Hizi Software 3 hazitokuja kupata mshindani wa kuzipindua kizazi hiki

kali linux

JF-Expert Member
May 21, 2017
1,996
5,054
Hello bosses....

Kwa mizunguko mizunguko nlopitia baada ya kufanya kazi na watu kadhaa kwenye field ya software dev nmekuja gundua (in my opinion) kuna software hizi 3 hata itokee alternative gani kizazi hiki hazitokuja kuwa replaced.

Kiufupi hizo ni:-
1) BLOOMBERG TERMINAL
2)MICROSOFT EXCEL
3)SAP BUSINESS ONE (B1)



Nitazifafanua kiufupi hapa chini

---> BLOOMBERG TERMINAL
Hii kama hujihusishi na financial markets (At Instutional Level) itakua bado hujaisikia lakini ni moja kati ya software zinazorun dunia hii. Nasema zinarun dunia coz inatumiwa na asilimia kubwa ya Financial Institutions kutrade kwenye Financial markets kuanzia kununua stocks, bonds, options, currencies na financial instruments & derivatives nyngne. Wanaohusika kwenye hii field hupenda kuiita 'BLOOMIE', ilitengenezwa na kuanza kutumika kwenye miaka ya 1980 chini ya Mike Bloomberg na kinachonifurahisha kuhusu hii software ni kwamba ime-maintain 'old-school look' ambayo naweza kuiita 'hacker-like' look. Rangi zake sana sana ni black and orange na mwonekano wake unavutia kwa wanaopenda 'less-bullshit UI'.

Gharama za kutumia hii software kwa mwaka ni USD 25,000 na mabillion ya dollar hupitia kwenye hii software kila mwaka. Toka ianze kutumika 1980s hadi sasa kuna wapinzani wengi wanatengeneza software zao lkn hawajafanikiwa kuipiku BLOOMIE.


---> MICROSOFT EXCEL.
Hii siwezi ongelea sana coz wengi tunaifahamu. Ni kati ya products za Microsoft ambazo nazikubali sana. Tumeona zinakuja spreadsheet software nyingine ila hii ipo on trend miaka nenda miaka rudi. Watu wanasema wahindi wako vzr kwenye biashara lkn deep down wengi wao wanatumia excel, hao hua ni wataalam wa excel. Nilienda kwa jamaa fln kuwapa proposal ya kutumia custom made accounting software lkn wakanionyesha excel setup zao na sikuamini nlichokiona, kuanzia accounting, stock management etc... zote walikua wanafanya kwa excel tu.

---> SAP Business One (B1)
Hii nayo ni kati ya software za zamani sana ambazo hadi leo bado zinatumika. ilitengenezwa mwanzoni kabisa mwa computer Era. Hii software iko complicated na pia ina programming language yake lkn hayo hayazuii watu kuendelea kuitumia. Kazi yake kubwa ni Kufanya Enterprise Resource Planning, software za category hii hujulikana kama ERP software. Kwenye business ndg ndg huwezi kuikuta lkn ukienda kwa Giants kama Alphabet, Meta na silicon valley companies nyingine basi utaikuta. Hata hapa Tanzania nimeona inatumika kwenye baadhi ya makampuni makubwa makubwa ya uzalishaji na usafirishaji.



Zipo nyingine baadhi kama QuickBooks, Microsoft word, etc... lkn hizo zina washindani ambao tyr wanafanya vizuri na miaka michache baadae zinaweza kupotea kama MySpace. Lakin hizo nilizotaja hapo juu zina 'Strong' foundation na 'Loyal' Customer base kiasi kwamba hata kama ni ngumu kutumia au ni nzito bado zitaendelea kuongoza kwenye nyanja zao kwa hiki kizazi


Peace......
~Kali Linux
 
Noted!
Hivi hiyo BLOOMBERG TERMINAL inatofauti gani META TRADE za wazee wa FOREX na kwanini kama BLOOMBERG TERMINAL ndio oldest isingekua common kama META TRADE
BLOOMBERG Terminal inatumiwa na larger financial institutions nikimaanisha banks, hedge funds, ETFs.

