ABEDNEGO
Senior Member
- Aug 20, 2009
- 109
- 30
Kundi la wezi wenye silaha mbali mbali usiku wa kuamkia leo wamevamia Ofisi za Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania -Usharika wa Kimara -Korogwe na kuiba mali nyingi na fedha taslim kwa kuwafunga na kuwakatakata mapanga walinzi wa Chui Security Company .Baadhi ya samani zilizoibiwa ni pamoja na Computer zote ,TV Sets,PA systems nk.Wezi hao walitumia gas kuvunja sefu ya kuweka fedha pamoja na milango ya magrill kuingia ofisini hapo.Tukiwa kwenye sehemu ya tukio askari wa doria walifika baada ya kuitwa tangu alfaajiri saaa kumi hadi saa moja kasoro.Hii ni mara ya pili kwa Kanisa hili kuvamiwa kwa mwaka huu,Mara ya kwanza lilivamiwa mwezi Juni wakati washarika wakiwa kwenye mkesha magari yakaibiwa vifaa mbali mbali,huku walinzi wakiuchapa usingizi.
Tuanatoa pole kwa Washarika wa Kimara na Mchungaji wao Rev.Wilbrod Mastahi
Tuanatoa pole kwa Washarika wa Kimara na Mchungaji wao Rev.Wilbrod Mastahi
Last edited: