KITUO cha Taarifa kwa Wananchi (TCIB) kimemshitaki Rais Jakaya Kikwete The HAGUE

Haya yote ya wabara kuchukiana na kutekana hayakuwepo kabla ya utawala wa Mbowe,Slaa na Lema. Tutafakari.
 
KITUO cha Taarifa kwa Wananchi (TCIB) kimemshitaki Rais Jakaya Kikwete kwenye Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu dhidi ya binadamu (ICC), mjini The Hague, Uholanzi kwa madai ya kutoa kauli zenye kuhamasisha uvunjifu wa amani nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari jana katika ofisi za kituo hicho zilizopo Mwenge jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa TCIB, Deus Kibamba, alisema kauli ya Rais Kikwete kuwataka wafuasi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) waamke na kujibu mapigo wanaposhambuliwa, ni uchochezi.

Alisema tayari ametoa taarifa kwa Mwendesha Mashitaka Mkuu wa ICC, Fatou Bensuda, kumwomba atume timu yake nchini ili ifanye uchunguzi wa awali juu ya matamshi ya viongozi wakuu nchini.


source: Tanzania Daima



Kwa katiba hii hii ya maccm ambayo rais ni kama mfalme sioni wapi pa kumshika huyu.
 
Huyu jamaa anahang'over zake kumkichwa anadhani anaweza kujipatia umaarufu kwa kumshtaki Rais kumbe jamii ndio inamuona kituko mtupu.

Kituko ni wewe mkuu ambaye huna hata fikra za athari ya kauli ya Rais. Yeye akiwa amiri jeshi mkuu kila anachotamka ni agizo. Mimi nilikuwa nampenda sana Mh JK lakini kwa hili ameteleza sana kama si kuanguka.
 
Ubaya upo sana maana wewe hauwezi waambia watoto wako eti mwenzako akikupiga na wewe mpige woote ni watoto wako. Hii ndio inaleta ubaguzi Kikwete ni Rais wa wote bila kuangalia itikadi ya vyama. Kikwete akiharibu madhara sio kwa ccm tu bali na kwa chadema na cuf n watanzania wote.

Leo hi amekuwa Rais wa wote ! wale walioupinga urais wake na wakatoka bungeni lini walilkili hadharani kwamba wamekubwali kuwa yeye ni rais? .Any way ni kweli lakini mbona hamjadili kauli iliyowahi pia kutolewa na mtoto mkubwa kwamba inchi hitotawalika? au hi kauli ni y kawaida tu?
 
Kampeini za Uchaguzi ulioiingiza serikali ya awamu ya tatu madarakani zilikuwa na mdahalo pale Kilimanjaro Hotel na Watanzania walijifunza mengi ikiwa ni pamoja na kupunguza kiwango cha makosa ambayo wangeliyafanya wakati huo.
Ili kuweka kumbukumbu na historia ya nchi hii sawa, daima tutafakari ni kwa nini awamu ya nne 'ilikwepa' mdahalo!???
JK amekuwepo wizara ya mambo ya nje kwa muda mrefu.Waliomteua hawakuliona hilo?Kwasababu kipindi cha nyuma kulikuwepo rumours kwamba ukiwekwa wizara ya mambo ya nje,basi unaandaliwa kuwa rais.

Kukwepa mdahalo, ndo panapoonyesha kwamba ccm si chama cha wananchi tena.

Na kwasababu si chama cha wananchi,inabidi kiwakandamize il kuendelea kuwepo madarakani na kufanya ufisadi bila bugudha.
 
kibamba hapa amekurupuka. Huwezi kukimbilia kwenye jumuiya ya kimataifa kabla hata hujatafuta suluhu ya ndani ikiwa ni pamoja na kutaka ufafanuzi wa kauli au kumtaka aliyetoa kauli aifute. Sasa kila jambo tukikimbilia kwenye jumuiya kimataifa bila kujiridhisha kwamba ni juu ya uwezo wetu si watatuona walalamikaji na kutuchoka mapema? Tanzania hatujafikia mahali pa kuhitaji msaada wa kimataifa kwa matatizo yetu ya ndani.

pesa za wafadhili zinamuwasha
 
Kimekuwa kijiwe cha waganga njaa? Wamiliki wa kituo hiki ni kina nani kwa faida ya nani? Jana walikuwa na jukwaa la katiba? kazi kuongea na hisia bila kuwa na takwimu au tafiti sahihi. njaa itawaua na salaamu pelekeni kwa wafadhili wenu kuwa hatu waamini hata mara moja.
 
Dogo kikwete ICC wamechelewa kumfuata ila Lema pongezi za dhati kwako zikufikie popote ulipo hakuna wa kukutisha kamanda tuko nyuma yenu makamanda japo KIKWETE kasema wajibu mapigo tunawasubiri walianzishe waje waone cha moto kama hataikimbia ikulu asubuhi na mapema
 
Kimekuwa kijiwe cha waganga njaa? Wamiliki wa kituo hiki ni kina nani kwa faida ya nani? Jana walikuwa na jukwaa la katiba? kazi kuongea na hisia bila kuwa na takwimu au tafiti sahihi. njaa itawaua na salaamu pelekeni kwa wafadhili wenu kuwa hatu waamini hata mara moja.

mkuu ,hiki.kituo ni cha kitapeli tu, wanawatapeli sana wafadhili wao
 
Unaweza ukamshtaki kama unataka....au unaweza ukawaconvince wengine wakamshtaki kama wewe huwezi....

