Watapatatabusana
Member
- Jul 30, 2018
- 13
- 12
MGOGORO unafukuta katika Kanisa la Kiinjili la Kirutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini Usharika wa Hai mjini baada ya Baraza la Usharika kuwasimamisha viongozi wake watatu kwa madai ya kuvamia na kuvuruga kikao cha uongozi Usharika na Waimbaji.
Baadhi ya Viongozi wanaotajwa kusimamishwa ni pamoja na Mwenyekiti wa Uamsho Ndeakomfoo Shoo, Mweka Hazina Clotilda Massawe na Katibu wa Uamsho Joseph Robert ambao wote kwa pamoja wamekwisha pokea barua ya kusimamishwa iliyosainiwa na Mchungaji Kiongozi wa Usharika wa Hai mjini na Kugonjwa Muhuri wa kanisa.