Kubenea kumwagiwa tindikali: Nini chanzo?

Status
Not open for further replies.
Majibu ya maswali ya Mzee Mwanakijiji yataendelea kupatikana kutokana na kesi inavyozidi kuchemka mahakamani.
a. Kwa kuchukulia matukio kama hayo yaliyopita tunaweza kukubali kuwa kuna watu waliopigwa,waliotendewa vitendo vibaya na wakajikuta pabaya mbele ya jamii na hata kuhama miji yao.
b.Mtu anayefanya madhara kwa kisingizio chochote bila shaka inabidi afikishwe mahakamani.
c.Mtu akiwa hana ujasiri wa kumshughulikia mwizi wake na hana jinsi anaweza kutafuta msaada kwa marafiki.
d.Kutumwa hakuwezi kuwafanya waepuke mkono wa sheria.
e.Si halali kukodisha watu walipize kisasi ila haya mambo hutokana na hasira ya aliyetendewa.
f.Kama Kubenea alifanya hivyo na yule mama hakwenda polisi ina maana walikuwa wanafanya siri.Baada ya mume kugundua ndipo alipohamaki na kufanya alivyoamua.

Ukweli wa saga hili utapatikana mahakamani.
 
Huyo mama yeye yuko wapi katika hili? Je ataitwa kama shahidi? Na akija na kusema hakuwa na uhusiano wa kimapenzi na Kubenea itakuwaje kwa hawa watuhumiwa?
 
Here we go again... classic case of divide and rule...

Wenyewe wanatucheka sana kwa malumbano haya yasiyo na kichwa, miguu wala mkia!

Read between the lines... those who know the truth will spare no expense at letting those who dont know the truth, NOT know it!
 
f.Kama Kubenea alifanya hivyo na yule mama hakwenda polisi ina maana walikuwa wanafanya siri.Baada ya mume kugundua ndipo alipohamaki na kufanya alivyoamua.

Hakuna cha hasira wala nini hapa hapono mtu.Hapa wanamwangamiza huyo aliyewatuma. Kukodi watu ni kitendo unachokipanga ukiwa na akili timamu na ukijua nini unafanya.
Hili siyo suala la kufumaniana guest then unampatia kipigo.
 
Huyo mama yeye yuko wapi katika hili? Je ataitwa kama shahidi? Na akija na kusema hakuwa na uhusiano wa kimapenzi na Kubenea itakuwaje kwa hawa watuhumiwa?

tusipredict mambo mkuu, mahakama ipo na inajua kazi zake.

au wewe unataka lazima iwe ya kisiasa kwa kuwa kubenea alikuwa akiandika habari za siasa?

tuwe wakweli na tusisukumwe na hisia na mori.

kama kubenea amekuwa akichukua wake za watu tutajua na kama amesingiziwa tutajua pia
 
Mtu wa Pwani, ni wewe uliyesema kwa uhakika kuwa ilikuwa ni sababu ya kufumaniwa na hukusubiri mahakama..ni mimi niliyejenga hoja ya mahakama. ...halafu kosa ni kuwa kesi iliyoko mahakamani siyo ya kuhusu kubenea kuchukua mke wa mtu.. au wewe ndivyo unavyoichukulia?

Maana kama ingekuwa hiyo huyu aliyechukuliwa mke yuko wapi?
 
wanasiasa wanajua kucheza faulo bwana sasa naona kesi imegeuzwa imeelekea kwa wanamtandao (experts wa kuchafua watu) kubenea anahitaji msaada jamani,,hakuna mtanzania ataekubaliana na huo utetezi kwamba alichukua mke wa mtu
 
Niliwahi uliza hapa JF " KUBENEA HAWA NDIO WATESI WAKO?" Sikujibiwa na mpaka leo mzee anakukuruka na mahakama lakini hatuna jibu, ujumbe wangu kwake "Kama unafanya ufisadi kwa kula Mapapai ya watu basi ni wajibu wako kukiri hadharani kuwa wewe ni FISADI HALISI"[/QUOTE/]
NAMJUA VEMA KUBENEA,NAJUA MAPUNGUFU YAKE NI YA KIBINADAMU,MWITENI NA MUMSHAURI AACHE WAKE ZA WATU,ANACHEMKA NA NAVYOJUA MIMI HATA PALE WAMEMPA CHA MTOTO KWA KAWAIDA WATU KAMA WALE HUWA WANA WASODOMA NA WANAPIGWA PICHA KWA KUMBUKUMBU.
 