Ila hawa wameona Kikwete anastahili kushtakiwa na wamechukua hatua na wameamua kumshtaki ! Ukiua mtu halafu ukashtakiwa hauwezi kujitetea kwa kusema mbona fulani naye aliua hakushtakiwa.....utaonekana kituko !

Kwahiyo BABU anahamasisha fujo na nchi isitawalike kwa sababu yeye sio amiri jeshi mkuu? Jukumu la kulinda tunu ya AMANI na UTULIVU ni la kwetu sote! Kwahiyo hata BABU SLAA inatakiwa akamatwe na kushtakiwa haraka sana!
 
kibamba umemuona kikwete yuleeeee! hivi huyo kibamba alimuulza kikwete kuwa alikuwa anamaanisha nini? wengi mbona wanatoa kauli za namna hyo au znazoendana na hyo. vp wanaosema hapatakalika .......
 
hata shauri kusikilizwa tu THE HAGUE inatosha kumchafulia jina lake kwy jumiya za kimataifa. Rais wa nchi kazi yako kuhubiri Amani na Rule of Law na siyo kikundi kimoja kipige kikundi kingine unaposema hivyo unajishushia uwezo unakuwa kama watu wa mitaani ktk historia ulishawahi kusikia Rais wa nchi akitoa kauli hizi.

Uko sawa ndugu yangu hapa inatakiwa dunia nzima ijue JK si mtu mwema kama wanavy mfikiria wao.
 
Msolwa a.k.a Mburula,

Nilishasema wewe ni failure wa kutupa.
Kwa hiyo kwa uelewa wako wewe ulitaka Rais wako Kiwete aseme moja kwa moja kwamba:.... kuanzia sasa CCM msiwe wanyonge,lazima mjibu mapigo, CHADEMA wakiwamwagia tindikali na nyie wamwagieni,wakiwachoma bisibisi na nyie wachomeni maana uvumilivu una mwisho!!!

Madai yako kwamba hapa Kiwete alikuwa anazungumzia swala la unyonge wa kisiasa kwa maana ya kuhamasisha ushindi kwa CCM,siyo kweli!!!Iweje azungumzie unyonge wakti CCM ndiyo wenye dola na wameshinda viti 23 vya Udiwani na wana zaidi ya 70% ya Wabunge wote???Unyonge upi unaotaka kuuzungumzia hapa????

Wazungu wanasema, ''You can fool some people for sometime,but you cannot fool all people all the time!!!
Msolwa le'me tell you this: Tuko kwenye dunia ambayo kwa sasa mambo yanabadilika kwa haraka sana kuliko unavyofikiri. Usije ukashangaa Rais wako Kiwete akajikuta yuko The Hague! Nawashangaa sana CCM kuendelea kuwafanya Watz mazezeta kwa propaganda za kishxxxnz!
Kila Uchaguzi mnataka mshinde nyie tu! Mkiona chama cha upinzani makini kama CDM na CUF mnaanzisha mizengwe kwa kutumia kila namna ya mbinu ikiwemo KUUA,KUBAMBIKIA KESI,KUTEKA NA KUNG'OA WATU MACHO NA MENO, KUWATUMIA NEC(TUME YA UCHAGUZI) KUIBA KURA,KUVURUGA DAFTARI LA WAPIGA KURA,KUCHAKACHUA SHERIA NA RASIMU YA KATIBA MPYA ILMRADI TU muendelee kuwa madarakani.

Your days are numbered, This is just beggining of a countdown. No sooer than later,the clock shall tick at 0 hour. That will be your end.

Wasaalamu.






Nina hakika wewe si mtu wa pwani, maana inaonesha kabisa hukijui kiswahili vyema. Tafakari kwa makini kauli ya Mh Raisi kabla ya kukurupuka.

Kwa akili yako fupi na finyu unafikiri mtaweza kumpeleka Jakaya The Hague kwa upuuzi kama huu wa kauli msiyoielewa?.
Semeni, imbeni, pigeni na vigelegele hakuna lolote mtakalofanya. Mnapiga makelele tu mwisho wa siku mtalala na kesho mtaamka na story zingine.

Bwana mdogo ni bora utumie muda wako kujitafutia riziki kuliko kutumia muda wako kumshupalia Mh Raisi kwa kutoa kauli ambayo mnashindwa kuielewa.

kama kweli una hasira na kauli ya Mh Raisi nenda polisi, mahakamani kashtaki. Ama andika barua ya malalamiko na ipeleke Ikulu.
 
Katika hili Mwakikibamba nyongise hilo, wimilile ulukani ulu umtemi uyu asindikwe kuvansungu uko,

Nyongise hilo ukugotola ulukani ulu,

Wilonga witigila waivasikisa makadinga. kilikwiya chewiwona apigite cha mana? ngali ingosi zelu ya kukupufya?
 
Back
Top Bottom