Komu aliuza ushindi wa Chadema Moshi Vijijini

Kuwanyima wananchi haki yao ni usaliti mkubwa na ni kitu ambacho hakiweze kuachwa hivi hivi. Sasa kama kuna mtu mwenye ushahidi wa data basi aweke wazi ili tujue ukweli. Otherwise hizi ni habari za udaku tu.
 
Huu udaku umesambaa mno. Kuna huko Bukoba, Nkenge, n.k. CHADEMA wafanye uchunguza kama sehemu ya kujipanga.
 
nilichelewa sana kuanzisha hii thread kwa sababu nilidhani ningeweza kupata data. watu walianza kulalamika kidogo kidogo. sasa hivi ni gumzo kila kona moshi vijijjini kwamba Komu aliuza nguvu za wananchi. mawakala 20 ambao nimeongea nao idadi ya kura waliyonayo inaonesha Komu kuongoza kwa zaidi ya kura 2000. lakini hii siyo sababu ya kusema kwamba alishinda, isipokuwa mawakala hao waliwasiliana na wenzao pia na wengi wanashangaa Chami alipata ushindi vituo gani.

chadema moshi vijijini watoe edadi ya kura katika kila kituo cha kupigia kura walizopokea kutoka kwa mawakala. kwa kuwa mawakala wanafahamiana na wanatumia simu, itakuwa rahisi kila wakala kuhakiki kama idadi ya kura zilizotolewa na Ofisi ya Chadema ndizo wakala huyo alizituma alizozituma. Hii itasaidia kurudisha imani kwa wananchi ambao sasa wanaamini wamedhulumiwa.

Hata baba yangu mwenye miaka 70 haamini kama Chami alishinda kwa idadi ya kura

Huu ndio tunaita usaliti, kweli watu wanajitoa kwenda kupiga kura alafu unawatusi kwa kurubuniwa, tena nasikia aliuza kwa bei ya kipumbavu 50M. Kama ni ukweli asipate amani yeye wala kizazi chake.
 
Kuna mazungumzo hapa moshi vijijini kwamba mawakala wa chadema wanaamini kwamba mgombea wao ndugu Komu aliuza ushindi wa chadema akidhani ulikuwa ushindi wake. Mawakala wote wanadai Komu aliongoza katika vituo vyote na wananchi walipigana kufa na kupona. Wanajilaumu kutokumlinda mgombea wao. Wamevunjika moyo sana. Ni usaliti unaokatisha wananchi tamaa

Inawezekana yanayosemwa ni kweli. Kwanza nashangaa kigezo ambacho CHADEMA kilitumia kumpa Komu wadhifa wa Mkurugenzi wa Fedha na Utawala. Ni kweli kuwa Komu amenza siasa (uanaharakati) kuanzia Chuo Kikuu Dar es salaam, baadaye NCCR na sasa CHADEMA; na ni graduate wa BA Economics. Hata hivyo, hayo pekee hayatoshi kumpa Komu cheo kikubwa hivyo. Komu ni mtu mwenye tamaa tangia akiwa kiongozi pale UDSM. Kama CHADEMA inataka kusonga mbele, ni bora ikapangua safu ya uongozi, ikiwemo ya kumtoa Komu katika nafasi hiyo.

Siku moja mtasikia kilio cha CHADEMA kwenye vyombo vya habari kama Komu ataendelea na wadhifa alio nao sasa.
 
Bora umesema, na nyie viongozi kama mna masikio na msikie. Tusifanye majaribio na maisha ya watu, mlifikia vipi kumpa huo wadhifa haituhusu, ila watu wameumizwa na hawana imani naye kwa chochote.
 
