Je, ni kweli NHIF wameondoa baadhi ya vifaa tiba (kama vile gloves) katika kitita kipya cha huduma?

JUMA JUMA

JF-Expert Member
Jan 5, 2013
666
835
JE NI KWELI NHIF WAMEONDOA BAADHI YA VIFAA TIBA KAMA GLOVES KATIKA KITITA KIPYA CHA HUDUMA?

Hivi karibuni kumekua na mjadala mkubwa wa kwamba kitita kipya cha NHIF kimeondoa baadhi ya vifaa tiba vinavyotumika katika huduma za kitabibu mathalani gloves, gauze na bandages.

NHIF wanasema gharama ya hizo za vitendanishi ziko ndani ya gharama za huduma husika na hivyo mwanachama hatakiwi kudaiwa malipo ya fedha taslim. Melezo haya yanaeleweka kwa namna hii;

Tuchukue mfano; gharama ya gloves box moja ni Tsh 5000 na ndani kuna pair 12, badala ya kila mgonjwa kulipiwa Tsh 5000 watachangia gharama ya hilo box hivyo itakua 5000/12=417. Kwa hiyo badala ya bima kulipa Tsh 5000 kwa kila mgonjwa italipia glove pair moja kwa Tsh 600 hivyo mpaka gloves zinaisha pesa ya kununua box jipya zitakuwepo na faida itakuwepo. Zamani hospitali walikua wanapata super profit kila mgonjwa akilipiwa box jipya Tsh 5000 alikua anapata 5000*12= 60,000, ukitoa gharama ya gloves na faida kidogo alikua anapata faida ya kama Tsh 50,000 kwa wagonjwa 12 waliotibiwa. Ambapo sasa atapata faida ya uhalisia ya Tsh 1356 (kumbuka faida kwenye afya haitakiwi kuwa kubwa inayozidi 10% ya gharama za uendeshaji).

Tuchukue mfano rahisi, marafiki 12 wana sherehe ambayo wanapanga kunywa soda moja moja, kreti la soda moja linauzwa Tsh 12,000/= busara inaelekeza kwamba kila mshiriki anapaswa kuchangia kiasi flani cha fedha ili kufikia lengo la kununua kreti. Hivyo Tsh 12,000/12 = 1,000. Kwa mantiki hii kila mtu akichanga Tsh 1000 kreti litanunuliwa na sherehe itafanyika, kama tunataka kupitia mchango huu tuweke na gharama zingine basi tunaweza ongeza Tsh 200 au 300 itapatika na hela ya keki. Lakini sio sawa kumwambia kila mtu anunue kreti zima ilhali atakunywa soda moja tu.

Jambo lingine ilikua gharama za baadhi ya dawa kutoendana na uhalisia na kuwa mzigo kwa wagonjwa mfano dawa ya kutibu kansa inayoitwa Trastuzumab 150mg bei ya kununulia sokoni ni Tshs 722,400, bei ya kitita kipya ambayo NHIF italipa hospitali ni Tsh. 929,120 lakini dawa hiyo kuna hospitali X inataka kumuuzia mwananchi Tsh 2,300,000. Hii sio sawa kwa ustahimilivu wa ukwasi wa Mfuko pamoja na kumuumiza mwanachama wa NHIF.

Hivyo tujitahidi sana kuwa wasikivu kwa vyanzo sahihi vya taarifa. Nyakati kama hizi ni muhimu sana kuwatambua Fake Experts.

Dkt. Johanes Martin MD MSc
Dar es Salaam
18.03.2024
 

Attachments

  • IMG-20240320-WA0219.jpg
    IMG-20240320-WA0219.jpg
    33.5 KB · Views: 2
NHIF acheni kujitetea, mfuko umeishiwa hela kwasabb serikali imechota hela kwenye mfuko na mabosi wa NHIF pia wamechota hela.

Hivi unafirkiri kinachotozwa huko hospitali binafsi ni bei ya dawa na vifaa tiba pekee? Na unadhani kinachowafanya watu wakimbilie hospital binafsi ni tiba na dawa tu?? Lugha nzuri, kujali, muda mfupi wa kusubiri huduma, usalama wa mgonjwa na mazingira masafi. Yote haya ni kivutio na yanapaswa kulipiwa.

Ushawahi kujiuliza kwann soda kwa mama ntilie inauzwa 700, migahawani inauzwa 1000, hoteli za kawaida 1500 na hoteli zenye nyota inauzwa 3000?
 
Back
Top Bottom