KITUO cha Taarifa kwa Wananchi (TCIB) kimemshitaki Rais Jakaya Kikwete The HAGUE

Kibamba hapa amekurupuka. Huwezi kukimbilia kwenye jumuiya ya kimataifa kabla hata hujatafuta suluhu ya ndani ikiwa ni pamoja na kutaka ufafanuzi wa kauli au kumtaka aliyetoa kauli aifute. Sasa kila jambo tukikimbilia kwenye jumuiya kimataifa bila kujiridhisha kwamba ni juu ya uwezo wetu si watatuona walalamikaji na kutuchoka mapema? Tanzania hatujafikia mahali pa kuhitaji msaada wa kimataifa kwa matatizo yetu ya ndani.

Hembu jaribu wewe kufafanua kauli ya muheshimiwa halafu utuambie ina utata gani unless huangalii TV wala hufuatiliagi taarifa ya habari
 
KITUO cha Taarifa kwa Wananchi (TCIB) kimemshitaki Rais Jakaya Kikwete kwenye Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu dhidi ya binadamu (ICC), mjini The Hague, Uholanzi kwa madai ya kutoa kauli zenye kuhamasisha uvunjifu wa amani nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari jana katika ofisi za kituo hicho zilizopo Mwenge jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa TCIB, Deus Kibamba, alisema kauli ya Rais Kikwete kuwataka wafuasi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) waamke na kujibu mapigo wanaposhambuliwa, ni uchochezi.

Alisema tayari ametoa taarifa kwa Mwendesha Mashitaka Mkuu wa ICC, Fatou Bensuda, kumwomba atume timu yake nchini ili ifanye uchunguzi wa awali juu ya matamshi ya viongozi wakuu nchini.

source: Tanzania Daima

buruza mahakamani muuaji mkubwa uyu.
 
ivi kikwete anajua maana ya unyonge kweli? nimefurai atleast sasa wakuu wa the hague wameshazijua kauli za pinda na kikwete wake

ngoja kna siku nasi tutachekelea wadhalimu wakipelekwa the hague, fatou si mnafiki na tutakuwa tayari kutoa ushahidi
 
kama sio taasisi ya cdm mbona hawakumpeleka slaa the hague 2010 aliposema tz haitakalika

hicho kituo ndio leo nakisikia, kimeshatoa taarifa gani kwa wananchi?hawa wasomi wa moshi ni janga la taifa
 
Niliwahi kuuliza katika kikao kimoja ni jinsi gani naweza kufungua mashitaka juu ya kauli na matendo kama haya. Majibu niliyopewa nilijiuliza kwa nini wanasiasa wetu hawshitakiwi maana unaruhusiwa kufungua shitaka la uchunguzi kama kauli ya kiongozi imesababisha madhara. Sioni bwana mkubwa akipona!

kuanzia mwenyekiti wake hadi chama hicjo vyote vita kufa mwisho wakupost..
 
KITUO cha Taarifa kwa Wananchi (TCIB) kimemshitaki Rais Jakaya Kikwete kwenye Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu dhidi ya binadamu (ICC), mjini The Hague, Uholanzi kwa madai ya kutoa kauli zenye kuhamasisha uvunjifu wa amani nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari jana katika ofisi za kituo hicho zilizopo Mwenge jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa TCIB, Deus Kibamba, alisema kauli ya Rais Kikwete kuwataka wafuasi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) waamke na kujibu mapigo wanaposhambuliwa, ni uchochezi.

Alisema tayari ametoa taarifa kwa Mwendesha Mashitaka Mkuu wa ICC, Fatou Bensuda, kumwomba atume timu yake nchini ili ifanye uchunguzi wa awali juu ya matamshi ya viongozi wakuu nchini.

source: Tanzania Daima

aanze kumshtaki mbowe kwa kujimilikisha gazeti la tanzania daima kinyume cha taratibu, mbowe amewadhulumu chadema gazeti la tanzania daima, hili gazeti lilikuwa la chadema, mbowe akajimilikisha .
 
Safari hii hawajaomba ndege ya Rais isafirishe ujumbe wa TCIB kwenda huko The Hague? Manake nakumbuka walishawahi kupanga maandamano na wakaomba wasindikizwe na Brass Band ya Jeshi la Polisi!

mkuu hiki kituo kimesajiliwa kweli? hizi ndio NGO feki zinazowatapeli wafadhili wa nje . hawa ndio wanachafua jina la tanzania. kikwete futa kabisa usajili wa hawa matapeli
 
KITUO cha Taarifa kwa Wananchi (TCIB) kimemshitaki Rais Jakaya Kikwete kwenye Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu dhidi ya binadamu (ICC), mjini The Hague, Uholanzi kwa madai ya kutoa kauli zenye kuhamasisha uvunjifu wa amani nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari jana katika ofisi za kituo hicho zilizopo Mwenge jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa TCIB, Deus Kibamba, alisema kauli ya Rais Kikwete kuwataka wafuasi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) waamke na kujibu mapigo wanaposhambuliwa, ni uchochezi.