Kuna mazungumzo hapa moshi vijijini kwamba mawakala wa chadema wanaamini kwamba mgombea wao ndugu Komu aliuza ushindi wa chadema akidhani ulikuwa ushindi wake. Mawakala wote wanadai Komu aliongoza katika vituo vyote na wananchi walipigana kufa na kupona. Wanajilaumu kutokumlinda mgombea wao. Wamevunjika moyo sana. Ni usaliti unaokatisha wananchi tamaa

Hii kama ni kweli basi ni hatari, data zaidi please!! :tape::tape::tape:
 
Bora umesema, na nyie viongozi kama mna masikio na msikie. Tusifanye majaribio na maisha ya watu, mlifikia vipi kumpa huo wadhifa haituhusu, ila watu wameumizwa na hawana imani naye kwa chochote.

Pengine kuna ambalo limo ndani ya mioyo ya wachangiaji dhidi ya Komu ambayo yamefichika! Nilifuatilia sana na kuona jitihada nyingi wanachadema wakiwa na Komu walivyokuwa wanawania kile kiti. Hii ni pamoja na uchakavu mwingi wa magari aliyokuwa anayatumia, na uhaba wa kifedha. Ninafahamu pia baada ya uchaguzi kulikuwa na zogo kubwa wakati kura zinahesabiwa na kutofautiana, hasa za madiwani wa Kibosho. Huyu mnayemsema ana tamaa, sijawahi kuona tamaa ndani yake. Kwa miaka yote aliyokaa katika nafasi ya Ukurugenzi wa Fedha kule NCCR na CHADEMA, ungetegemea kama angekuwa mtu wa tamaa basi angekuwa na magari ya kisasa na ya kifahari, lakini hana! Muulize Zito atashuhudia hili! Angekuwa na nyumba ya kisasa, HANA, Nenda Tegeta uone nyumba yake!

Mnamtuhumu bure mtoto wa watu, na zaidi ya tuhuma hamna ushahidi wowote! Badala yake mnakiri alikuwa mwanaharakati tangu UDSM (early 1990s), ushuhuda kwamba amejitolea kupigania hizo harakati na sio kwenda kujitajirisha kama wengine walivyofanya!

Sidhani ukurugenzi wa Fehda na Utawala kama ni taalamu mahsusi (NGOJA ukurugenzi wa Fedha ni taaluma, ukurugenzi wa utawala ni taaluma, lakini zikichanganywa?)! Katika nafasi kama hii unahitaji mtu wa ujumla na nadhani Economist anafaa lakini ni lazima mtu awe strategist, sasa sijui kwa kiasi gani unayetuhumu kuhusu yeye kuwa Mkurugenzi unajua Komu ni strategist kiasi gani? Hujiulizi tu inakuwaje unasikia CHADEMA wamepata hela fulani fulani, wamefanya kile, na hiki, wafikiri hizi ni mana kutoka mbinguni! La hasha! Jua siku zote kuna mtu jikoni anapika na sisi tulio sebuleni tunasubiri chakula tusianze kuwakoroga wapishi, wataharibu mapishi.

Hoja hii iko binafsi mno na haina mshiko(data) naona nimepoteza muda hata kuijibu!
 
Kuna mazungumzo hapa moshi vijijini kwamba mawakala wa chadema wanaamini kwamba mgombea wao ndugu Komu aliuza ushindi wa chadema akidhani ulikuwa ushindi wake. Mawakala wote wanadai Komu aliongoza katika vituo vyote na wananchi walipigana kufa na kupona. Wanajilaumu kutokumlinda mgombea wao. Wamevunjika moyo sana. Ni usaliti unaokatisha wananchi tamaa

Cooked
 
Kuna haja ya kuwa waangalifu na kufanya utafiti wa kina kabla ya kuanza kushutumu. Lazima tufahamu siasa ni mchezo wa kuharibiana, nguvu ya CHADEMA imeonekana dhahiri, wapinzani wa CHADEMA sio wajinga wakae kimya tu, watatafuta kila njia kupandikiza chuki dhidi ya chama na wapenzi au wapiga kura ili chama kionekane ni cha wababaishaji. Mtasikia mengi kuhusu wagombea wa Chadema na chadema kama chama, tuwe macho na hizi propaganda!
 
