T2015CCM
JF-Expert Member
- Sep 13, 2012
- 7,931
- 987
Utafiti unaonyesha kuwa kwa kipindi cha miaka miwili na ushee tangu CCM iingie madarakani na kuunda serikali, chama hicho kimezidi kuimarika mara dufu zaidi tofauti na ilivyokuwa 2015.
Utekelezaji wa ilani unaofanywa na Serikali yake, utatuaji wa kero za wananchi, ukaribu wa chama hicho na wananchi wake waliokiweka madarakani unazidi kukipaisha huku vyama vya upinzani vikizidi kudorora.
Chama kinachodorora zaidi ni CUF kikitafunwa na mgogoro wa ndani baina ya viongozi wake wakuu wa kitaifa. CHADEMA inazidi kupukutika na kufanya kuwa chama cha pili kwa kudorora kunakosababishwa na kukimbiwa na viongozi wake kwa kasi kubwa hususani madiwani zaidi ya 55 kujiuzulu nafasi zao na wenyeviti wa mitaa na vijiji 300 hali kadhalika pamoja na mbunge mmoja.
CHADEMA pia kinatafunwa na mgogoro wa kimya kimya wa uongozi wa chama hicho ambapo kundi kubwa la viongozi hawamkubali mwenyekiti wao lakini yeye anajisimika kwa mabavu na kwa kutumia fedha.
ACT cha ZITTO kinapambana na hali yake kuchukua nafasi ya upinzani lakini nacho kina hali mbaya sana ambapo viongozi wake kadhaa wa kitaifa wamejivua uanachama na kuhamia vyama vingine ikiwamo CCM. Amebaki ZITTO peke yake akipiga kelele huku na kule.
Upinzani ujitathmini!