Kizazi gani hiki?

Speaker

JF-Expert Member
Aug 12, 2010
6,324
2,238
Ina sikitisha kwamba tabia hii bado ipo hadi leo.
Nakumbuka nikiwa mdogo (ingawa ilitokea mara moja tu) mjomba
wangu aliwahi nichapa kwakua nilienda kumuwashia sigara na nilipo
mpelekea ikawa ime zimika.

Na alinambia ikiwaka tu,ivute kidogo ili isizimike ndo uniletee.
Nashukuru Mungu niliondoka pale mapema sana sijui ningekuwa wapi.

Lakini hadi leo tabia za kutuma watoto wadogo wa washe sigara bado zipo.
Tuna tengeneza kizazi gani?

427758_309520412441667_100001511310375_842005_1378749658_n.jpg
 
hilo fulana limeandikwa summer,halafu manzese pale bigbrother wapo wengi sana hata kikwete anatumia hiyo je wananchi wake!hahahaha kweli hii nchi ya sigara.
 
Yawezekana katumwa awashe au kapewa apulize.
Lakini nani kamfundisha?
Nini chanzo cha yeye kufanya anacho fanya?
Yaweza kuwa kajifunza mwenyewe kwa kuangalia watu wengine .
ama ni tabia ya kitoto tu anataka kujaribu kila kitu.
?
 
Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo, kama mzazi umemzoelesha mtoto kumtuma akuwashie sigara usimshangae ukimkuta anavuta sigara make we ndo utakuwa umemfundisha
 
Nakumbuka kabinti kangu wakati kapo kadogo, kuna shemeji yangu alikuja kututembelea akakaa kama mwezi hivi. alikuwa anavuta sigara. sasa binti akapenda sana uvutaji, si akawa anaokota vipisi vya sigara anawasha, hakuna mtu anajua. siku nikashangaa, mbona unanuka sigara? mwenyewe alikuwa anaita sigere, akaniambia niliokota ile uncle aliitupa, kichapo alichopata, ilikuwa siku yake ya mwisho kuokota vipisi
 
Ahhh! sigara nisivyo ipenda yani kwangu hata ash tray hakuna,kama unavuta basi utavutia nje ukimaliza uingie ndani...
 
Hiki kizazi ni corrupted balaa! Mbaya zaidi wavuta sigara wanaona cyo issue kumtuma mtoto wakati imeandikwa explicitly kabisa ONYO: UVUTAJI WA SIGARA NI HATARI KWA AFYA YAKO...(GRRRRRRRRRRRRRRRRRRR)
 
Mkuu speaker, kitu cha kwanza unachopaswa kujua ni kwamba wafutaji wengi wa sigara ni selfish. Wanapenda kujitazama wao tu then furaha yao nikupata kile wakitakacho wao. Hapa kitaani kwetu kana jamaa mmoja mshamba sana., daily yeye ni kutuma mtoto kibandani kununua sigara moja moja, yani huyo dogo kwa siku hakosi kibandani zaidi ya hata mara 24, na maana kila baada ya nusu saa dogo anafata mzigo. Hii ni aina ya usumbufu pia!
 
Yaweza kuwa kajifunza mwenyewe kwa kuangalia watu wengine .
ama ni tabia ya kitoto tu anataka kujaribu kila kitu.
?

Wala simlaumu mtoto,nawalaumu wazazi/walezi wake
na watu wote wa mtaani kwake.
Kesho akiwa kibaka ni hao hao walo mfundisha mambo ya hovyo
ndio watakao mchoma moto.
 
Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo, kama mzazi umemzoelesha mtoto kumtuma akuwashie sigara usimshangae ukimkuta anavuta sigara make we ndo utakuwa umemfundisha

Yawezekana kama mzazi humtumi mtoto au huvuti
kabisaaaa,lakini huko anakopita toka shule hadi afike nyumbani
labda amesha vutishwa,...na wewe kama mzazi uko mbali nae
hata hug humpi utajua lini anavuta?
 
Ahhh! sigara nisivyo ipenda yani kwangu hata ash tray hakuna,kama unavuta basi utavutia nje ukimaliza uingie ndani...

Nakumbuka kwenye umri wa "kujaribu jaribu" niliwahi vuta pia.
mafua niliyo kuwa nayapata sijawahi experience maishani,kama unakufa vile
ya nikipenda ni kama mchanganyiko wa damu.
Nilijitahidi mara 3 tu,...na toka hapo niliichukia sigara.
 
Malezi ya watoto pia yanachangia kwa kiasi kubwa ku corrupt kizazi cha sasa. Ni vizuri kuwa makini na familia zetu hususan watoto na mama zao.
 
hii yote inatokana na kuiga yale yanayofanywa na jamii, hapa wa kulaumiwa ni wanajamii!
 
Mkuu speaker, kitu cha kwanza unachopaswa kujua ni kwamba wafutaji wengi wa sigara ni selfish. Wanapenda kujitazama wao tu then furaha yao nikupata kile wakitakacho wao. Hapa kitaani kwetu kana jamaa mmoja mshamba sana., daily yeye ni kutuma mtoto kibandani kununua sigara moja moja, yani huyo dogo kwa siku hakosi kibandani zaidi ya hata mara 24, na maana kila baada ya nusu saa dogo anafata mzigo. Hii ni aina ya usumbufu pia!

Haha,yaani 24 kwa siku?
Duh,kuna mzee alinisimulia kaanza kuvuta akiwa sekondari.
Hadi leo ana wajukuu wako sekondari lakini bado anavuta tena sio chini
ya 3 kwa siku.

Kinacho nishangaza ni kwamba HAJAFA anapeta tu sijui mapafu yake yana hali
gani saivi,wengine ukijaribu siku mbili
tu unakohoa kama ndo unataka kutoa roho,una nuka mdomo...............
 
hilo fulana limeandikwa summer,halafu manzese pale bigbrother wapo wengi sana hata kikwete anatumia hiyo je wananchi wake!hahahaha kweli hii nchi ya sigara.

Mheshim rais wako wewe.Acha kuumia lugha chafu.Unauhakika na unachokisema.Mtakuja pata laana kwa Mungu nyie shauri yenu.
 
Yawezekana kama mzazi humtumi mtoto au huvuti
kabisaaaa,lakini huko anakopita toka shule hadi afike nyumbani
labda amesha vutishwa,...na wewe kama mzazi uko mbali nae
hata hug humpi utajua lini anavuta?

Bora avutishwe sigara kuliko bangi!
 
Back
Top Bottom