Kongole Serikali kwa kutoa fedha ununuzi wa vifaa tiba na dawa

Apr 9, 2022
66
32
Mkurugenzi wa MSD, amedhibitisha kuwepo kwa ongezeko la upatikanaji wa Bidhaa vya afya kwa mwaka 2022/2023, ambapo ambapo juni 2022, ongezeko lilikuwa kwa asilimia 51, na kupanda hadi asilimia 64, juni 2023, wakati upatikanaji wa dawa kwa sasa umefikia asilimia 82, mwezi juni 2023 kutoka asilimia, 57 juni 2022.


Ongezeko hilo limechangiwa na Serikali ya awamu ya sita, kutoa fedha za kutosha kwa ajili ya kufanya ununuzi wa dawa na vifaa tiba pamoja na kusambazaji wake katika vituo vya afya.

Akizungumza na Wahariri wa Vyombo vya Habari katika mwendelezo wa vikao vya mpango kazi unaoratibiwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina, Mkurugenzi wa Bohari ya Dawa ya Taifa (MSD), Mareva Tukai, ametoa taarifa ya utendaji, mafanikio, na mwelekeo wa MSD.

Amesema katika kuimarisha upatikanaji wa dawa na vifaa tiba unazingatiwa, wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuzuia uagizwaji wa dawa kutoka nje ya nchi na badala yake wataendelea kusimamia uzalishaji dawa wa ndani kwa viwango vinavyohitajika.

Akizungumzia maboresho yaliyofanywa na MSD pamoja na mikakati iliyopo, Tukai amesema wameimarisha mifumo ya usimamizi kwenye ununuzi, kwa kushirikisha balozi zilizopo China, Algeria, Urusi na Korea Kusini kutafuta wadau wa uzalishaji na ununuzi, lakini pia wataendelea kushirikiana na sekta binafsi katika kuanzisha na kusimamia viwanda vya bidhaa za afya.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jukwaa la wahariri (TEF), Deodatus Balile akizungumza kwa niaba ya wahariri ameishauri serikali kulipa deni wanalodaiwa na MSD, ili kuwezesha upatikanaji wa dawa na vifaa tiba kwa uharaka, pamoja na kupongeza ushirikiano uliopo kati ya MSD na sekta binafsi.
 
Back
Top Bottom