wanasiasa wanajua kucheza faulo bwana sasa naona kesi imegeuzwa imeelekea kwa wanamtandao (experts wa kuchafua watu) kubenea anahitaji msaada jamani,,hakuna mtanzania ataekubaliana na huo utetezi kwamba alichukua mke wa mtu


Nakusamehe bure kwa kuwa inawezekana hujui uchungu wa mke.kwa taarifa yako wanaume wengi sana wamekufa kwa kufata wake za watu.kila siku tunasikia matukio ya mauaji kwa ajili ya wake za watu.au unadhani kubenea akichukua mkeo ni baraka?mpe mke wako ndio tujue kama huo utetezi hautoshi.
 
Mkuu Fisadi,

Heshima mbele, hivi hiyo tabia unayosema wanafanyiwa watu kama Kubenea, inafanyiwa hata viongozi wa taifa au wananchi tu walalahoi wanaoandika ufisadi wa viongozi kama Kubenea!

Maana tunaweza kukupa dataz za viongozi wetu wakuu na wake za wananchi, je utayafanya hayo uliyoyasema hapo juu ya kusodoma na kupiga picha za kumbu kumbu? au!
 
Mkuu Fisadi,

Heshima mbele, hivi hiyo tabia unayosema wanafanyiwa watu kama Kubenea, inafanyiwa hata viongozi wa taifa au wananchi tu walalahoi wanaoandika ufisadi wa viongozi kama Kubenea!

Maana tunaweza kukupa dataz za viongozi wetu wakuu na wake za wananchi, je utayafanya hayo uliyoyasema hapo juu ya kusodoma na kupiga picha za kumbu kumbu? au!
Kaka aliyosema fisadi ni kweli,japo wanayofanya si taratibu wala sheria inategemea na hasira za alieibiwa mkewe.wakubwa ni wakubwa hata adhabu wanazopata wezi wa kuku za kuchomwa hawazipati wakubwa.Hivyo kwa kuwa wakubwa hawafanywi kitu basi ndio inahalalisha kubenea apige wake za watu?
 
1. Kaka aliyosema fisadi ni kweli,japo wanayofanya si taratibu wala sheria inategemea na hasira za alieibiwa mkewe.

2. wakubwa ni wakubwa hata adhabu wanazopata wezi wa kuku za kuchomwa hawazipati wakubwa.

3. Hivyo kwa kuwa wakubwa hawafanywi kitu basi ndio inahalalisha kubenea apige wake za watu?

Hivi mkuu Dikteta,

Kwanza heshima mbele, kweli swali nililouliza linafanana na hili jibu?

Halafu, Kubenea ameanza lini kula wake za watu? Alianza siku ile alipotoka kuhojiwa na kamati ya Mwakyembe kuhusiana na Richimnoduli, au ni hivi karibuni?
 
duh ni kweli yataibuka mengi hio ya Ali karume kudai mkewe amemendewa na mgombea mwenzake, sijawahi kusikia

Mtu wa Pwani, hujawahi kusikia kuwa Kikwete (akiwa waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa) alimtokea mke wa Karume (akiwa balozi Uswizi)?
 
hii kali, sidhani kama mna ukweli wowote.

amtokee iwe bifu halafu amwache aendelee na ubalozi?
 
Kubenea: Tulishambuliwa kwa chuki

na Asha Bani

MKURUGENZI na Mhariri Mtendaji wa magazeti ya MwanaHalisi na Mseto, Saed Kubenea, ameiambia mahakama kwamba kushambuliwa kwake kulitokana na chuki za viongozi wa serikali wanaoandikwa na magazeti yake juu ya vitendo vya ufisadi.

