Ni Mchungaji Wilbroad Mastai wa Kimara au Dkt. Elioina Kimaro wa Kijitonyama?

Ngongo

JF-Expert Member
Sep 20, 2008
18,932
31,178
Mkutano Mkuu wa KKKT uliofanyika Chuo Kikuu Makumira Arusha ulimchagua Askofu Dr Malasusa kuwa Mkuu wa kanisa KKKT.

Mabadiliko ya katiba ya KKKT Mkuu wa Kanisa hatakuwa tena Askofu wa Dayosisi. Kwakuwa Askofu Dr Malasusa ni Mkuu wa KANISA atalazimika kuachia nafasi yake ya Mkuu wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani.

Inatarajiwa sasa nafasi ya Askofu Mashariki na Pwani itagombewa baina ya Mchg Matsai Usharika wa Kimara na Mchg Dr Kimaro wa Usharika wa Kijitonyama.

Ifahamike sana Mkuu wa Kanisa KKKT atakuwa na nguvu kubwa na yale magomvi au ubabe wa baadhi ya Maskofu wa Dayosisi mbali mbali yanakwenda kudhibitiwa na katiba ya sasa.
 
Mchg Chadiel Ajuaye Lwiza Msaidizi wa Askofu ni mmoja ya wachungaji wanaotajwa tajwa.
 
Back
Top Bottom