Zito na komu wamo ndani ya jungu moja. Wanapikiwa zengwe watoke. Nadhani wameingia chadema kimakosa. I believe they have something in common! What is it?? Sijui ila najua
 
mimi bado nasisitiza kwamba chadema wabandike hapa janvini idadi ya kura zote za jimbo la moshi vijijini kwa kila kituo cha kupigia kura, ili mawakala wa chadema waweze kuoanisha na za kwao. naamini ni kwa njia hii tunaweza kutatua hili tatizo kama tunataka jimbo la moshi vijijini 2015.

kuna watu wanazungumzia tofauti kati ya kibosho na uru, nadhani hata Komu anaweza kuwa alichukulia mtazamo huu kuwa unaweza kufanya wananchi wakaamini kwamba kweli ameshindwa. naomba niwahakikishie wanajanvi kuwa katika uchaguzi huu hicho hakikuwa kigezo katika upigaji kura. kigezo kilikuwa kimoja tu, kwamba ama ccm au chadema.

tukumbuke kwamba kuna muingiliano mkubwa na wa karibu sana kati ya wananchi wa moshi mjini, kibosho, na Hai. Moto wa chadema moshi mjini na Hai uliambukiza Kibosho nzima. wakibosho wakaamua hawadanganyiki na tofauti za ukibosho na uuru. Pia safari hii wakibosho hawakutaka kuonekana ni wabaguzi, kwanza hawana akili ya namna hiyo. wao huangalia uwezo wa mtu na siyo anakotoka.

sasa hivi wakibosho wanatembea vichwa chini mbele ya watu wa Hai na Moshi mjini, wanasemwa kwamba wameendekeza ukabila kuchagua ccm. lakini wao wanataka uthibitisho kwamba ni kijiji kipi hasa ambacho kilimpa Chami kura, na ni kura kiasi gani.

naomba chadema waweke wazi hili jambo kwani mimi niliamini tofauti za kibosho na uru ndizo zilipeleka jimbo hili kwa ccm, hadi nilipowasiliana kwa karibu sana na rafiki zangu wa kibosho, na kupata bahati ya kutembelea vijini vitatu katika kata za kibosho.
 
Kuna mazungumzo hapa moshi vijijini kwamba mawakala wa chadema wanaamini kwamba mgombea wao ndugu Komu aliuza ushindi wa chadema akidhani ulikuwa ushindi wake. Mawakala wote wanadai Komu aliongoza katika vituo vyote na wananchi walipigana kufa na kupona. Wanajilaumu kutokumlinda mgombea wao. Wamevunjika moyo sana. Ni usaliti unaokatisha wananchi tamaa

Huyu Komu haa mimi nilimpigia kura japo simfahamu.
 
naheshimu mawazo ya watu wanaotaka Komu aenguliwe ukurugenzi wa fedha chadema, lakini siungi mkono hilo. kwamba amenunuliwa ni hisia za wapiga kura wake, ninachodai hapa ni yeye na chadema kujisafisha ili kurudisha imani ya waliopigania chadema na waliopigia chadema kura. naomba pia msifananishe hii thread na zile zinazoeneza chuki kwa baadhi ya viongozi wa chadema.

kama tuna kaki ya kuomba kura kwa wananchi pia tuna wajibu wa kujieleza pale ambapo wanahisi hatukuwatendea haki. ni hatari kubwa kwa chadema wananchi kufika hatua ya kuamini wamesalitiwa na chadema!!
 
binafsi yangu sidhani kama hili la kuuza nguvu ya umma halikutokea kabisaaaa lakini ni vizuri kukubali si vyema kumnyooshea mtu kidole pasipo eveidence. lazima tukubali hata wale waliojitokeza sio wote 100% walikuwa na nia thabiti ya kutetea watanzania na chadema kwa ujumla lazima mamluki walikuwepo kwa dhamiri za ubinafsi wao... katika msururu wa mamba ni vigumu kumkosa kenge...ila sio sahihi kukata tamaa kwa uchache wa uwepo wa watu wa staili hiyo lazima siku moja watagundulika maana njia ya mwongo siku zote ni fupi na hujuikana mapema tu.
nawakilisha..
 
Kuna mazungumzo hapa moshi vijijini kwamba mawakala wa chadema wanaamini kwamba mgombea wao ndugu Komu aliuza ushindi wa chadema akidhani ulikuwa ushindi wake. Mawakala wote wanadai Komu aliongoza katika vituo vyote na wananchi walipigana kufa na kupona. Wanajilaumu kutokumlinda mgombea wao. Wamevunjika moyo sana. Ni usaliti unaokatisha wananchi tamaa

Ndugu habari yako.Kabla hujaandika habari nzito kama hizi unatakiwa kwanza ukae chini na utafakari kwa kina.Inawezekana wewe unaona hili ni jambo dogo sana lakini kumbuka uancheza na maisha ya watu hapa.Hivi unamfahamu Komu au umesikia tu?Komu hawezi kuuza jimbo kwa kuwa anafahamu Ubunge is worth than any amount of money.Yaani apigane weee halafu mwishoni auze jimbo,haiwezekani.Jamani sio kila manchokisikia ni cha ukweli muwe mnajaribu kupambanua kwanza.Inasikitisha sana!!!!
 
mimi bado nasisitiza kwamba chadema wabandike hapa janvini idadi ya kura zote za jimbo la moshi vijijini kwa kila kituo cha kupigia kura, ili mawakala wa chadema waweze kuoanisha na za kwao. naamini ni kwa njia hii tunaweza kutatua hili tatizo kama tunataka jimbo la moshi vijijini 2015.

kuna watu wanazungumzia tofauti kati ya kibosho na uru, nadhani hata Komu anaweza kuwa alichukulia mtazamo huu kuwa unaweza kufanya wananchi wakaamini kwamba kweli ameshindwa. naomba niwahakikishie wanajanvi kuwa katika uchaguzi huu hicho hakikuwa kigezo katika upigaji kura. kigezo kilikuwa kimoja tu, kwamba ama ccm au chadema.

tukumbuke kwamba kuna muingiliano mkubwa na wa karibu sana kati ya wananchi wa moshi mjini, kibosho, na Hai. Moto wa chadema moshi mjini na Hai uliambukiza Kibosho nzima. wakibosho wakaamua hawadanganyiki na tofauti za ukibosho na uuru. Pia safari hii wakibosho hawakutaka kuonekana ni wabaguzi, kwanza hawana akili ya namna hiyo. wao huangalia uwezo wa mtu na siyo anakotoka.

sasa hivi wakibosho wanatembea vichwa chini mbele ya watu wa Hai na Moshi mjini, wanasemwa kwamba wameendekeza ukabila kuchagua ccm. lakini wao wanataka uthibitisho kwamba ni kijiji kipi hasa ambacho kilimpa Chami kura, na ni kura kiasi gani.

naomba chadema waweke wazi hili jambo kwani mimi niliamini tofauti za kibosho na uru ndizo zilipeleka jimbo hili kwa ccm, hadi nilipowasiliana kwa karibu sana na rafiki zangu wa kibosho, na kupata bahati ya kutembelea vijini vitatu katika kata za kibosho.

Kama umeweza kutupatia habri hizi kutoka kwa mawakala kwnini basi usilete na hizo idadi ya kura walizopata wagombea wote?weka halafu tuzichambue.Ukiamua kufanya jambo fanya kwa ukamilifu wake.
 
Mimi napendekeza apatikane mtu akusanye data toka kwa mawakala wa CHADEMA na kama ikidhihirika kuwa ni kweli jamaa kahujumu wenzake, basi mawakala wawafikishe mahamani mpokeaji na mtoa rushwa, ili kutoa fundisho kwa wengine kuwa kura za wazalendo sio za kuchezea!
 
Wakuu,

Naona yale yaliyotokea NCCR yanaanza kutengenezwa hapa. CHADEMA inatengenezewa zengwe kusambaratisha uongozi wake
na naona wanaanza kwa uchonganishi. UNLESS KUNA SOLID EVIDENCE THIS THREAD IFUNGWE
 
Back
Top Bottom