KIWIRA na MCHUCHUMA: A Campaign To Reclaim...

Ibrah, wazo lako ni zuri sana, wasi wasi wangu sijui hii kampeni yaweza fanyikaje? Nilisha uliza huko nyuma kwamba jamani hata hii mikataba mibovu ambayo wote tunaishuudia hata huu wa Buzwagi ambayo haijaanza ( kwa maana kwamba muwekezaji hajatumia pesa yake) hatuwezi izuia?? Jibu nililo pata lilinimaliza kabisa, kwamba hapa tumeisha saini mkataba! na hicho ndo kitanzi kinacho tumaliza! sasa na hili la kiwira, mkataba ulisha sainiwa sasa hapo ndo naona giza tupu! na kuishiwa nguvu na matumaini ya kampeini inayo weza fanyika na ikaleta nuru mpya!

Rwabugiri, ni kweli kuna utata mwingi katika hili, hata hivyo kuna maelezo fulani hivi yalipatikana kutoka kwa Bwn. Tundu Lissu, alipohojiwa na Mwanakijiji, mimi naona yana leta matumaini ya aina fulani hivi kama kusurutisha mikataba yote kunashindikana. unaweza kusikiliza kwa kubonyeza hapa. Inabidi usikilize mpaka mwisho.

SteveD.
 
Nimeandika Makala kwenye gazeti la Kulikoni la Leo yenye kichwa cha habari "Mkapa, Yona Wanyang'anywe Kiwira". Kwa wale walioko bongo makala hiyo imeanzia ukurasa wa mbele. NItawawekea hapa makala hiyo baada ya muda kidogo.
 
Nimeandika Makala kwenye gazeti la Kulikoni la Leo yenye kichwa cha habari "Mkapa, Yona Wanyang'anywe Kiwira". Kwa wale walioko bongo makala hiyo imeanzia ukurasa wa mbele. NItawawekea hapa makala hiyo baada ya muda kidogo.

Mwanakijiji tunaisubiri hiyo Makala; asubuhi nimeisikia kwenye kipindi cha kutoka Magazetini RTD. Tuwekee hapa Mwanakijiji!
 
Mwanakijiji tunaisubiri hiyo Makala; asubuhi nimeisikia kwenye kipindi cha kutoka Magazetini RTD. Tuwekee hapa Mwanakijiji!
Yaani RTD wamesoma kichwa cha habari cha gazeti linalosema "Mkapa Yona wanyang'anywe kiwira"!. Basi kweli Tanzania Demokrasia inapanuka.
 
Kuna wakati chepeo lazima iitwe chepeo na kijiko kiitwe kijiko. Kuna wakati ambapo mtu aliyechukua kitu kisichochake bila kuomba isiitwe kuazima bali iitwe wizi na kuna wakati ambapo viongozi wanapojigawia mali ya wananchi kama njugu tusiseme “wamestaafu siasa” bali tuwawajibishe hata kama hawatakikusikia. Binafsi leo nimeamua kuwatolea uvivu Rais Mstaafu Mkapa na Waziri wake wa Nishati na Madini Bw. Daniel Yona. Ndugu zetu hawa wametumia nafasi zao vibaya kujichukulia mali ya taifa hili na bila haya wala shaka wameliingiza Taifa kwenye mkataba mbovu kabisa kuliko yote iliyowahi kuingiwa na nchi yetu. Watu hawa wawili wanyang’anywe mali hiyo na irudishwe kwenye usimamizi wa Taifa hadi mwekezaji makini atakapotokea.

Kwa muda mrefu gazeti dada la “Kulikoni” limekuwa likiandika habari kuhusu jinsi viongozi hawa walipokuwa madarakani walivyoweza kutumia nafasi zao kujichukulia kampuni ya Kiwira Coal Mine na kujimegea hisa nene kwenye kampuni hiyo wao wawili na familia zao wakishikilia karibu asilimia themanini na tano ya kampuni hiyo. Hakuna mtu ambaye yuko tayari kuelezea hadharani ilikuwaje Rais wa Jamhuri ya Muungano na Waziri wake wa Madini waweze kujipatia kampuni hiyo ya makaa ya mawe. Hivi ni nani anajua hizo hisa za asilimia 85 ziliuzwa kwa kiasi gani na kina Mkapa na Yona walilipa kiasi gani na toka wapi?

Wakati Waziri Daniel Yona akiwakilisha makadirio ya mapato na matumizi ya wizara yake kwa mwaka 2004/2005, alisema hivi kuhusu machimbo ya Kiwira “juhudi za kumtafuta mbia ili aweze kuufufua mgodi huo zimekukuwa zikielekezwa kwa makampuni toka China. Hata hivyo, kwa kuwa jitihada hizo za muda mrefu hazijazaa matunda, sasa PSRC imefungua milango kwa wawekezaji wengine watakaojitokeza.”. Kauli hiyo iliyotolewa Bungeni iliashiria kuwa kuna watu “wengine” wanaoangaliwa ili waweze kuchukua jukumu la “kufufua” mgodi huo ili hatimaye uweze kuchangia katika kuzalisha nishati ya umeme nchini. Tatizo ni kuwa, wakati anazungumza Bungeni Waziri Yona alijua kabisa watu hao “wengine” ni kina nani na kwa kweli hakukuwa na juhudi zozote zile za kutafuta “mbia” au “wabwia” wengine.

Tunachofahamu kwa uhakika sasa hivi ni kuwa wakati anazungumza Bungeni kuwakilisha makadirio hayo Bw. Yona alikuwa anafahamu kuwa yeye na Rais wake walikuwa mbioni kuingia katika ubia wa kuunda kampuni ya Tanpower Resources mwishoni mwa mwaka 2004 ambayo miezi sita baadaye (mwaka mmoja baada ya hotuba ya Yona Bungeni) ikajinafasi kuchukua kampuni ya Kiwira Coal Mine.

Wakurugenzi wa kwanza wa kampuni hiyo walikuwa ni mama Anna Mkapa, Waziri Daniel Yona (Waziri aliyeshughulikia Nishati na Madini), Nicholas Mkapa (mtoto wa Mkapa), Joseph Mbuna (Baba Mkwe wa Niko), na Evans Mapundi. Katikati ya mwaka 2005 timu ya watu hawa wawili wakaingia katika ununuzi wa hisa za Kiwira Coal Mine na kuchukua asilimia 85 na kuiachia serikali (ambayo wao ndio watendaji waandamizi wa serikali hiyo kwenye Nishati) asilimia 15 tu. Kwa mtindo wa kutoa mkono huu na kuchukua kwa mkono mwingine, wakaweza kujipatia Kiwira.

Mwaka 2006 Machi, Serikali ya Rais Kikwete, ambayo ilichaguliwa kwa asilimia kubwa kuiamsha Tanzania kwa ahadi ya “kutofanya mambo yale yale” na kuanza kufanya mambo kwa “kasi mpya, ari mpya na nguvu mpya” huku ikijua “dili” hili ikaamua kuingia mkataba na kampuni ya kina Mkapa na Yona. Mkataba huo ambao kwa hela ya madafu unagharimu zaidi ya Bilioni 300 gharama yake inafanya ununuzi wa rada na mkataba wa Richmond kuwa ni mtoto! Inasikitisha kuona kuwa serikali iliyoahidi kuwa itapitia mikataba na kuhakikisha kuwa Taifa haliingii kwenye mikataba mibovu tena ndiyo imeliingiza Taifa kwenye mkataba mbovu kama wa Kiwira tena kiujanjaujanja kiasi kwamba hatukuambiwa wakati ule kuwa kampuni ya Kiwira ni ya kina Mkapa na Yona.

Kinachosikitisha zaidi ni kuwa hakuna mbunge wa CCM ambaye amekuwa na ujasiri wa kuhoji biashara hiyo na mkataba huo na kuwaachia jambo hilo wapinzani kana kwamba kuuzwa Kiwira kutawaathiri wapinzani tu. Sijui wako wapi wabunge wa Mkoa wa Mbeya ambao mgodi huu upo? Ni nani anatetea maslahi ya wananchi wa Ileje na Kyela? Leo hii tuna matatizo na Tanesco hadi Mkurugenzi wake anataka kujiuzulu kwa sababu ya mikataba mibovu ya nishati iliyosokomezwa kwenye koo la lake. Leo hii wanaundia tume suala la Richmond lakini wanakwepa hata kutamka Kiwira kwa sababu tu Rais Mstaafu anahusika. Woga huu wa uongoza, hofu hii ya kitoto, na mtazamo huu finyu wa kiuwajibikaji ndio kiini cha matatizo tuliyonayo kwenye mikataba hii ya nishati na madini.