Hio ni kwa sababu BLOOMIE inakuunganisha na players wote kwenye market, pia inakupa access ya data zoote unazohitaji ili kufanya speculation zako. Ni ngumu kukuta Solo Investor anatumia bloomie

Hizo MT4 na MT5 unazosemea zinakuunganisha na brokers tu ambao wengi ni market makers. Na pia hizo wanatumia sana retail traders. Pia zinaruhusu mode fln za kutrade ambazo ni maalum kwa small to medium investors. Pia sidhan kama unaweza nunua real stock kupitia mt4 au mt5 Sanasana utaishia kununua hizo stock CFDs na sio real stock.
 
Yaani matumizi ya Excel tunayoyajua/kuyatumia kila siku Ni labda 0.5% ya uwezo wote wa MS Excel.Lile dude Ni kubwa mno,Lina makorokocho ambayo kiukweli Ni advanced kinyama.

Nilimuona jamaa mmoja mwanajeshi wa US huko YouTube akiitumia ku-calculate hesabu zake za milipuko,nikasema tu hiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii
 
Yaani matumizi ya Excel tunayoyajua/kuyatumia kila siku Ni labda 0.5% ya uwezo wote wa MS Excel.Lile dude Ni kubwa mno,Lina makorokocho ambayo kiukweli Ni advanced kinyama.

Nilimuona jamaa mmoja mwanajeshi wa US huko YouTube akiitumia ku-calculate hesabu zake za milipuko,nikasema tu hiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii
Mie nilishangaa kuona mzungu fln hv huwa nafuatilia blog yake kuhusu mambo ya genetics anaitumia, na sio tu kwa kutunza record bali kwa operations zake. Ila sema yeye alikua analalamika kwamba excel inaconvert hizi gene names kuwa date. Mfano kuna gene inaitwa SEPT2, sasa excel ikiona hvo yenyewe inadhan ulikua unataka kuandika trh so inabadili hilo neno kuwa tarh 2 SEPTEMBER.

All in all excel ni program ambayo inabidi iwekwe kwenye syllabus za mashulen, inaweza rahisisha vitu vingi sana
 
Hapo kwenye excel kuna jamaa alikuwa anahitaji software kama ya supermarket, ya billing system kwa ajili ya duka lake nikampiga kizinga cha 15 million mpaka kukamilika,Aloo kumbe akaenda kwa wahindi wenyewe wanatumia excel kama inventory system. Nikaumbuka all in all naipa heshima excel.
Ulicomplicate mkuu....
Kwa VBA ungemtolea kitu kizuri.
 
Tz nadhani Data Science /SATATISTICS tupo nyuma sana. Hata wataalum tu wa Advanced Data Analysis ni shida. Mfano. Ku master Excel, SPSS, R, nk hizi ndogo tu ni changamoto.
Changamoto sio wataalamu, changamoto ni motivation.

Hizo hata ukimaster nani atatumia Data-driven research yako humu bongo. Kwa ulizotaja hapo ambayo sijamaster ni SPSS tu. R, Excel, Tensorflow etc.... zote nmemaster na nmetumia lkn kila mtu ukimpa proposal yako anapita kushoto .Sometimes unaishia kusoma tu unabaki masikini coz haya mambo yanahitaji time na brainpower kubwa sana

Biashara na hata operations za serikali humu tz hazitumii data-driven researches. Watu wanadhan biashara kubwa kama apple au tesla zinakua kwa bahati lkn mule kuna wachawi wa analysis wanatumia data driven researches kujua wafanye nn watengeneze nn kwa wakati gani.

Issue sio kukosa wataalam, issue ni kukosekana kwa motivation na harnessing ya wataalm waliopo
 
Yaani matumizi ya Excel tunayoyajua/kuyatumia kila siku Ni labda 0.5% ya uwezo wote wa MS Excel.Lile dude Ni kubwa mno,Lina makorokocho ambayo kiukweli Ni advanced kinyama.

Nilimuona jamaa mmoja mwanajeshi wa US huko YouTube akiitumia ku-calculate hesabu zake za milipuko,nikasema tu hiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii
Hahahaaa noma sana
 
Back
Top Bottom