Alisema tayari ametoa taarifa kwa Mwendesha Mashitaka Mkuu wa ICC, Fatou Bensuda, kumwomba atume timu yake nchini ili
ifanye uchunguzi wa awali juu ya matamshi ya viongozi wakuu nchini.

source: Tanzania Daima

Hii mahakama siiami tena...toka waliposhindwa kumtia hatiani G.Bush Jr. na Blair wa U.k...kwa uhalifu wakivita huko Iraq...

Rais aliwekwa madarakani na watanzania waliowengi....ni watanzania hao hao ndiyo wanapaswa kumuwajibisha Rais...Binafsi siamini kutatuliwa matatizo yetu ya ndani na nchi ama mashirika ya nje...anachokifanya Kibamba ni sawa na kutembeza bakuli la kuomba msaada nje ya nchi wakati tuna rasilimali nyingi za kupata hizo hela/misaada tunayoomba nje.
 
Mi ndio maana siku hizi naangaliaga positively masuala ya mapinduzi ya kijeshi...
Raisi anapokuwa this much insane kunakuwa hakuna option...
 
ICC itachukua hatua endapo JK ni adui wa wazungu,ila kama ni kibaraka mwaminifu kwao....tusitegemee kuona action. ICC ni kwa ajili ya wazalendo wa Afrika
 
kwa kawaida mashabiki wa mtoa kauli za kichochezi kama hii ya jk ndo huwa wa kwanza kuathiriwa na madhara yatokanayo na kauli husika.
Wale wote wanaocheka na kushangilia kwa sbb ya kauli hii ovu dhidi ya haki za binadamu ya mh.rais,ndio watakuwa wa kwanza kulia kwa uchungu na kusaga meno baada ya madhara kuanza nao wenyewe,ndugu zao,jamaa zao na/au watu wao.
 
Kibamba hapa amekurupuka. Huwezi kukimbilia kwenye jumuiya ya kimataifa kabla hata hujatafuta suluhu ya ndani ikiwa ni pamoja na kutaka ufafanuzi wa kauli au kumtaka aliyetoa kauli aifute. Sasa kila jambo tukikimbilia kwenye jumuiya kimataifa bila kujiridhisha kwamba ni juu ya uwezo wetu si watatuona walalamikaji na kutuchoka mapema? Tanzania hatujafikia mahali pa kuhitaji msaada wa kimataifa kwa matatizo yetu ya ndani.

Mkuu nakwambia Kibamba yuko sahihi kabisa.
Tungelalamika wapi? Wakati mahakama zimeingiliwa na mafisadi?
TCIB Hongereni sana kwa maamuzi mazuri kwa Taifa letu! Huyu rais janga kweli kweli kwa Taifa letu!
 
Kweli hapa JF kuna watu wavivu wa kufikiria na kuchambua mambo.

Kosa la Mh Raisi ni lipi?, jamani tuwe wakweli kauli aliyoitoa Mh Raisi si kauli ya kichochezi hata kidogo bali alikuwa anawahimiza wana CCM kuwa imara katika kukiimarisha chama.

Kuna mambo mengi yanafanywa na wapinzani katika kujiimarisha huku CCM ikiwa kimya kama haipo. Tumeshuhudia M4C Daima ilivyofanywa na CDM kwa lengo la kujiimarisha.

Kauli ya Mh Raisi ilikuwa inalenga kuwahamasisha wana CCM kufanya mambo ya kukipa uhai chama si zaidi ya hapo.

Naomba tusiwe bias katika hili, bali tuwe wakweli na wenye kuchambua mambo kabla ya kukurupuka.
 
Kibamba hapa amekurupuka. Huwezi kukimbilia kwenye jumuiya ya kimataifa kabla hata hujatafuta suluhu ya ndani ikiwa ni pamoja na kutaka ufafanuzi wa kauli au kumtaka aliyetoa kauli aifute. Sasa kila jambo tukikimbilia kwenye jumuiya kimataifa bila kujiridhisha kwamba ni juu ya uwezo wetu si watatuona walalamikaji na kutuchoka mapema? Tanzania hatujafikia mahali pa kuhitaji msaada wa kimataifa kwa matatizo yetu ya ndani.

Kam Sheria za Kimataifa zinaruhusu kufanya hivyo kwanini wasifanye, halafu pia hakuna utashi wa humu ndani uwe wa kikatiba au wa kisheria wa kumburuta rais aliyeko madarakani kotini.
 
Back
Top Bottom