Kuna maswali ambayo yana budi kujibiwa kuhusu suala hili zima na hatua muafaka kuchukuliwa. Swali la kwanza na la msingi ni kuwa PSRC iwaeleze Watanzania kuwa ilikuwaje kampuni ya Tanpower Resources kununua hisa za Kiwira na isiwe kampuni nyingine? Kama kulikuwa na tenda yoyote ile iliyotolewa ilitolewa lini na masharti yake yalikuwaje? Pia tunahitaji kuambiwa ilikuwaje Waziri aliyeko madarakani ajiundie kampuni na halafu kampuni hiyo hiyo ipate tenda kubwa toka serikalini? Je, hisa za Kiwira ziliuzwa kwa bei gani na kampuni ya Tanpower Resources ililipa kiasi gani na pesa zake zilitoka wapi? Kuna habari kuwa Rais Mkapa na Waziri wake walijipatia kampuni ya Kiwira bila kulipa hata senti moja na wakiitwa wezi watakataa? Iweje mtu achukue mali ya umma kinyemela huku anajikinga kwa kinga ya Urais?

Ndugu zangu kuna wakati siyo tu tuwakatalie watawala wetu bali pia tuwaoneshe kuwa hatuko tayari kuendelea kuburuzwa na kufanywa wajinga katika nchi yetu. Haiwezekani kikundi cha watu wachache kijiamulie kuwa kina uwezo wa kufanya lolote, wakati wowote, na kwa namna yoyote bila ya kuhojiwa na mtu yeyote yule. Ni lazima watanzania kupitia wawakilishi wao wawahoji kina Yona ili ukweli kuhusu Kiwira ujulikane.

Tusiendelee kuwaonea haya viongozi wanaotumia nafasi zao vibaya ambao kwa kiburi chao hawataki kuzungumzia tuhuma zinazowakabili. Kitendo cha Mkapa na Yona kujichukulia Kiwira kinyemela ni kitendo cha wizi wa mchana kweupe. Ni sawa na kitendo cha Mwenyekiti wa Kijiji kuiba kuku wa wanakijiji wenzake halafu akajitengenezea yeye mwenyewe banda kubwa ambako kuku wale wa wizi wanataga mayai ambayo atawauzia wanakijiji wale kwa bei ya juu. Hakuna kitu ambacho kinaweza kusemwa kuhusu Kiwira ambacho kinabeba mantiki.

Ni kwa sababu hiyo basi wakati umefika wa kiongozi kuonesha umakini na uthabiti wa vitendo. Wiki karibu mbili zilizopita maamuzi mawili yalifanyika. Bunge la Muungano liliamua kuunda Kamati Teule ya kuangalia mazingira yote yaliyosababisha Taifa kuingia mkataba wa Richmond, tume inayoongozwa na Dr. Harrison Mwakyembe. Wakati huo huo Rais wa Jamhuri ya Muungano aliunda Kamati yake ya kupitia mikataba mikubwa na sheria ya Madini. Maamuzi hayo ambayo yameonekana yamekuja wakati muafaka ni maamuzi ambayo yalikuwa yanasubiriwa kwa hamu na Watanzania.

Licha ya kuwa Kamati ya Rais haina nguvu kubwa kama ile ya Bunge, ni matumaini ya Watanzania wengi kuwa endapo itabadilishwa na kufanywa Tume ya Rais au itatenganishiwa majukumu basi kuna makubwa ambayo yanaweza kufanyika. Kati ya mikataba mikubwa ambayo Kamati hiyo haina budi kuipitia na mazingira yake ni mkataba huu wa Kiwira na kuangalia ilikuwaje kina Mkapa na Yona wajipatie mkataba wa mabilioni ya shilingi wakitumia ofisi zao kwa kisingizio cha “ujasiriamali”. Vinginevyo, umefika wakati wa Rais Kikwete kwa kutumia mamlaka aliyonayo Kikatiba kuingilia kati na kuwanyang’anya wajanja hawa kampuni hiyo na kuirudisha mikononi mwa PSRC ili muwekezaji mwingine au mbia mwingine ajitokeze.

