Profesa Ndakidemi, Mbunge Moshi vijijini na fitna za wanajimbo

Ruwamangi

JF-Expert Member
Jun 23, 2020
949
1,683
Mbunge wa Moshi Vijijini Profesa Ndakidemi.

Ni mbunge anaesakamwa na watu wasiomtakia mwema kuanzia kwenye chama chake mpaka kwa wapiga kura. Chuki hizo zinakolezwa na wasaka ubunge kwenye jimbo hilo liliko kaskazini mwa Tanzania.

Madiwani na baadhi ya viongozi wa Chama cha Mapinduzi wamekuwa wakimlaumu Mheshimiwa huyo kwa hoja kwamba ameshindwa kutimiza ahadi kwa wananchi na hivyo viongozi wa chama na madiwani kuwa kwenye wkati mgumu mbele ya wapiga kura wao.

Chanzo cha habari kinathibitisha kuwa nyuma ya kauli hizo kuna watu wenye malengo na nafasi ya ubunge katika jimbo hilo moshi Vijijini.

Duru za kisiasa jimboni hapo na kwa wazaliwa wanaoishi nje ya jimbo hilo zinawataja vigogo wawili wa chama hicho ambao wameanza kujipitisha kwa wananchi.

Chanzo cha habari kinawataja vigogo hao kuwa mmoja ni mwakilishi wa wananchi katika kata moja na mwingine aliwahi kuwa diwani wa chadema na kurudi ccm ambako nyota yake iling'aa 2020 ndani ya chama hicho cha Mapinduzi.
 
2025 KAZI IPO, KUNA WABUNGE WATAPIGWA CHINI...HUYU AKIWEMO
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom