Kitu gani ambacho mama yako amekufanyia hutakaa usahau?

Huwa napata tabu sana kila inapofika mwisho Wa mwaka coz my Mom use to call m like Raymond Baba angu happy new year my son...nilikua najickia raha sana so akanitengenezea kitu kama alarm HV yani ntapokea wishes zte lakini bila kusema yy mwaka bdo haujaisha..since 2012 mpaka Leo bdo upo moyoni mwangu... upumzike kwa amani hko ulipo nilikupenda,nakupenda,na nitakupenda cku zte za maisha yngu,Ahsante kwa kunileta duniani!!! Unisamehe kitu kimoja2 nacho ni sikuwahi kukwambia au kutamka kama "nakupenda sana"ni neno dogo lakini ukikosa fursa ya kulisema hakika utajutia maisha yko yte...mm ni mmoja wpo ckuwah kumwambia mama Angu kama nampenda sana thou anajua kama nilikua nampenda kuliko kitu chochote mpaka inafika tym namlilia but kwakweli ckuwah kumwambia live kama nampenda sana so guys ambao mmebahatika kua na Mama zenu pls waambieni kama mna wapenda...ukikosa hyo nafasi ndio utajua umuhim Wa nnachokisema
 
Thread kama hizi zinakufanya urealize how blessed you are. Nakushukuru Mungu kwa neema na zawadi hii kubwa, hadi Leo hii na uzee wangu, bado nipo na mama (na baba), and I'm her best friend. Mungu Uendelee kunitunzia shoga angu yule, hakuna cha kumfanyia ambacho kitafikia upendo na sacrifices zake. Thanks momma HS

Hongera kwa kuwa na wazee wenzako bado.
 
Happy birthday mama Bavaria!

Hayahesabiki wala siwezi kuyahesabu, kitendo cha kuitunza mimba yangu, kunileta duniani na kunilea katika shida na kunifikisha pale aliponifikisha yatosha kusema ahsante mama.
Your the one and no one to compare, nakumiss kila iitwapo leo. Mungu azidi kukupa pumziko la amani....... RIP mama ram!

Pole sana Ram. RIP mama ram.
 
  • Thanks
Reactions: ram
Mamaangu kanifanyia mambo mengi makuu sina budi kumshukuru japo sina zawadi nzuri ya kumpatia ili aridhike na makuzi aliyonukuza mpaka leo hii. Ila kikubwa nampongeza na Kumuombea kwa Mwenyezi Mungu aendelee kumpatia hekima, busara, nguvu na amlinde dhidi ya Watu wabaya aishi kwa amani maisha marefu yenye fanaka.
[HASHTAG]#SophiaNyakwesi[/HASHTAG],M
 
Haya maisha yangu i owe all kwake. Mama yangu ndio Mungu wangu. Alicreate life akanipa uhai, hakuniabort though she was young & with lots happening at the moment. Akanivisha, akanilisha. Akahakikisha nasoma kwenye the best schools amehakikisha nimepata the best education as far as uwezo wake. Amejinyima vingi sana ili mimi niwepo nilipo. Kwahiyo ni ngumu kusema lipi hasa maana kila sekunde moyo unadunda, kila sekunde pumzi inavutwa ni yeye amesababisha.
 
Kunizaa,kunilea si kazi ndogo,huwa ananipa moyo sana kwa kila hatua nayopitia,nakumbuka nilipokuwa mdogo,alikuwa ametoka kazini alafu kachoka aliniambia nifute vyombo nikamkatalia,akanichapa sana,nililia nikasusa kula nilipoenda kulala kumbe alijisikia vibaya akaja chumbani kwangu na kuninyanyua na kunilaza ubavuni mwake,akaanza kunibembeleza huku ananilisha,hakika najivunia kuwa mama jasiri km huyu,kipindi hiko anatuangaikia ili tupate maisha mazuri na huku mzee akiwa km mguu nje,mguu ndani akiwa aweshikiriwa na hawara,hakika mungu amefanya maajabu yake mpaka sasa wazaz wapo pamoja
 
Nikiwa nimemaliza chuo nlienda kaa mkoa tofaut na nyumban kufight ajira na ujasiriamal. Siku moja nlichoka sana kifedha na baht mbaya hata unga na mafuta vilikua vimeisha ndani.. Deal haziendi n naogopa hata kumshtua maza maana nishampiga mixing a sana.. Nkiwa nmekaa sehem natafakar hku nalaum maisha na cjui ntakula nn...ghafla nliona mzigo umeingia kwenye simu.kuangalia n kutoka kwa nama bila kumuomba... Daah sitasahau nililia sana.. Nikaamini kweli.. Baada ya Mungu ni wazazi..tuwaheshimu sana wazazi..ni Miungu wa duniani.
 
Mama yangu amehangaika sana na mimi,nakumbuka nilipokuwa mdogo nilikuwa nasumbuliwa sana na asthma alikuwa akinibeba mgongoni usiku wa manane kunipeleka hospitali.. Siwezi kuyahesabu aliyonifanyia na anayoendelea kunitendea.. Mungu nakushukuru kwa kunipa nafasi ya kupata upendo na malezi ya mama, kwangu yeye ni mama bora.. Nakupenda mama yangu jana leo kesho na siku zote
 
  • Thanks
Reactions: ram
Happy birthday mama Bavaria.
Poleni mlioondokewa na mama zenu.
Nilimfanyia vituko vingi mama yangu kimojawapo nilipokuwa narudi kutoka shule sekondari ya kutwa nikifika home kama alikuwa hajapika msosi nilikuwa nakasirika naongea maneno makali juu yake lakini yeye alikuwa hajibu ananiangalia tu huku akiwa anafanya maandalizi ya kupika,nilikuwa sifikirii kwa sababu na yeye alikuwa ametoka kazini ,lakini Mimi nilikuwa sijali,nilimkosea sana.
Hakuna kama mama nitakupenda daima mama .
 
Rip my mom...huwa natamani ata siku zirudi nyuma
Mungu akulinde uko ulipo..mlio na mama wapendeni sana mana ipo siku utatamani umwone lkn ndo itakua ngumu
Daa ni kweli ndugu upendo na mapenzi ya mama hayana mfano. Mungu awabariki wamama wote popote walipo duniani na sisi watoto tuwapende, tuwaheshimu na kuwatunza maana hakuna kama mama
 
Leo ni siku ya kuzaliwa mama Bavaria.
Huwa nakumbuka mengi kuhusu mama, vimbwanga vyote nilivyofanya nikiwa mdogo.
Ni moja kati ya wanawake 'strong' sijawahi ona. Pamoja na kubanwa na majukumu yote aliyokuwa nayo, ila hakukosa kuihudumia ipasavyo.
Moja kati ya vitu sitasahau, nilikuwa shule ya msingi. Tulikuwa na safari ya shule kwenda makumbusho ya taifa jmosi moja hivi. Kwa jinsi mzee alivyokuwa mkali, sikutaka kumuomba. Nikamtuma mama akaniombee. Mzee akazingua.
Basi asubuhi nimeshajiandaa nikijua lazima bimkubwa amerekebisha mambo. Kumbe la. Wakati najiandaa nikamuuliza bimkubwa akasema mshua amezingua. Nilikuwa dissapointed sana. Ila nikasema lazima niende hata iweje.
Kumbe bi mkubwa alienda kwenye kibubu chake akachukua 5000 anipe. Akaiweka mezani. Nilivyomaliza kujiandaa nikasepa zangu bila hata kuangalia pembeni, nikijua mzee hajaacha mpunga.
Maza alikuwa anachambua maharagwe abandike jikoni. Alivyomaliza akaiweka sufuria mezani juu ya ile hela bila kujua. Baada ya kuwasha mkaa akaweka maharage jikoni akasepa. Hakujua kama ile hela iligandamana na ile sufuria. Ikaungua.
Jioni narudi, maza akaanza kuulizia chenji. Nikamwambia hakunipa hela ila yeye akasisitiza ameiweka mezani. Nikamwambia sikuiona. Akagundua kumbe ilikuwa imegandamana kwenye sufuria, ikaungua.
Niliumia sana siku ile, nililia kwa uchungu mno. Sijui kilichoniliza ila hadi leo nakumbuka kile kitendo.
Huwa nikimwangalia moyoni najisemea i love you mama.
Kuvumilia kuniweka tumboni miezi tisa na kunizaa kwa uchungu,kamwe hakuna kiumbe mwingine duniani ashawahi kunionyesha upendo wa namna hiyo.
 
My Mum is very unique to me, She has been there for me, I remember the day she cried before my eyes baada ya mimi kukosa ada ya kwenda shule nikiwa naingia form three, bahati nzuri nilikuwa nimekwisha kufanya kibarua nikamwambia nimepata nauli mama, akasema baba yako mdogo kakataa kutoa ada just because umekataa kwenda kuchunga. I remember mama yangu nikiwa form five nilikosa nauli ya kurudi nyumbani likizo, alichukua barua kwa mwenyekiti wa kijiji inayomwonesha kuwa ana mtoto ambaye yupo form five, so anaomba msaada amtumie nauli, akapita kila office kuomba msaada wa mchango ili mimi nipate nauli ya kurudi nyumbani, kitendo hichi kiliniuma sana kuliko vyote, she did it and alinitumia nauli nikaja nyumbani, nikamwambia mama kuanzia sasa pumzika usiangaike tena na michango acha nifight mwenyewe, nikamwambia mama nipo na rafiki zangu ambao baba zao wameahidi kunisomesha mpaka form six, Namshukuru Mungu Nilimaliza salama na nimesahau kabisa kama kulikuwaga na matatizo kama hayo. Haya ni matukio muhimu ambayo mama alinifanyia nikiwa mkubwa kabisa achana na yale ambayo ni lazima akufanyie kama mtoto wako. Namshukuru sana Mama yangu Mzazi, Mama yangu ni Mvumilivu sana, Mama yangu ananipenda, Mama yangu sijawahi kumpa pesa akasema ni ndogo na hajawahi kusema nipe pesa shilingi kazaa, yaani hata shilingi 30,000 she is happy. My Mum is everything, she has been there for me in sorrow and happiness, My Mum is A woman I believe, She care for me always as if I am still young............Najua kuna watu watasema what have you done for her, well nilipopata job cha kwanza kabisa nilimjengea nyumba yake kijijini nikamwekea na sola, yupo na wajukuu zake, kila mwaka lazima nihakikishe hamna adha ya chakula hata kidogo, matumizi anapata kila akiishiwa anasema, Namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunipa such a kind of Mama, Amekuwa Baraka kwangu na kwa Wengine, Mungu aendelee kuwapa afya akina Mama wote! Biblia inasema waheshimu baba na mama ili siku ziwe nyingi, yet Quran inasema pepo yetu ipo kwenye nyayo za mama zetu. I Bless every woman at JF.
Von Mo.
 
Ameen!!asante sana!
Nimekulia na mama mlezi for 24yrs!!wanangu sitakubali walelewe na mtu yoyot labda nife mapema!
Nataka wapate Yale ambayo Mimi sikuyapata kwa mama angu!!
Thats my wish too, tuombe uzima tu.
 
Back
Top Bottom