Inapotokea mtu amekwapua kitu na ameanza kukitumia kama cha kwake basi hatuhalalishi na kusema tumuonee haya kwa vile tu kinapendeza mikononi mwake. Wakati mwingine inabidi kitu hicho anyang’anywe kwani amejipatia kwa njia isiyo halali au ya udanganyifu.

Rais Mkapa na Daniel Yona pamoja na familia zao na washirika wao wa Tanpower Resources wamejipatia mgodi wa Kiwira kinyemela, wametumia nafasi zao vibaya na wamewarubuni wananchi wa Taifa hili na wakati umefika walipe kwa makosa hayo. Katika Taifa letu na ijulikane sasa na milele kuwa hakuna mtu aliye juu ya mwingine hata kama ana bendera mia zina pepea; ni lazima watambua kuwa hakuna kiongozi ambaye yuko juu ya sheria hata kama anajisikia hivyo; na ya kuwa hakuna Mtanzania mwingine ambaye kutokana na nafasi yake anaamini kuwa anastahili au ana haki zaidi ya Mtanzania mwingine kwa sababu tu ana nafasi fulani! Tunawakatilia watawala wetu uwezo huo, tunawakatilia watawala wetu haki hiyo, na ndiyo! tunawakatalia watawala wetu nafasi hiyo. Kiwira irudishwe kwa wananchi, Mkapa na Yona wanyang’anywe ili liwe fundisho kwa viongozi wengine walafi na wenye uroho wa mali ya umma na wanaotumia madaraka yao vibaya. Kufa kwa Nyerere kisiwe kisingizio cha watu wachache kujifanya miungu watu!

Muwanyang’anye sasa ama sivyo watanyang’anywa siku moja wakiwa na pingu kizimbani. Ni lazima turudishe nidhamu ya utumishi wa umma kwani kuendelea kuwafumbia macho watawala kama kina Mkapa na Yona ni kukaribisha uporaji wa mali ya umma na ni kuwapa kibali cha ufisadi. Hata kama hawataki kusema sasa na wakae kimya lakini Kiwira itolewe midomoni mwao kama tonge la ugali kabla hawajaanza kutafuna na kumeza fedha za wananchi. Ama zao ama zetu, Mkapa na Yona rudisheni mali zetu. Vinginevyo, mtanyang’anywa na kuachwa na roho zenye kutu. Na viongozi wanaoogopa kuwachukulia hatua watu hawa na wenyewe watambue siku moja na wao watanyang’anywa madaraka hayo na waliowalinda na wenyewe watalipa uzembe huo wa kiuongozi.
 
MKJJ umeongelea vizuri sana wajibu wa bunge, lakini umesahau wajibu wa vyama vya upinzani, mashirika ya hiari (TGNP), wasomi wetu (kina Shivji na Tundu Lissu) na mashirika ya dini. Wanawajibika wote hawa kuhakikisha kiwira inarudishwa mikononi mwa wenye mali. Anyway, siku ya Mkapa inakuja, tena iko karibu!
 
Tena napendekeza wapewe halimashauri usika ilikuchochea maendeleo ktk jamii,na sio wao wapewe laki mbili kila mwezi .
 
Wakuu wote JF, ninaomba kuwafahamisha kuwa ninajaribu kukusanya habari zote kuhusiana na hii ishu ya Kiwira Coal Mine, nimeombwa hivyo na baadhi ya wabunge na viongozi wa serikali yetu, ambao wana uchungu sana na taifa letu, kwa hiyo ninajaribu ku-print all the posts, na kuzipitia tena na kuandika ripoti maalum toka JF,

Viongozi walioniomba, wanasema kuwa ndio hasa azimio lao next year kisiasa, kutaka mgodi urudishwe kwa taifa, kwa mwenye habari zozote muhimu kushusiana na hii ishu please, ziweke hapa au nitumie kwenye mtuwameli@yahoo.com.

Ahsante Wakuu, pole pole tutafika!
 
Labda naota, but mkuu FME Mungu akutangulie na hakika ufanikiwe!

Mkuu, I did this na Richmond deal nilikusanya info na wananchi hapa walinitumia in private, nafikiri unajua kuwa Richmond is live and going very well na majibu yanakuja,

Kwa hiyo ninaamini this one too is coming, na viongozi walioniomba hizi info ninawaamini sana na maneno walioniambia kuwa uwezekano mkubwa wa kuurudisha huu mgodi.