Alidai hayo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, alipokuwa akitoa ushahidi katika kesi ya kumwagiwa tindikali, akiongozwa na Kamishna Msaidizi wa Polisi Charles Kanyella, mbele ya Hakimu Addy Lyamuya.

Akielezea zaidi, Kubenea alidai kuwa wakati akiwaanika viongozi wanaofanya ufisadi serikalini, mawakili wanaotumiwa na viongozi hao ambao aliwaita mafisadi, wamekuwa wakimwandikia barua za vitisho ili aache kufanya hivyo, vinginevyo watampeleka mahakamani.

Mbali na vitisho vya mawakili wa viongozi hao, alidai kuwa Msajili wa magazeti nchini amekuwa akitumiwa kumkaripia kwa kumwandikia barua za kumuonya mara kwa mara na kumkataza kuandika habarai hizo huku akimtaka kubadili msimamo wa gazeti hilo.

“Kuvamiwa kwangu kunatokana na mambo ya kisiasa, ambayo kwa miaka miwili tangu kuanzishwa kwa gazeti la MwanaHalisi, nimekuwa na msimamo wa kuandika habari za uchambuzi wa masuala ya siasa, jamii, biashara ikiambatana na kuwaandika viongozi mafisadi,” alidai Kubenea.

Aliendelea kueleza kuwa, siku ya tukio akiwa katika ofisi za MwanaHalisi saa mbili usiku, alisikia mlango wa ofisi yake ukigongwa na kusukumwa kwa nguvu. Kubenea alidai baada ya kusikia hivyo aliamua kwenda mlangoni na kumhoji aliyegonga huku akichungulia kupitia katika vioo lakini hakufanikiwa kumtambua mgongaji kwa vile alikuwa gizani.

Alieleza kuwa siku hiyo alikuwa na mshauri wa magazeti hayo, Ndimara Tegambwage, aliyemtaka kufungua ili amjue anayegonga mlango huo. Alidai baada ya kufungua mlango, aliamriwa kukaa chini na watu watatu walioingia ndani ya ofisi hizo, lakini walikaidi amri hiyo na ndipo walipoanza kumshambulia.

“Baada ya kuniambia nikae chini niligoma ndipo wakaanza kunishambulia kwa panga na mtu mwingine ambaye sikumuona alikuwa ameshika kikopo na kunimwagia maji maji usoni ambayo yalikuwa yanauma sana,” alidai Kubenea.

Alidai baada ya kushambuliwa zaidi, aliingia katika chumba kingine cha ofisi ambapo alikwenda kutafuta silaha ya kupambana nao lakini alishindwa kupata, akaamua kuvunja kioo cha ofisi akidhani atafanikiwa kupata kioo cha kupambana nao lakini kioo kile kilidondoka kwa nje.

Alieleza baada ya kuona hakuweza kufanikiwa, aliamua kutoka ili kuweza kupambana nao hivyo hivyo, lakini aliwakuta wameshaondoka na kumuona Ndimara akiwa anavuja damu nje ya ofisi na watu wakiwa wamemzunguka.

Kubenea alidai baada ya hapo walifanikiwa kupata usafiri na kuelekea hospitali, huku Polisi kutoka Kituo cha Oysterbay walikuwa wamefika katika eneo la tukio tayari kwa kuchukua maelezo.

Mbali ya maelezo hayo, Kubenea alidai kumtambua aliyekuwa anamjeruhi ambapo alimtaja kuwa ni mtuhumiwa namba moja Alex Anyimike, ambaye mbali na kumtambua mahakamani, aliweza pia kumtambua katika gwaride la utambulisho lililofanyika katika Kituo cha Polisi Oysterbay.

Katika utambuzi wa watuhumiwa, Kubenea alikana kuwatambua watuhumiwa wengine kwa kuwa hakuwaona wakati wa tukio na kudai waliokuwepo katika tukio ni watuhumiwa wengine, ambao hawajakamatwa na akiwaona atawatambua pia.

Wakati akiendelea kutoa ushahidi wake alidai hadi sasa kutumiwa meseji za vitisho na kwamba kabla ya kutokea kwa tukio alitumiwa meseji nzito kupitia namba 0787 775 692, aliyodai ilikuwa ikitumika mara kwa mara kumtumia ujumbe wa vitisho.

