Ubunge Moshi Vijijini 2025 pamoto

Jun 20, 2023
55
52
Harakati za chini kwa chini za kuwania jimbo la Moshi vijijini zimeanza kwa kasi ya kutisha huku zikizongwa na siasa za kuchafuana kwenye mitandao ya Kijamii.

Mbunge wa Sasa wa jimbo Hilo ,Profesa Patrick Ndakidemi anazongwa na upinzani mkali kutoka kwa makada wenzake ambao wameanza kujijenga kisiasa kuelekea 2025.

Baadhi ya madiwani (CCM)wametangaza wazi wazi kujitenga na mbunge wao hasa wanaotoka jimbo la Moshi Vijijini Hali ambayo inatajwa kuleta mgawanyiko mkubwa.

"Kama chama hakitakemea hii tabia nakuambia 2025 jimbo tunalikowa,haiwezekani huu uasi ndani ya chama uangaliwe bila watu kuchukuliwa hatua"anaonya kada wa CCM.

Kwa upande wake Ndakidemi anakili kuwepo kwa mpasuko huo ambao inadaiwa unafadhiliwa na kigogo mwenye ushawishi mkubwa wa kisiasa katika jimbo Hilo ambaye anadaiwa kuwaweka mfukoni aslimia kubwa ya madiwani.

Anasema ni Bora wenye Nia ya ubunge waache wabunge walioko madarakani watimize majukumu yao ya kuwatumikia wananchi na wakati ukifika nafasi itatolewa kila mwenye Nia achukue fomu",anasema.

Anasema si jambo lenye afya kuanza kuchafuana kwa sababu ya kusaka ubunge na kwamba jambo Hilo halikijengi chama Bali linakibomoa akidai badala ya kuwaza kuwapa watu maendeleo watu wanavurugana wenyewe kwa wenyewe kwa kujitengenezea nafasi.

"Tusubi wakati ufike kila mmoja atoke kuomba nafasi hiii kama viongozi wetu wa chama wanavyosema wapltupe muda wabunge tulioko madarakani tutekeleze majukumu yetu kwani wote ni CCM na tunajenga nyumba moja"anasema.
 
Jimbo la moshi vijijini limekuwa halina mbunge wa kudumu kutokana na uchapakazi wake tangu enzi za mrema kabla jimbo hilo halijagawanywa na kupata jimbo la vunjo. Kila uchaguguzi wanapata mbunge mpya wa upinzani au wa ccm. Jimbo hilo huwa na wagombeaji wengi sana ndani ya ccm na vyama vya upinzani. Kuna vijana wadogo wapo huwa wanajaribu na kuishia kwenye kura za maoni za vyama vyao. Ni kawaida mbunge wake kuongoza muhula mmoja tu muhula wa pili hutupwa nje
 
Hii ni kweli tangu 1995 Moshi haijawahi kumilikiwa na chama, ila wanaangalia upepo, ila mbunge atakayekumbukwa kwa sana ni Cyril Chami tu, alifanya mengi sana ya kukumbukwa ila alishindwa 2015 sababu ya vijana walitaka mabadiliko bila kujali uzuri wa mbunge anaetoka ccm
 
Hii ni kweli tangu 1995 Moshi haijawahi kumilikiwa na chama, ila wanaangalia upepo, ila mbunge atakayekumbukwa kwa sana ni Cyril Chami tu, alifanya mengi sana ya kukumbukwa ila alishindwa 2015 sababu ya vijana walitaka mabadiliko bila kujali uzuri wa mbunge anaetoka ccm
Mimi namkumbuka kwa kutolewa uwaziri R.I.P.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom