Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba yabaini Kiwanda Bubu Arusha kinachotengeneza Dawa Bandia za mifugo

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,987
Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) Kanda ya Kaskazini kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha iliendesha operesheni maalum ya kuwasaka watu wanaojihusisha na uzalishaji wa dawa bandia ambapo mamlaka hiyo imefanikiwa kubaini kiwanda bubu ambacho kinatengeneza dawa bandia za mifugo aina ya vidonge maeneo ya Murieti Jijini Arusha.

Akiongea na waandishi wa HabarI Mkaguzi wa Dawa kutoka Mamlaka ya Dawa na vifaa tiba kanda ya kasikazini Dkt. Furaha Nyunza amesema wamefanya operesheni hiyo kutokana na uwepo wa Daw bandia zinazoingizwa sokoni kinyume na taratibu za uuzaji wa dawa na vifaa tiba hapa nchini.
da11.JPG

da1.JPG

Amesema opersheni hiyo imefanyika nchi nzima huku ikihusisha vyombo vingine vya ulinzi na usalama ambapo ilipelekea kubaini uwepo wa dawa bandia katika maeneo tofauti hapa nchini na kiwanda bubu kinachotengeneza dawa hizo kilichokamatwa maeneo ya Murieti Jijini Arusha.

Dkt Nyunza amebainisha kuwa Uchunguzi umeonyesha kuwa kiwanda hicho kimekuwa kikitengeneza dawa pasipo kusajiliwa ambapo amewataka wazalisha wa ndani ya kufuata taratibu za usajili wa viwanda vya uzalishaji wa dawa katika mamlaka ya dawa na vifaa tiba hapa nchini.

Aidha amebainisha kuwa operesheni hiyo ni endelevu huku akiwaomba wananchi kuendelea kushirikiana na mamlaka ya dawa na vifaa tiba kwa kutoa taarifa za watu wawache wanaofanya uzalishaji wa dawa katika mazingira ambayo wanamashaka nayo ili mamlaka hiyo ifanye chunguzi kubaini kama wanazalisha dawa kwa kufuata taratibu.
da.JPG

Ametoa wito kwa watengenezaji wa dawa kutengeneza bidhaa salama kwa watumiaji huku akiwataka kufanya usajili wa viwanda vyao katika mamalaka ya dawa na vifaa tiba ili kutoingia katika mkono wa dora kwa kukiuka taratibu za uzalishaji dawa husika.
 
Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba Kanda ya Kaskazini kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha iliendesha operesheni maalum ya kuwasaka watu wanaojihusisha na uzalishaji wa dawa bandia ambapo mamlaka hiyo imefanikiwa kubaini kiwanda bubu ambacho kinatengeneza dawa bandia za mifugo aina ya vidonge maeneo ya Murieti Jijini Arusha.

Akiongea na waandishi wa HabarI Mkaguzi wa Dawa kutoka Mamlaka ya Dawa na vifaa tiba kanda ya kasikazini Dkt. Furaha Nyunza amesema wamefanya operesheni hiyo kutokana na uwepo wa Daw bandia zinazoingizwa sokoni kinyume na taratibu za uuzaji wa dawa na vifaa tiba hapa nchini.
View attachment 2831756
View attachment 2831757
Amesema opersheni hiyo imefanyika nchi nzima huku ikihusisha vyombo vingine vya ulinzi na usalama ambapo ilipelekea kubaini uwepo wa dawa bandia katika maeneo tofauti hapa nchini na kiwanda bubu kinachotengeneza dawa hizo kilichokamatwa maeneo ya Murieti Jijini Arusha.

Dkt Nyunza amebainisha kuwa Uchunguzi umeonyesha kuwa kiwanda hicho kimekuwa kikitengeneza dawa pasipo kusajiliwa ambapo amewataka wazalisha wa ndani ya kufuata taratibu za usajili wa viwanda vya uzalishaji wa dawa katika mamlaka ya dawa na vifaa tiba hapa nchini.

Aidha amebainisha kuwa operesheni hiyo ni endelevu huku akiwaomba wananchi kuendelea kushirikiana na mamlaka ya dawa na vifaa tiba kwa kutoa taarifa za watu wawache wanaofanya uzalishaji wa dawa katika mazingira ambayo wanamashaka nayo ili mamlaka hiyo ifanye chunguzi kubaini kama wanazalisha dawa kwa kufuata taratibu.
View attachment 2831758
Ametoa wito kwa watengenezaji wa dawa kutengeneza bidhaa salama kwa watumiaji huku akiwataka kufanya usajili wa viwanda vyao katika mamalaka ya dawa na vifaa tiba ili kutoingia katika mkono wa dora kwa kukiuka taratibu za uzalishaji dawa husika.
Ingefaa aweke hapa aina ya dawa za bandia zinazotengenezwa na kiwanda hicho ili waumiaji tusizinunue maana kama hajazitaja bado ziko madukani na tutaendelea kuzitumia bila kuzitambua
 
Nchi yetu raha sana. Mtu anaanza ujasiriamali,mpaka anafika hatua anazalisha bidhaa hatujui?

Ukiacha uzembe wa watendaji ,hata sisi watz tuwazembe sana. Tuna tabia ya kufuga uhalifu.

Uzunguni ukijamba, ushuzi ukiwa si wa kawaida ,mtu anaweza kupiga simu polisi akidai umepuliza kemikali yenye kudhuru.

Kuna uwezekano huu uzembe umesababishwa na haohao watendaji baada ya kuwa na poor feedback.
 
Back
Top Bottom