nderingosha
JF-Expert Member
- Mar 20, 2011
- 4,281
- 3,243
I'm not disputing that. Nyinyi mliomchagua JK wachumia tumbo na wasiojielewa
..siku hizi ikulu imekua kitengo cha damage control propaganda....kwasababu ya blunder ya ------....hakika nitawalaumu hadi siku ya mwisho ile NEC na CC iliyopitisha jina la huyu mswahili kugombea urais 2005...maana nchi hii imekua stagnant kwa karibia miaka 9 sasa...
...Hivi nani humu anaweza kusema kwa mda huu i sera gani alikuja nayo na kuisimamia vema mkwerekiasi cha TZ kufaidi?..sera ipi??hamna ...nchi imekua inaendeshwa kizimamotozimamoto tu....na sasa jamaa anataka kumalizia mda wake kwa mbwembwe za kutuangamiza....inauma...
....Kwa kulinganisha tu watawala wetu waliopita...Nyerere alituletea ujamaa na kujitegemea na tukauona....Mwinyi akaja na biashara huria (free markets)..ama "ruksa"....Mkapa akaja na ubinafsishwaji (privatization)...pamoja na mapungufu yake...Je yeye JK kaja na nini cha kukumbukwa akiondoka???...kama si maneno na blah blah tu zisizo na mwisho...na kututia hasara zaidi ka kutuongezea deni la taifa ambalo yeye na family yake wala hawatahusika kulilipa...
...Ile NEC na CC ya ccm iliacha jina la mtu kama Dr.Salim ..mtu makini mwenye maono(vision)na asiye na njaa....tena ni mwenyekiti wa kamati ya Dr.Mo Ibrahim inayochagua viongozi bora Africa (kipimo tosha cha umakini na uadilifu)....Wakamwacha huyu wakatuletea mtu mwenye njaa...msanii....kaifanya ikulu yetu kijiwe cha kuwanufaisha washkaji na family yake...
...Nchi ya TZ imejaa utajiri lakini imegeuzwa ombaomba wa dunia ...sababu tu ya kuendekeza njaa kwa watawala...Inasikitisha sana mtu anaona ujiko kupanda ndege kwa kodi za walala hoi wa TZ kila kukicha kwenda kuhemea vibaba nje ya nchi....wakati madini na pembe zetu zinapakiwa kila kukicha kupelekwa nje ya nchi....hii hali kama si jana kuu kwa nchi hii ni nini??....alfu eti kuna genge la wezi wa ccm waliokuwa kwenye mtandao wake wa urais bado wanaonyesha nia ya kutaka kuja kututawala tena????...ili waendeleze majanga haya!!!....no way...we need to veto them .....TZ needs a role model president..and not a mere beggar....
......Aniambie mtu humu ndani ni ipi sera alikuja nayo JK na akaisimamia vema na hata akiondoka akumbukwe nayo!!...hamna kitu kwa kifupi...zaidi ya sera ya safari za nje....hata issue ya katiba mpya wameleta wapinzani anaowaita maadui wa ccm...amka TZ!!!!!
....Neno la faraja kwa wapinzani wenye mapenzi mema na nchi....Dunia hutawaliwa na principle moja muhimu kuwa..."mla huliwa".....ama..."ukidhulumu nawe utadhulumiwa"(hata kama si leo)...hivyo wakati JK anatangaza kuwashughulikia wapinzani kwa kutumia nafasi yake kama rais ..nae ajue kuwa anawindwa kushughulikiwa na watu kama kina Kagame....hata kama atakuwa amemaliza mda wake wa urais....Wakati JK anatangaza uadui na wanasiasa wa upinzani ndani ya TZ...nae ajue ana maadui nje ya nchi....tena wanaotokana na mdomo wake mwenyewe...Huu ni uhalisia ambao unatakiwa uwape faraja wapinzani wanaotishiwa na JK ndani ya TZ....yeye anaweza kuonekana shujaa kwa watu kama NEC ya ccm wanaofaidi matunda ya utawala wake.....lakini ajue nae anaweza kuonekana adui mkubwa kwa wengine (kama kina Kagame).....tafakari.....
....