Ahsante Mkuu.
 
Mining sector under the microscope: Review team to visit Kiwira coal mine

-Set to delve further into Mkapa-Yona connection

THISDAY REPORTER
Dar es Salaam


THE presidential-appointed mining sector review committee is next month scheduled to visit the Kiwira coal mine in Mbeya Region, which was owned by the state until its 2005 sale in dubious circumstances to a private company set up by former president Benjamin Mkapa and senior cabinet minister Daniel Yona while both were still in public office.

Well-placed sources have told THISDAY that members of the committee, chaired by Judge Mark Bomani, will make a site visit to the mine whose new owners have since entered into a $271.8m (approx. 326bn/-) contract with the Tanzania Electric Supply Company (TANESCO) for the generation of up to 200 megawatts of coal-fired electricity.

The sources said the Bomani committee was set to turn its attention over to the Kiwira coal mine issue after concluding its ongoing review of major gold mining contracts in the country.

Since the signing of the agreement between TANESCO and the Kiwira Coal and Power Limited company last year, production deadlines for the project are reported to have spiralled out of control, forcing a revision of the original schedule. Government officials say under the revised production schedule, Phase One of the project is now expected to come online by April 2009 with the generation of 50MW of coal-fired electricity to be connected to the national power grid.

The second and final phase is to begin in October 2009 with the generation of another 150MW of electricity from the Kiwira mine, bringing the total output to 200MW.

When asked exactly when his team intended to visit the Kiwira mine, Judge Bomani would neither deny nor confirm the reports, but said the committee was scheduled to resume its work early next month after the year-end holidays.

’’The committee will be back at work on January 2 and we will then embark on site visits to the gold mines. Afterwards, we will proceed to Manyara and Arusha Regions to visit gemstone-producing areas, and finally we will conduct visits to the southern parts of the country,’’ he said.

The Kiwira coal mine is located in Rungwe District, Mbeya Region, which forms part of the country’s southern highlands zone.

While Judge Bomani remained noncommittal regarding the planned visit to the Kiwira coal mine, sources familiar with the mining sector review committee’s working schedule have reconfirmed to THISDAY that the trip is indeed on.

It is also understood that before winding up its work, the committee will also review the controversial privatisation process underwent by the Kiwira coal mine, and how it eventually ended up being bought by a private company formed by Mkapa, Yona and members of their immediate families.

Committee members are also likely to look into the circumstances that led to the current owner of the Kiwira mine project also acquiring the nearby Kabulo coal prospect, also in Mbeya Region, which was reportedly wrestled from the control of the State Mining Corporation (STAMICO) - a government agency.

Previous government-commissioned studies have shown that the Kabulo area, which lies within the East African Rift Valley system, has proven reserves of up to 14 million tonnes of coal. While still in control, STAMICO had been actively promoting the area with the intention of attracting a strategic investor to develop a coal-fired power station.

It has been well-established through THISDAY investigations that at least 85 per cent of shares in Kiwira Coal and Power Ltd are owned by Tanpower Resources Limited, a little-known private company formed in 2004 by Mkapa (then still president) and Yona (then the minister responsible for both energy and minerals). The Tanzanian government currently retains the remaining, token 15 per cent shares.



Source: Thisday
 
'Katika uchunguzi wetu kuhusu umuliki wa Kiwira Coal Mining, tumegundua hakukuwa na zabuni yoyote iliyotangazwa kuhusu uuzwaji wa KCM. Pia hatujui bei ya kuuzwa KCM kwa wamiliki wake ilipangwa na nani na ilifikiwaje na kwa maoni yetu bei hiyo ni ndogo sana ukilinganisha na tani za mkaa wa mawe uliopo katika mgodi huo wa Kiwira.

Kuhusu mkataba kati ya KCM wa shilingi bilioni 327 hakukuwa na mjadala wowote kati ya viongozi wa TANESCO na KCM kuhusiana na mkataba huo. Tuliomba nyaraka za majadiliano kati ya KCM na TANESCO toka makampuni yote mawili lakini wote hawakuweza kutupatia nyaraka za majadiliano ya mkataba huo.

