Dkt. Slaa aachiwa kwa Dhamana kituo cha Polisi Oysterbay

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,034
Mwanasiasa mkongwe nchini Tanzania Dkt. Wilbroad Slaa ameachiwa kwa dhamana saa chache zilizopita ikiwa ni siku chache baada ya kukamatwa akituhumiwa kwa makosa yaliyoelezwa kuwa ni uhaini na uchochezi.

Taarifa za kuachiliwa kwa Dkt. Slaa zimekuja ndani ya saa 24 baada ya jopo la Mawakili wanaomtetea yeye na wenzake watatu kufungua kesi dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mkuu wa Jeshi la Polisi, Mwendesha Mashtaka Mkuu, Mkuu wa Polisi Mkoa wa Mbeya na Mkuu wa Polisi Kituo Kikuu cha Mbeya Mjini kwa kuendelea kuwashikilia wateja wao kinyume na taratibu za kisheria.

Pia soma
- Dkt. Slaa arudishwa kituo cha Polisi Oysterbay kutoka Mbeya. Wakili wake aambiwa akashughulikie dhamana

 
Back
Top Bottom