Kitu gani ambacho mama yako amekufanyia hutakaa usahau?

Bavaria

JF-Expert Member
Jun 14, 2011
53,102
53,353
Leo ni siku ya kuzaliwa mama Bavaria.
Huwa nakumbuka mengi kuhusu mama, vimbwanga vyote nilivyofanya nikiwa mdogo.
Ni moja kati ya wanawake 'strong' sijawahi ona. Pamoja na kubanwa na majukumu yote aliyokuwa nayo, ila hakukosa kuihudumia ipasavyo.
Moja kati ya vitu sitasahau, nilikuwa shule ya msingi. Tulikuwa na safari ya shule kwenda makumbusho ya taifa jmosi moja hivi. Kwa jinsi mzee alivyokuwa mkali, sikutaka kumuomba. Nikamtuma mama akaniombee. Mzee akazingua.
Basi asubuhi nimeshajiandaa nikijua lazima bimkubwa amerekebisha mambo. Kumbe la. Wakati najiandaa nikamuuliza bimkubwa akasema mshua amezingua. Nilikuwa dissapointed sana. Ila nikasema lazima niende hata iweje.
Kumbe bi mkubwa alienda kwenye kibubu chake akachukua 5000 anipe. Akaiweka mezani. Nilivyomaliza kujiandaa nikasepa zangu bila hata kuangalia pembeni, nikijua mzee hajaacha mpunga.
Maza alikuwa anachambua maharagwe abandike jikoni. Alivyomaliza akaiweka sufuria mezani juu ya ile hela bila kujua. Baada ya kuwasha mkaa akaweka maharage jikoni akasepa. Hakujua kama ile hela iligandamana na ile sufuria. Ikaungua.
Jioni narudi, maza akaanza kuulizia chenji. Nikamwambia hakunipa hela ila yeye akasisitiza ameiweka mezani. Nikamwambia sikuiona. Akagundua kumbe ilikuwa imegandamana kwenye sufuria, ikaungua.
Niliumia sana siku ile, nililia kwa uchungu mno. Sijui kilichoniliza ila hadi leo nakumbuka kile kitendo.
Huwa nikimwangalia moyoni najisemea i love you mama.
 
Kuna wakati hatukua na hausgeli. Akiwa anarudi home hata awe amechoka vipi, atahakikisha anafanya kazi zake zote bila tatizo.
Huwa napata picha jinsi leo hii nikirudi nyumbani nnavyokuwa nimechoka ila yeye anafanya yote bila shida.
Ikabidi tugawane shughuli. Nikapewa kitengo cha upishi. Hahahahahaha nilikuwa natoa maboko ya hatari. Ila watu walikuwa wanakula bila shida. Na hakuna anayehoji.
 
Leo ni siku ya kuzaliwa mama Bavaria.
Huwa nakumbuka mengi kuhusu mama, vimbwanga vyote nilivyofanya nikiwa mdogo.
Ni moja kati ya wanawake 'strong' sijawahi ona. Pamoja na kubanwa na majukumu yote aliyokuwa nayo, ila hakukosa kuihudumia ipasavyo.
Moja kati ya vitu sitasahau, nilikuwa shule ya msingi. Tulikuwa na safari ya shule kwenda makumbusho ya taifa jmosi moja hivi. Kwa jinsi mzee alivyokuwa mkali, sikutaka kumuomba. Nikamtuma mama akaniombee. Mzee akazingua.
Basi asubuhi nimeshajiandaa nikijua lazima bimkubwa amerekebisha mambo. Kumbe la. Wakati najiandaa nikamuuliza bimkubwa akasema mshua amezingua. Nilikuwa dissapointed sana. Ila nikasema lazima niende hata iweje.
Kumbe bi mkubwa alienda kwenye kibubu chake akachukua 5000 anipe. Akaiweka mezani. Nilivyomaliza kujiandaa nikasepa zangu bila hata kuangalia pembeni, nikijua mzee hajaacha mpunga.
Maza alikuwa anachambua maharagwe abandike jikoni. Alivyomaliza akaiweka sufuria mezani juu ya ile hela bila kujua. Baada ya kuwasha mkaa akaweka maharage jikoni akasepa. Hakujua kama ile hela iligandamana na ile sufuria. Ikaungua.
Jioni narudi, maza akaanza kuulizia chenji. Nikamwambia hakunipa hela ila yeye akasisitiza ameiweka mezani. Nikamwambia sikuiona. Akagundua kumbe ilikuwa imegandamana kwenye sufuria, ikaungua.
Niliumia sana siku ile, nililia kwa uchungu mno. Sijui kilichoniliza ila hadi leo nakumbuka kile kitendo.
Huwa nikimwangalia moyoni najisemea i love you mama.[/QUOT

Mkuu ukweli ni kwamba MIUJIZA ya MAPENDO wafanyayo Mama kwa sisi watoto wao yananifanya nishindwe kusema IPI NI SPECIAL!! Yote aliyomifanyia Mama(including kichapo kama paka mwizi pale nilipokuwa nafanya ndio sio).......ni THE BEST EXPERIENCE.

Asante Mama kwa kuwa Mama yangu mpendwa
 
Nakumbuka kuna siku we had a fight na kaka. Yangu nikawa na hasira mpka Mishipa imensimama akaniita akanipa Maji ya. Barid then akanilaza miguun after a while hasira zote zmeisha sjui yalikua ni yale Maji au kulala miguun but nakumbuka sana hiyo moment
R.I.P Huko ulipo mama!
 
Back
Top Bottom