Kwa maoni yetu KCM irudishwe katika umiliki wa serikali na mkataba kati ya TANESCO na KCM uwe batili.'

Yakiwemo haya niliyoyaandika hapo juu katika hiyo ripoti ya kamati hii itakuwa ni furaha iliyoje kwa Watanzania wote wapenda haki nje na ndani ya Tanzania.
 
Dr Slaa on Kiwira mine takeover saga: ’Mkapa should be held accountable’

JUMBE ISMAILLY, PST
Singida
THIS DAY


FIREBRAND opposition legislator Dr Wilbrod Slaa yesterday challenged President Jakaya Kikwete to hold his predecessor, Benjamin Mkapa, accountable for ’illegally’ acquiring the Kiwira coal mine in Mbeya Region.

Dr Slaa, the Member of Parliament for Karatu Constituency and also Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) secretary general, told a public rally in Singida that Mkapa’s move to privately acquire the Kiwira mine while still in power was a violation of the national Constitution.

He said it was therefore important that President Kikwete take appropriate disciplinary measures against both the ex-president and his apparent associate in the Kiwira mine takeover, former energy and minerals minister Daniel Yona.

The two are understood to have jointly registered a private company called Tanpower Resources Company Limited, with various close relatives including wives, children and in-laws in tandem, in 2004 and the same company then went on to acquire 85 per cent of shares in the Kiwira mine after its privatization.

It has also been established that during both the Tanpower Resources establishment and Kiwira coal mine privatization processes, Mkapa and Yona were still serving as president and minister for energy and minerals, respectively.

With Tanpower Resources at the helm, the reinstituted Kiwira Cioal and Power Limited company has now entered into an agreement with the still state-owned Tanzania Electric Supply Company (TANESCO) for development of a $271.8m (approx. 326bn/-) project to produce up to 200MW of coal-fired electricity for the national grid.

’’CHADEMA will continue to put pressure on President Kikwete to take action against former president Mkapa, for breaching the Constitution of the United Republic of Tanzania in the way he acquired the Kiwira mine and then secured the TANESCO contract,’’ Dr Slaa told the rally here.

The firebrand opposition politician, who has been in the forefront in condemning high-level corruption in both the Mkapa and Kikwete governments, said former finance minister Basil Mramba should also be held accountable for alleged ministerial misdoings.

According to Dr Slaa, it was Mramba who awarded a hugely expensive gold mining audit contract to the international firm Alex Stewart Assayers, which then proceeded to take 1.9 per cent of the 3 per cent royalty which the country gets from gold mining companies.

The CHADEMA secretary general also accused Mramba of playing a lead role, while still finance minister, in the latest 133bn/- Bank of Tanzania (BoT) looting scandal uncovered by a special audit.

’’This is the right time for President Kikwete to exercise his constitutional powers and sack Basil Mramba from his ministerial position,’’ Dr Slaa stressed. Mramba currently serves as Minister for Trade, Industry and Marketing.

Meanwhile, according to Dr Slaa, the disgraced former BoT governor Daudi Ballali has already left the United States and sought refuge in Malta.

He said Ballali departed from the States aboard a private jet on Wednesday last week.

The CHADEMA secretary general was in Singida to prop up support for his party and mobilize people to reject the ruling CCM government for allegedly plundering the economy and making the lives of ordinary people more and more difficult.

 
Dk. Slaa sasa amgeukia Mkapa

na Jumbe Ismailly, Singida
Tanzania Daima


KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willbrod Slaa, ameapa kuendelea kulivalia njuga suala la umiliki wa kampuni ya kufua umeme inayomilikiwa na Rais mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa.

Dk. Slaa alisema kitendo cha rais mstafu huyo kumiliki kampuni ya kibiashara ni ukiukwaji wa katiba ya nchi, hivyo alisisitiza suala la kumwajibisha halina budi kupewa kipaumbele na Rais Jakaya Kikwete.

“CHADEMA itaendelea kumshinikiza Rais Kikwete ili amwajibishe Rais mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa, kutokana na kuvunja katiba kwa kuwa mmoja wa wamiliki wa Kampuni ya Kiwira inayozalisha nishati ya umeme unaotumia makaa ya mawe na kuliuzia Shirika la Ugavi wa Umeme nchini, yaani Tanesco,” alisisitiza.

Dk. Slaa alieleza hayo wakati akizungumza na wananchi wa Halmashauri ya Manispaa ya Singida, waliofurika kwenye mkutano wake wa hadhara, uliofanyika kwenye viwanja vya Shule ya Msingi ya Ipembe, mjini Singida.

Aidha, Dk. Slaa alielekeza lawama zake pia kwa aliyekuwa Waziri wa Fedha katika Serikali ya Awamu ya Tatu, Basil Mramba, na kumtaka Rais Kikwete amwajibishe na yeye pia kwa kile alichodai kuwa alikuwa akipokea kila mwezi hongo kutoka moja ya kampuni kubwa inayohusiana na madini.

“Ni wakati muafaka hivi sasa kwa Rais Kikwete kutumia mamlaka aliyonayo ili aweze kumwajibisha Mramba kwa kumwondoa kwenye kikosi chake,” alisema huku akishangiliwa na wananchi waliofurika kumsikiliza.

Dk. Slaa alisema kuwa ziara yake hiyo ni sehemu ya mikakati yake ya kuendelea kufichua maovu yanayofanywa au yaliyowahi kufanywa na viongozi waliopo madarakani na wale waliostaafu.

Kwa upande mwingine, alisisitiza madai yake kuwa aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu, Daudi Ballali, amefichwa ili asitoe siri anazozifahamu kuhusu ubadhirifu uliofanywa katika taasisi hiyo nyeti nchini.

Alidai kuwa Ballali amefichwa na viongozi wa serikali ili asitoe siri kwa sababu viongozi hao wana hofu kuwa iwapo Ballali atayasema hadharani yale anayoyafahamu kuhusiana na ubadhirifu ndani ya BoT, hata wao (viongozi) hawatakuwa salama.
 
...nchi imeibiwa balaa,rushwa kubwa kubwa lakini mafisadi bado wapo wanapeta tuu,angalia kina Mramba na wengine kina Mgonja ndio wanaongezewa vyeo kama hakuna kilichotokea,nimeamini JK hakuna anachosaidia zaidi ya kuongeza ufisadi tuu,nchi inategemea 40% ya budget lakini zinazoibiwa ni zaidi ya hizo,dawa ni kuwapiga chini tuu hawa mafisadi uchaguzi ujao maana hata tukianza prosecution haitasaidia na yatakimbia yote kama hilo lingine lililokimbia na private jet kwa pesa zetu
 
Slaa Mungu akupe maisha marefu uenelee kuitetea Tanzania tajiri lakini inamilikiwa na watu wachache na wake na watoto wao na marafiki zao .Mimi nasema saga la BTO JK has failed before hakujakucha . Hana lolote na Kiwira ndiyo hatagusa kabisaaaaaaaaaaaaaa
 
’’..Put pressure on President Kikwete to take action against former president Mkapa, for breaching the Constitution of the United Republic of Tanzania in the way he acquired the Kiwira mine and then secured the TANESCO contract,’’

Hili halina mjadala. Waliondoa "MIIKO YA UONGOZI" ili kupata fursa ya kufanya walichokifanya, UFISADI USIOPIMIKA. Hata kama miiko ilikuwa imepitwa na wakiti...Lakini Matunda yake ndiyo hayo!!! Na wakati uliopita ni upi? utu na maadili ya kibinadamu hayapitwi na muda.

1. Kikwete ahakikishe viongozi waliotumia uongozi wao kama "dili" mara moja wanarudisha mali ya taifa, bila kubabaishana.

2. Wafikishwe kwenye vyombo vya sheria.

3. Katiba ya Tznia maramoja irudishe "mbadala" ya MIIKO YA UONGOZI Iliyoondolewa kifisadi kwenye azimio la arusha kwa azimio la zanzibar.Hiyo iliakuacha Uhuru wa viogozi kufanya mchezo wa kifisadi kwa mali ya taifa. "Mbadala" wa miiko ni lazima, Ili pasitokee nafasi ya kuji uma uma ; na kujifanya cha kufanya hakiko wazi. Kilichompooza Mkapa ..Ni kulegezwa kwa Miiko ya Uongozi,akatake it ease.. akajikubalisha akilini ..kwamba naweza kujifanyia alichofanya now they have to pay the price...wako wengi!!!!
 
Back
Top Bottom