Mwendesha Mashitaka alimuomba hakimu kupokea meseji hizo kama kielelezo kitakachotumika mahakamani kama ushahidi lakini kutokana na ujumbe huo haukuchapishwa kwenye karatasi (IT) haukupokelewa.

Hakimu Lyamuya alimwambia Mwendesha Mashitaka Kenyella kulifanyia kazi hilo kwa kuchapisha ujumbe huo na kuutoa kama kielelezo Juni 16. mwaka huu.

Hata hivyo ushahidi wa Kubenea ulikatishwa baada ya Kenyella kuiomba mahakama kuendelea kutolewa Mei 19 na leo Ndimara atapanda kuendelea na ushahidi wake.

Washitakiwa katika kesi hiyo ni Alex Mwandemele (Chusu), mfanyabiashara na mkazi wa Kigogo; Hashim Mdoe (Madilu), dereva wa teksi na mkazi wa Tegeta; Augustino Joseph (Cheusi), mfanyabiashara na mkazi wa Mwananyamala.

Wengine ni Hamis Almasi Ramadhani; fundi wa kuchomea na mkazi wa Mwananyamala; Alfred Bernard Moshi (Chambya), fundi umeme, mkazi wa Kinondoni; na Ferdinand Msepa.

Source: Tanzania Daima
 
Mnajua viongozi wanatufanya sisi wajinga kwa sababu sisi wenyewe tunakubali kuwa ni wajinga. Mbona huyu mfanyakazi wa Bharesa hawamtaji kama mtuhumiwa mkuu kama yupo, hiki ni kituko kikubwa sana, kama kweli yupo alitakiwa kuwa mtuhumiwa namba moja, lakini wanasema tu wala hawamtaji, halafu na sisi hapa tunabisha na makada RA na EL bila kujiuliza swali la msingi.

Hawa wanaojifanya wanamjua sana kubenea kwa kuiba wake za watu watuambie mtu gani ameshitakiwa aliyeibiwa mke na kutoa tenda ya kumwagia tindikali kubenea.

Otherwise ni mafisadi ndo waliwatuma kama hawataki kusema ukweli waache wakaozee gerezani, na huko watakuta jamaa wenye uchungu na nchii hii wanawasubiri wawape fundisho.
 
Nafikiri tunahitaji kujua zaidi kwani mi naona kama kuna harufu ya uongo tena mkubwa, wanajaribu tu kupindisha ukweri ili waweze kudifend interest zao pamoja na hao wanaowajua. Kaka kubenea naamini haya yanayosemwa si kweri na ukweri waujua. sisi si wajinga wote tunafahama mambo hizi zi zama zile za watanzania wa kuburuzwa. infact hayo maelezo hayaingi kichwani.

to the right we will stand
 
sasa nyinyi mshaamini upande mmoja tu kama kubenea kashambuliwa kwa ajili ya ufisadi, nyinyi mnahukumu kabla ya ushahidi haujatimia.

jee haiwezekani kuwa mkuu alikuwa mzuri wa kuwazunguka waume na kuwalia wake zao?

jee haiwezekani haya yametokea coincedence na kwa vile nyinyi mnapenda aonekane shujaa na sio fisadi?

wakati utatwambia kama kubenea ni fisadi kama fisadi wengine

fisadi si lazima aibe pesa za wananchi tu
 
sasa nyinyi mshaamini upande mmoja tu kama kubenea kashambuliwa kwa ajili ya ufisadi, nyinyi mnahukumu kabla ya ushahidi haujatimia.

jee haiwezekani kuwa mkuu alikuwa mzuri wa kuwazunguka waume na kuwalia wake zao?

jee haiwezekani haya yametokea coincedence na kwa vile nyinyi mnapenda aonekane shujaa na sio fisadi?

wakati utatwambia kama kubenea ni fisadi kama fisadi wengine

fisadi si lazima aibe pesa za wananchi tu

Na Fisadi Kiwembe ambae utajwa sana kwenye nyimbo za taarabu na mipasho huwa na sifa zipi?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom