KKKT Kimara wavamiwa

ABEDNEGO

Senior Member
Aug 20, 2009
109
30
Kundi la wezi wenye silaha mbali mbali usiku wa kuamkia leo wamevamia Ofisi za Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania -Usharika wa Kimara -Korogwe na kuiba mali nyingi na fedha taslim kwa kuwafunga na kuwakatakata mapanga walinzi wa Chui Security Company .Baadhi ya samani zilizoibiwa ni pamoja na Computer zote ,TV Sets,PA systems nk.Wezi hao walitumia gas kuvunja sefu ya kuweka fedha pamoja na milango ya magrill kuingia ofisini hapo.Tukiwa kwenye sehemu ya tukio askari wa doria walifika baada ya kuitwa tangu alfaajiri saaa kumi hadi saa moja kasoro.Hii ni mara ya pili kwa Kanisa hili kuvamiwa kwa mwaka huu,Mara ya kwanza lilivamiwa mwezi Juni wakati washarika wakiwa kwenye mkesha magari yakaibiwa vifaa mbali mbali,huku walinzi wakiuchapa usingizi.

Tuanatoa pole kwa Washarika wa Kimara na Mchungaji wao Rev.Wilbrod Mastahi
 
Last edited:
Kundi la wezi wenye silaha mbali mbali usiku wa kuamkia leo wamevamia Ofisi za Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania -Usharika wa Kimara -Korogwe na kuiba mali nyingi na fedha taslim kwa kuwafunga na kuwakatakata mapanga walinzi wa Chui Security Company .Baadhi ya samani zilizoibiwa ni pamoja na Computer zote ,TV Sets,PA systems nk.Wezi hao walitumia gas kuvunja sefu ya kuweka fedha pamoja na milango ya magrill kuingia ofisini.Tukiwa kwenye sehemu ya tukio askari wa doria walikuja baada ya kuitwa tangu alfaajiri saaa kumi hadi saa moja kasoro.

Tuanatoa pole kwa Washarika wa Kimara na Mchungaji wao Rev.Wilbrod Mastahi


Too bad!
Poleni sana washarika wa Kanisa hilo.
Hali ya ubabe inazidi kushamiri hapa nchini!
 
Duu poleni sana. kwa nini hawajapeleka hizo pesa bank jamani hapo wamekomba sadaka zote za jumapili.
 
Poleni sana Jamani, Inasikitisha sana kuona jinsi watu wasivyojali utu
 
Doooo Pesa zetu za sadaka wamezigawana maharamia.....doo wataalaaniwa haoo..hawatafika popote na pesa za walalahoi tulizotoa kwa Mungu
 
Dawa ni moja tu nayo ni kufunga na kuomba na kuona watu hawa wanarudisha mali hizo walizoiba
 
........Amen! Kupitia tukio hilo, hao wezi watatubu na kuokoka kabla hawajawa wainjilisti!!
 
Wengine tunatoa sadaka wao wanaiiba, kweli dunia inakwisha hata Mungu aliewapa hizo nguvu wanamchezea?
 
Sijui kama kwenye Biblia kuna maandiko ya kuwaombea wawe ndondocha kama wenzetu wanavyowasomea albadri ili wapate kichaa, wenye ufahamu na hilo tuelezeeni tuwaombee waehuke, lakini sijawhi sikia hilo kwenye biblia
 
Sijui kama kwenye Biblia kuna maandiko ya kuwaombea wawe ndondocha kama wenzetu wanavyowasomea albadri ili wapate kichaa, wenye ufahamu na hilo tuelezeeni tuwaombee waehuke, lakini sijawhi sikia hilo kwenye biblia

Tusiwaombee wawe ndondocha, itakuwa bora tukiwaombea kwanza watambue kuwa ni dhambi, pia waache hiyo dhambi si kanisani tuu, bali mahali popote wasiibe tena. Pia wamfahamu Bwana Yesu kuwa ni mwokozi wao, ili waweze kuurithi ufalme wa mbinguni na pia kupitia wao na watu wengine waokoke
 
Poleni wanaKKKT Kimara. Mungu anazo sababu kwa nini ameruhusu jambo hilo kutokea. Lililopo ni kummuliza Mungu awaelimishe makusudi yake katika hili mpate somo kwa ajili ya baadaye. Uzuri ni kwamba Mungu anajua kujitetea, hatawaacha wezi hao kushamiri kwa sadaka ambazo watu wa Mungu wamezitoa wakfu kwa kazi yake. Nimewaona wengi waliofanya mzaha kama huo juu ya pesa iliyopitia madhabahuni, hali zao hutatamani kuwa nazo. Mungu anajua atakavyoshughulika nao.

Utakuwa na bahati kubwa kama utaiba mali ya madhabahuni na ukapelekwa mahakamani, vinginevyo wakikunyamazia na Mungu akaamua kutumia tratibu zake,....... utajuta kuzaliwa. Pesa zile zimesemewa neno na waliozitoa kwa nadhiri kabisa, wazee wa Kanisa wameyasogeza matoleo hayo madhabahuni na Mchungaji au Mwinjilisti au Kiongozi yeyote ameyaombea kwa Mungu. Hapo tena sio mali ya Kimara, ni mali ya Mungu. Compyuta na vifaa vyote walivyoiba kwa kawaida vinawekwa wakfu kwa sala kabisa na Mungu anavitakabari kwa kazi zake. Huyo anayevichukua hawaibii wnaKimara, anamwibia Mungu kwa kumtishia kwa bunduki. Upo hapo?

Nawatakia macho yenye kuona na masikio yenye kusikia wezi hao, na vichwa vyenye akili nzuri.

Leka
 
Tusiwaombee wawe ndondocha, itakuwa bora tukiwaombea kwanza watambue kuwa ni dhambi, pia waache hiyo dhambi si kanisani tuu, bali mahali popote wasiibe tena. Pia wamfahamu Bwana Yesu kuwa ni mwokozi wao, ili waweze kuurithi ufalme wa mbinguni na pia kupitia wao na watu wengine waokoke

Amina
 
BWANA YESU awahurumie, ashughulike na dhamiri zao huko waliko wajutie dhambi zao kisha warudishe hizo mali na kuokoka.
 
Mola ajaribiwi. nafikiri hawa watu lazima mufikishe malalamiko yenu kwa mola na yeye atawahukumu.
 
hata katika nyumba ya ibada?well hao wezi ndo mwisho wao sasa,hawafiki mabali,next sunday wenyewe watakuja kutoa ushuhuda ibadani!! tunasali pamoja
 
our country is a gangster mob!from Ufisadi to armed robbery!Both they need sever punishment.I am sure the latter will be caught,as ones who terrorised NMB Temeke!
But Ufisadi mob are walking free
 
kundi la wezi wenye silaha mbali mbali usiku wa kuamkia leo wamevamia ofisi za kanisa la kiinjili la kilutheri tanzania -usharika wa kimara -korogwe na kuiba mali nyingi na fedha taslim kwa kuwafunga na kuwakatakata mapanga walinzi wa chui security company .baadhi ya samani zilizoibiwa ni pamoja na computer zote ,tv sets,pa systems nk.wezi hao walitumia gas kuvunja sefu ya kuweka fedha pamoja na milango ya magrill kuingia ofisini hapo.tukiwa kwenye sehemu ya tukio askari wa doria walifika baada ya kuitwa tangu alfaajiri saaa kumi hadi saa moja kasoro.

Tuanatoa pole kwa washarika wa kimara na mchungaji wao rev.wilbrod mastahi
poleni sana washirika
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom