanapo kopa hadi kuwa kero mitaani na jamii.

6. MABOSI WENGI, hapa mtendaji wa kijiji, balozi wa nyumba kumi, mgambo, mtendaji kata, afisa biashara, diwani, wafanyakazi wa masijala nk hawa wote na wengine wanaweza kumuamrisha na kuwapelekesha walimu wetu vile watakavyo na bila kuangalia umri.

7.DHANA YA UWALIMU NI WITO/KIOO CHA JAMII, kasumba hii imewatafuna hawa watu vibaya sana na kuwafanya kuwa duni na pia kuwafanya kundi lisilotakiwa kuwa fedha.Mfano zama hizi kumwambia mtoto(mwanafunzi) kuwa mwalimu ni kwa mfano labda siyo kizaki hiki na ndiyo maana hawana ushawishi hata kwa wanafunzi kwani kupitia elimu waliyokuwa nayo hawana tofauti na ambao hawajasoma tena wanazidiwa mambo mengi tu na ambao walikataa shule.Huwezi kumwambie mtoto asome awe na maisha bora wakati wewe unayemshauri huna maisha bora.
Ushauri kwa serikali,iweke vigezo vya ufauli mzuri kwa wanaotaka kusomea uwalimu wawe wenye div one na pia iwe lazma wapitie jkt .Hapa tunaweza kupata malimu watakao kuwa na msaada kwenye taifa hili tofauti na sasa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom