Kizazi gani hiki?

Uvutaji wa sigara ni hatari kwa maisha yako.

Inatia huruma mtoto mdogo kama huyo kuvuta sigara.
 
hii yote inatokana na kuiga yale yanayofanywa na jamii, hapa wa kulaumiwa ni wanajamii!

Kweli,na sijui kwanini kusiwe na vibanda vya kuvutia sigara.
maana nasikia inaathiri wanao sikia moshi wake kuliko wanao vuta.
Unakuta mtu yuko kwenye public lakini anapuliza moshi kama treni.
Yuko nyumbani na mtoto wake anavuta tu sigara,....no wonder
watoto wa wavuta sigara akili zao shuleni zinakuwa haziko stable.
 
Bora avutishwe sigara kuliko bangi!

Mara nyingi sigara huwa ni stepping stone tu.
Aki graduate kuvuta sigara akaona haimpi raha tena ata rukia bangi tu.
Baada ya hapo Unga,etc.

Mungu amsaidie,pray for him.
 
Haha,yaani 24 kwa siku?
Duh,kuna mzee alinisimulia kaanza kuvuta akiwa sekondari.
Hadi leo ana wajukuu wako sekondari lakini bado anavuta tena sio chini
ya 3 kwa siku.

Kinacho nishangaza ni kwamba HAJAFA anapeta tu sijui mapafu yake yana hali
gani saivi,wengine ukijaribu siku mbili
tu unakohoa kama ndo unataka kutoa roho,una nuka mdomo...............

Mkuu nikwa kudra za Mungu, uvutaji wa sigara ni hatari kwa Afya!
 
kiukweli hata mimi hii tabia inaniudhi sana sio sigara peke yake hata kuwatuma watoto walete au wakanunua bia au kuingia na mtoto bar au gest mpaka usiku wa manane hii inampelekea mtoto kuingia kwenye tabia mbaya hata kumjenga vibaya kiujumla maadili yameporomoka kotekote na ndosababu kubwa ya watoto kuwa na tabia mbaya sana siku hizi
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom