Kikwete amuwakilisha Rais Samia katika hafla ya Mazishi ya Kitaifa ya Rais wa Zamani wa Finland, Hayati Martti Ahtisaari, Novemba 10, 2023

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,989
Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete amemwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan katika hafla ya Mazishi ya Kitaifa ya Rais wa Zamani wa Finland, Hayati Martti Ahtisaari iliyofanyika Helsinki tarehe 10 Novemba 2023.

Wakati wa kutoa salamu za pole, Rais Kikwete alisema kuwa Rais Samia anatoa salamu za rambirambi kwa Rais wa Findland, Sauli Niinistö, Familia ya Marehemu na watu wote wa Finland kufuatia kifo cha kiongozi huyo mkubwa duniani.

Rais Kikwete aliungana na viongozi mbalimbali walioshiriki mazishi hayo wakimwemo Rais wa Kosovo, Vyosa Osmani na Rais wa Namibia, Mhe. Hage Geingob na kummwagia sifa Hayati Martti Ahtisaari kwamba alikuwa kiongozi mwenye maono na mpenda amani duniani.

Hayati Martti Ahtisaari aliwahi kuwa Balozi wa Finland nchini Tanzania kuanzia mwaka 1973 hadi 1976 na alikuwa Rais wa Finland kuanzia mwaka 1994 hadi 2000. Katika vipndi vyote hivyo, Hayati Martti Ahtisaari aliimarisha uhusiano wa Tanzania na Finland katika nyanja mbalimbali ikiwa ni pamoja na kufanya ziara ya kitaifa nchini Tanzania mwaka 1997 wakati wa Serikali ya Awamu ya Tatu iliyokuwa inaongozwa na Hayati Benjamin Mkapa.

PHOTO-2023-11-11-14-48-39.jpg

Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete (kulia) akiwa na viongozi na waombolezaji wengine katika hafla ya mazishi ya kitaifa ya Rais wa Zamani wa Finland, Hayati Martti Ahtisaari iliyofanyika Helsinki tarehe 10 Novemba 2023. Rais Kikwete alimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan katika mazishi hayo.

PHOTO-2023-11-11-14-48-42.jpg
PHOTO-2023-11-11-14-48-40.jpg
PHOTO-2023-11-11-14-48-41 2.jpg
PHOTO-2023-11-11-14-48-41.jpg

Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Kikwete akimpa pole Mjane wa Rais wa Zamani wa Finland, Hayati Martti Ahtisaari.

PHOTO-2023-11-11-14-48-41 3.jpg

Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Kikwete amemwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika hafla ya Mazishi ya Kitaifa ya Rais wa Zamani wa Finland, Hayati Martti Ahtisaari iliyofanyika Helsinki tarehe 10 Novemba 2023.

Wakati wa kutoa salamu za pole, Rais Kikwete alisema kuwa Rais Samia anatoa salamu za rambirambi kwa Rais wa Findland, Mhe. Sauli Niinistö, Familia ya Marehemu na watu wote wa Finland kufuatia kifo cha kiongozi huyo mkubwa duniani.

Rais Kikwete aliungana na viongozi mbalimbali walioshiriki mazishi hayo wakimwemo Rais wa Kosovo, Mhe. Vyosa Osmani na Rais wa Namibia, Mhe. Hage Geingob na kummwagia sifa Hayati Martti Ahtisaari kwamba alikuwa kiongozi mwenye maono na mpenda amani duniani.

Hayati Martti Ahtisaari aliwahi kuwa Balozi wa Finland nchini Tanzania kuanzia mwaka 1973 hadi 1976 na alikuwa Rais wa Finland kuanzia mwaka 1994 hadi 2000. Katika vipndi vyote hivyo, Hayati Martti Ahtisaari aliimarisha uhusiano wa Tanzania na Finland katika nyanja mbalimbali ikiwa ni pamoja na kufanya ziara ya kitaifa nchini Tanzania mwaka 1997 wakati wa Serikali ya Awamu ya Tatu iliyokuwa inaongozwa na Hayati Benjamin Mkapa.
Bila picha ni uzushi
 
View attachment 2810549View attachment 2810550View attachment 2810551View attachment 2810552View attachment 2810553View attachment 2810554
Mstaafu maarufu nchini Tanzania.
 
Back
Top Bottom